PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NAUFUNGA MDOMOWANGU

NAUFUNGA MDOMOWANGU
NAUFUNGA MDOMO WANGU

JANUARI ISIKUZINGUE, KUCHEKA BADO RUKSA CHEKA NA KITIME....eti Yanga yakata pumzi .....

 Iko siku kuna mtu atakula makwenzi, hebu kwanza tukumbuke hesabu za mafumbo, sasa ukichukulia kila mpenzi wa Yanga akikukongota kwenzi moja tu, hiyo ni sawa na mikwenzi milioni kadhaa, Je itachukua siku ngapi kukamilisha kukutia mikonzi? na je utahitaji siku ngapi kupona? Ukishajua hesabu hiyo ndio uanze kusema jamaa wamekata pumzi, we timu bado fiti unadai imekata pumzi? Unajua kukata pumzi wewe? 


 Yatakuwa madudu gani tena? Isije ikawa majongoo, sasa majongoo yameingiaje posta? Au kuna mtu kayaposti kutoka nchi za nje? Eneweyi kwa vile yameibuliwa najua yatabebwa na kutupwa baharini, posta zetu ziwe safi tena.


 Hahahahaha kuna wimbo wa Dar Jazz wa zamani enzi za wahenga, unasema hivi;
Yamewafika wenzetu,
Kila wakitaka kujitahidi ohh
Mambo yanawashangaza
Watafanya jambo gani ohh
Aise huu wimbo saizi yao wenzetu, wamelikoroga hasa, ikifikia Rais wenu mnampima akili kama yuko fresh ina maana anafanya mambo wanayofanya wasio fresh. Watoto wa mjini wanawaitaga 'chizi fresh'.  Wahenga walishasemaga kuchamba kwingi......... Ngoja niimbe kawimbo ketu ...Yamewafika wenzetu........

 Wafanyakazi wa blogu hii wanahusika, maana mambo yao hayaeleweki, we fikiria kuchambua gani magazeti huku? Ni wazi vyeti vyao feki, sasa tatizo bosi wao nae feki, sasa panya feki gani amvishe paka feki, kegele feki?

 Watumie tu dawa, kuna dawa nyingi za presha ya kupanda. Nawashauri wasitumie kahawa wala koka. Wapende kujipumzisha, wasitumie chumvi, inapandisha sana presha. Kama mwananchi mwenye nia njema naona nami nimetoa ushauri, naomba kupigiwa makofi kwa uzalendo tafadhali, piga makofi, piga makofi, piga makofi  tafadhali

 Naogopa kuchambua hii habari, imekaa kama vile polisi ndio wanavaa mavazi mafupi. Zamani ni kweli walikuwa wanavaa kaptura, sasa siku hizi wanavaa suruali hapo ndipo panaponiletea utata kuhusu wao kuvaa nguo fupi. Halafu si mnawajua wale hawapendagi utani,, sasa ishu ya nguo zao inaweza ikanikosti. Halafu sijajua Tibaijuka yupi aliyewaibukia. Ngoja ninyamaze sasa. Maana yake hii kitu iko vere kontrovesho

 Why? Kwanini wasije Dar baada ya 2020, kwani paspot zao ni za wapi? Yaani hapa sielewi kabisa kabisa, Mtz halafu ukatazwe kuja Dar? Au ni wabunge wa Kenya?

 Mkuu tafuta pafyumu haraka, ukiona watu wameshakushtukia kuwa unatoa kaharufu kengine sio freshi. Unajua ukikaa karibu na mbuzi utanukia mbuzi, ukikaa karibu na simba utanukia simba, ndio maana wazungu wakatengeneza pafyumu, so ni ushauri tu, zamani tulikuwaga na pafyumu kama Odorono, Lady Gay, Fa kwa hiyo sisemi zaidi najua umenipata.

 No no no jamani yaani kombe tu mnataka kufanya mapinduzi? Siku hizi hiyo kitu haikubaliki, Mataifa yote hayatawaunga mkono, kila kitu kinafwata demokrasia. Sasa badala ya mapinduzi litafutwe suluhisho la amani ili kombe lirejee. Unajua sie wengine tuna akili sana za kidiplomasia

 Yaani kivipi? Ulaya kuna mambo heri kwetu, kuna watu wanalala kwenye mitaro, hawajui watakula lini na wapi so najiuliza Ulaya kivipi?

 Aise hiyo chama ngoja niisake, sio vyama vyetu havitoi hata senti tano tena vinataka eti sie ndio tulipe ada ili visavaiv.Yaani dah wakuu mwenye namba ya hawa jamaa naomba pliz.

 Baba, mzee, mukulu,  Bonjuu nisikilize kiduchu soka la Bongo sio la Afrika, tofauti kabisa. Sasa usiseme sana kaa nao miezi miwili ndipo useme , huku soka lake ni la kistaili yake, huku kila mtu mtaalamu, hata teja barabarani anaweza kubishia timu uliyopanga akakupangia yake, na akapata watu wakamuunga mkono we ukaonekana huna maana, huku mkataba sio ishu, saa yoyote wakilianzisha kesho yake unapanda tiketi kwenda kwenu. Siri ya huku ni moja tu, fungwa na timu zoteeee, usifungwe na yanga

 Sasa nimehamia mtaa wa saba, unakumbuka wimbo huo? Mbaraka alikuwa anasema kule alikokuwa kulikuwa na paka wanalia usiku kucha darini, kazini kafukuzwa, shida tupu, akahamia mtaa wa saba. Sasa Yanga umebakia kwanini mtaa wa tano?

Niwatafsirie wale ndugu zangu wanaojua Kiswahili na Kifaransa tu.....JPM ATEMA MOTO GHARAMA ZA SHULE.....sijui nijidai kuchambua .... ngoja nikanywe chai kwanza ntarudi subirini...................

Comments