PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NAUFUNGA MDOMOWANGU

NAUFUNGA MDOMOWANGU
NAUFUNGA MDOMO WANGU

PESA MWANAHARAMUUU


Binti mmoja alitoroka kijijini kwao na kukimbilia mjini kutafuta maisha, akarudi kwao baada ya miaka mitano. Na muda wote huo alikuwa kimya hakuandika barua wala kutuma ujumbe. Siku hiyo ghafla akarudi kijijini akiwa kwenye gari jipya zuri sana. Mtu wa kwanza kukutana alikuwa baba yake ambaye wakati huo alikuwa anatoka kilabuni kunywa pombe. Ile kumtambua tu binti yake ambaye wakati huo kajichubua  kavaa nywele bandia, mzee akamcheki kisha akaanza  kumpa vipande vyake  ‘We mwanaharamu umeondoka hapa kwa miaka mitano hukutaka kutuandikia barua wala kutuma salamu unajua ulimtesa sana mama yako?’ Binti kajiumauma kasha akamjibu baba yake,’ Baba unajua niliona niwe kimya maana kazi niliyokuwa nikifanya msingefurahia’. Baba yake akauliza ‘Kwani ulikuwa unafanya kazi gani hiyo ambayo tusingeifurahia na wewe ndiye binti yetu?’ Binti akajibu huku anaangalia chini, ‘Baba nilikuwa nafanya kazi ya umalaya’. Duhh mzee akawa mbogo mara dufu, ‘Unasema nini we mwendawazimu? Yaani ulikuwa huko mjini unalitia nuksi jina la ukoo wetu na kijiji chetu? nakuambia hivi geuka sasa hivi urudi ulikotoka, mimi ntainuaje uso wangu hapa kijijini?’ Binti akamwambia baba yake, ‘Sawa baba ntaondoka ila kuna zawadi  nimeleta naomba niziache. Nimemletea mama sanduku la nguo na kanga 20 na pesa kidogo milioni tatu. Na wewe baba nimekununulia hilo gari nililokuja nalo na nimekufungulia akaunti ina milioni kumi, na ntakuwa naongeza kila mwaka ili isipungue, utaweza kupumzika kulima sasa, na ntakujengea nyumba nyingine ya kisasa’ Mzee alikuwa kama kapigwa shoti, pombe yote ikamtoka akabaki mdomo wazi anamwangalia tu binti yake. Akili ilipomrudia akamuuliza binti yake, ’Mwanangu mpenzi ulisema ulikuwa unafanya kazi gani mjini?’ Binti akajibu ‘Samahani baba nilisema kuwa nilikuwa nafanya kazi ya umalaya’. Mzee akachekaa saana na kusema, ‘Unajua sikukusikia vizuri ndio maana nilikasirika. Eti nilisikia umesema ulikuwa unafanya kazi ya uyaya, ndio nikasema binti yangu mzuri kwanini afanye kazi ya kulea mtoto wa mtu? Karibu nyumbani mwanangu mpenzi’
Chezea pesa wewe

Comments