HATUPIMI BANDO

24 February 2017

UKIINGIA SUPAMAKETI UTAKUTANA NA WATU HAWA


Aina za watu utakaokutana nao kwenye supa maketi siku hizi
1. Wapiga picha- Hawa hawanunui chochote cha maana, kiukweli wanakuja supamaketi kupiga selfi na kisha kuishia kununua maji ya shilingi 500.
2. Wanunuaji wadogowadogo- Hawa hununua vitu ambavyo vinapatikana hata kwenye vigenge mtaani kwao. Hawa hununua mkate, biskuti, soda sukari na kadhalika. Kiukweli hawa huwa wanataka kuonekana wamenunua kitu supamaketi, hakuna la ziada.
3. Wakagua bei- Hawa huzunguka na kuangalia bei ya kila kitu kona zote za supamaket lakini hawanunui chochote. Na hawachoki, kwa wiki mtu anaweza kuingia supamaketi hata mara nane na kukagua bei za TV, friji, Washing machine, sub woofer, baiskeli za mazoezi, cornflakes, makochi

4. Wanunuaji sugu- Hawa ni wale ambao anaingia supamaketi akiwa hajui hasa atanunua nini lakini huishia kununua vitu kibao. Hawa pia huingia baa kunywa lakini kila machinga anaepitisha kitu wao hununua, hivyo mpaka akishalewa unakuta pia kanunua sufuria mbili, kanda mbili, kitabu, sahani za plastiki, ndoo, fagio, mto, redio, dvd, taulo, shuka......No comments: