PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NAUFUNGA MDOMOWANGU

NAUFUNGA MDOMOWANGU
NAUFUNGA MDOMO WANGU

KIDUME HAKIKIMBII ISHU NDOGONDOGO WEWE


Aise wiki hii ngumu sana kwa rafiki yangu mmoja, haonekani wala hajulikani aliko, simu yake kazima, vijiwe vyote haonekani, sijapata wasiwasi wa kutaka kwenda kutoa ripoti polisi kwani najua ni mzima ila ndio kapotea. Baba zima likipotea halafu sio ndugu yako unaendaje polisi kulalamika, unaweza ukajikuta wewe unapumzishwa maana sio siri vituo vingi vya polisi kuingia bure kutoka ni ishu nyingine. Hakafu jamaa nilihisi atapotea siku kama nne hivi kabla, maana alianza kudai kuwa simu yake eti mbovu haipokei meseji na mtu akimpigia spika mbovu. Nikajua kuna kitu anakwepa, maana namjua ana simu tatu na zote zina ni zile zenye laini mbili sasa zitakuwaje zote zimepata ugonjwa sawa?. Jamaa tumemzoea ni mjanja mjanja sana mwenye stori nyiiingi, lakini ghafla tukaona kawa mpole sana, ukiwa nae anaonekana yuko mbali, kwanza tukajua labda kafiwa au kapata barua nzito toka kwa wazazi wake, kumbe bwana ameitwa Ilala. Yaani katika siku chache za karibuni ukisikia mwanaume unaitwa Ilala,moyo unaanza kwenda mbio, unasikia kizunguzungu, mara nyingine miguu inakufa ganzi basi ni shida tu. Siku za nyuma jamaa yangu alikuwa kila mara akitamba kuwa yeye ni kidume cha mbegu, na kwa kutuhakikishia alikuwa anatembea na picha za watoto sita aliokuwa anajisifu walitokana na kazi yake mahiri. Kwa kweli hatukuwahi kumuuliza hao watoto wako wapi, maana tulitegemea kidume cha mbegu kinajua kutunza matokeo ya kazi nzuri, kumbe jamaa alikuwa akijua tu kazi aliyofanya imepata matokeo anahama mtaa. Sasa kuna wadada sita wameenda kulalamika Ilala, kila mmoja akienda kwa wakati wake bila kujua kuna wenzie wametangulia. Na ndipo  ukaanza wito mfululizo ukimtaka jamaa yangu ahudhurie mazungumzo Ilala,  kidume cha mbegu kawa mpole na mnyonge hata ukimtia masinge anakuangalia tu. Hahahaha. Sasa hajulikani aliko. Najua atasoma tu ujumbe huu maana huwa hakosi gazeti hili. Aise chalii yangu we rudi tu ukutane na janga lako ndipo litaisha maana utakimbia mpaka lini? We si kidume bwana kidume hakikimbii ishu ndogondogo kama hizi hahahahahahahahah

Comments