PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NAUFUNGA MDOMOWANGU

NAUFUNGA MDOMOWANGU
NAUFUNGA MDOMO WANGU

MY LIFE SOMA HAPA


Mimi mwenyewe 'live'

Naitwa John Kitime, nilianza kufurahia vichekesho mara baada ya kuzaliwa na kukuta watu wazima kila wakinichukua walijitahidi kunichekesha kwa kuanza kuonea lugha ambayo sijaijua mpaka leo, maana mara alikuja mmoja na kuanza ‘bujibujibujibujibuji,jigijigjigjigjijij, grugrugrugru’ na maneno mengine ya ajabu nilijitahidi kuwavumilia nisiwacheulie maziwa lakini baadae nikagundua heri niwe nacheka wakianza vituko hivyo, maana baada ya hapo walikuwa wanajiona wanajua kuchekesha watoto wachanga.Niliendelea kukua nikaanza shule nakukuta vituko vingi sana vya kuchekesha, kama vile  watu kujikojolea darasani, hili bahati mbaya nililikuta linajirudia pia kuwakuta wakubwa wakijikojolea kwenye baa, na kilabuni, ene way, nilimaliza shule na kujiunga na vyuo mbalimbali nchini na huko nilijifunza utalaamu wa kunywa pombe na huko nilikutana na watu wengi wenye kujua kuchekesha, kucheka na hata wasiojua kuchekesha wakijitahidi kuchekesha , cha kushangaza si nikakuta wengine hawajui kucheka kabisa, au wanaweza kucheka mahala pasipo na kichekesho cha kuchekesha wachekaji.
Katika kiota hiki ntaweeleza mengi yaliyonikuta katika maisha yangu haya yaliyojaa furaha sana NAMSHUKURU MUNGU.
Pia mimi ni mwanamuziki napiga gitaa naimba kwenye bendi, lakini huwa sichezi, sijui kucheza, hasa Chacha ndio kabisa halafu siku hizi kuna hii inaitwa Kwaito, wakati najitahidi kujifunza imeanza Kiduku, sijaishika sawasawa imekuja Kibajaji heee jamani si mngoje japo nijuwe staili moja ndio mbadili? Halafu huwa inanishangaza, mtu analipa kuingia muziki halafu anacheza kuliko sisi wanamuziki jamani, mnajua mngepewa majembe mlime badala ya kucheza mngesha maliza tatizo la njaa hapa nchini?

J F K

Comments

Anonymous said…
hahahaha daah Wallah ni saa sita na dakika 40 usiku nacheka mpaka machozi yanantoka kisa Biography yako Mzee Kitime haswaa ending party daah haya Mzee u made ma 9t
Anonymous said…
Sasa basi ya kwangu ni ilikuwa kali. Nakumbuka nikiwa mdogo,godfather wasngu alifika nyumbani. Akaninyanyua juu na akaanza kunichezea. Nilikuwa sijavaa kaptula. Basi mzee wa watu akajifanya anataka kukata kalamu yangu kwa meno kisa nisisahau kuvaa kaptula tena. Kwa hofu misuli ilajiachia na mzee akanyweshwa kisichonywewa. Hdi leo ananikumbushia yaliyojiri zaidi ya miaka arobaini iliyopota
Anonymous said…
Mzee Kitime,nashukuru kwa post zako kwani zimenifanya niongeze siku za kuishi. Ubarikiwe saaaana!!!
Anonymous said…
Duh!!!! Tangu nikufahamu wewe kama mwanamziki maarufu sikuwahi hata siku moja dhani eti utakuja kuwa msanii wa sanaa ya ucheshi. Kwa kweli hongera sana Mzee mi nakuahidi kuwa fisadi maarufu wa vichekesho vyako kwa kuvi copy paste kwa profile, groups pages na blogs zingine. Wah!!!! Umetisha kama nyoka chatu mwenye vichwa viwili yaani msani wa muziki na msanii wa ucheshi, nimecheka hadi wenzangu ofisini wananiona nimekuwa akili punguani.
Anonymous said…
haahahaha aisee we nikiboko nilikuwa bored hapa ila nimecheka hata bila kupenda,we nimkali.
Anonymous said…
thanx kitime wazidi kunipa burudani God bless u
DAVID KULWA said…
Kaka heshima yako kichwa kilikuwa kuinauma sasa kimepona ahsante sana endeleaa kaka
Ester Ulaya said…
hahahhahaha duh, nimecheka mnoo
JFK said…
Ester Europe, why is you laughing my life? Eh Whyyyy? I am living this life and you are laughing why?