HATUPIMI BANDO

25 February 2017

SIOI TENA 'WAKUNYUMBA'

Naomba nikiri simlaumu mtu, walinikanya wakanambia niachane na hawa watani zangu 'wakunyumba', nikabisha. Nikapata mrembo mzuri sana nikawataarifu ndugu kuwa nataka kumuoa, wakanikanya sikusikia sasa leo nimerudi na rafiki zangu toka mpirani, timu yetu imeshinda, akatangaza anataka kutupikia wali wa nazi ili tufurahi. Mambo ndio hayo pichani. Sasa nimekubali namrudisha kwao  aolewe na wakunyumba wenzie.

24 February 2017

JE UNA MPANGO WA KWENDA SALUNI WIKI HII, CHAGUA STAILI YA KUTOKEA HAPA


UKIINGIA SUPAMAKETI UTAKUTANA NA WATU HAWA


Aina za watu utakaokutana nao kwenye supa maketi siku hizi
1. Wapiga picha- Hawa hawanunui chochote cha maana, kiukweli wanakuja supamaketi kupiga selfi na kisha kuishia kununua maji ya shilingi 500.
2. Wanunuaji wadogowadogo- Hawa hununua vitu ambavyo vinapatikana hata kwenye vigenge mtaani kwao. Hawa hununua mkate, biskuti, soda sukari na kadhalika. Kiukweli hawa huwa wanataka kuonekana wamenunua kitu supamaketi, hakuna la ziada.
3. Wakagua bei- Hawa huzunguka na kuangalia bei ya kila kitu kona zote za supamaket lakini hawanunui chochote. Na hawachoki, kwa wiki mtu anaweza kuingia supamaketi hata mara nane na kukagua bei za TV, friji, Washing machine, sub woofer, baiskeli za mazoezi, cornflakes, makochi

4. Wanunuaji sugu- Hawa ni wale ambao anaingia supamaketi akiwa hajui hasa atanunua nini lakini huishia kununua vitu kibao. Hawa pia huingia baa kunywa lakini kila machinga anaepitisha kitu wao hununua, hivyo mpaka akishalewa unakuta pia kanunua sufuria mbili, kanda mbili, kitabu, sahani za plastiki, ndoo, fagio, mto, redio, dvd, taulo, shuka......23 February 2017

BANGI MBAYA USIONJE OHOO


Kutumia dawa za kulevya sio ujanja kabisaaa. Ni mtego ambao ukiingia kutoka sio rahisi. Dawa za kulevya zina haribu kabisa taratibu za maisha, vijana wengi hawataweza tena kufikia kiwango chao cha mafanikio katika maisha kutokana na kuingia katika janga hili, kwani malengo ya maisha hubadilika kukawa na lengo moja tu, nalo ni kupata pesa tu ya kununua dawa nyingine ili kulewa tena na tena. Usikubali kuingia katika mtego wa dawa za kulevya.

Ila vituko vya watumiaji wa dawa za kulevya ni vingi mno. Wakati niko sekondari kuna mwenzetu mmoja alifanya maajabu makubwa. Ilikuwa ni wakati wa mapumziko ya saa nne asubuhi, akawakuta rafiki zake wako chooni wanavuta bangi nae siku hiyo akaona aonje huo moshi. Mwanzo hakuona tofauti yoyote mpaka pale alipoingia darasani. Akiwa kimya anafuatilia masomo mara akahisi kuwa kuna siafu wameingia ndani ya shati lake, akapiga ukelele na kuanza kuvua shati huku akilalamika ‘Siafu siafu’. Darasa zima tukashtuka na kuanza kumuangalia, alipomaliza kuvua shati akilalamika kuhusu siafu ambao sie wengine tulikuwa hatuwaoni ghafla akadai wamehamia kwenye suruali na kuivua suruali, ilichukua muda mfupi wenzie aliovuta nao bangi wakatambua kuwa kuwa ni matokeo ya bangi, si ndipo minong’ono ya bangi ikaanza kuzunguka darasani watu wakaanza kucheka badala ya kumhurumia. Ndugu yetu akatimka nje ya darasa kukimbia siafu aliokuwa akiwaona yeye peke yake. Suruali na shati akiwa kaviacha darasani. Wanafunzi waliokuweko nje wakaanza kumfukuza na hatimae kumkamata, wakati huo akawa kabadili maneno, akawa analalamika kuwa mawingu yanashuka. Akawa na anaangalia juu na kulalamika kuwa mawingu yanashuka yatamgandamiza. Shule nzima ilikuwa imepata habari kuwa mwenzetu kavuta bangi sasa inamletea aluweluwe. Akapelekwa kwa mwalimu mkuu huko akabadilika, akaanza kumkumbatia mwalimu mkuu aliyekuwa mama mtu mzima na kudai ni valentine wake wa siku nyingi. Ilikuwa kazi mwalimu kujaribu kujinasua kwa kijana ambaye alikuwa kavaa bukta tu  aking’ang’ania kuwa anamkumbatia valentie wake. Hatimae akafungwa kamba mikono nyuma japo aliendelea kucheka na kudai mambo mbalimbali mara akijitetea kuwa yeye ni Rambo na ataweza kujifungua mara alalamike kuwa yeye mfungwa wa kisiasa. Ila jambo moja ni kuwa kuanzia siku ile aliapa hataonja tena dawa za kulevya za aina yoyote maishani mwake.

15 February 2017

11 February 2017

MIZIMU ITAAMUA


Teknolojia mpya zinatufanya tuwe watu wa ajabu ajabu. Unaweza ukaingia hotelini watu wanakula lakini mkono mmoja wameshika simu, wako bizi wanachati, hapo ndipo uatashangaa mtu kashika tonge la ugali mkononi lakini halipeleki mdomoni wala halishushi liko hewani tu, akili yote kwenye simu halafu anacheka peke yake. Kuna wajinga wengine wanavaa iafon masikioni, wakiwa wamefungulia muziki mkubwa wanatembea barabarani wanakoswakoswa na magari kama vile hawasikii honi, uchizi mtupu. Juzi sinakaingia ofisi flani nilikokuwa na shughuli nyeti, kama kawaida nikamkuta mdada ambaye ndie anaruhusu watu kumuona bosi au la, mdada alikuwa nyuma ya bonge la kompyuta. Nikamuuliza, ‘Bosi yupo?’ Bila kuniangalia sura akasema subiri kidogo’ Nikakaa kwenye makochi mazuri napigwa na kiyoyozi. Nikaanza kusoma soma vijigazeti mpaka nikavimaliza, nikainuka kumucheki yule mdada kuona kama kamaliza kazi yake anisikilize, nikawa nashangaa, alikuwa bizi sana kwenye kompyuta yake, mara atabasamu, mara anune, mara asonye. Nikajaribu kumkumbusha tena kuwa nipo akanijibu kwa ukali , ‘Huoni niko bizi, nimesema subiri, we mzee vipi?’ Nikawa mpole. Kwa bahati bosi akatoka, kuniona tu, akaanza, ‘Shikamoo mzee, loh mbona hujanambia uko hapa samahani sana mzee wangu ningejua uko hapa ningekwisha kutoka’. Yule mdada kuona bosi wake kawa mdogo vile ndipo akagundua kumbe kisha likoroga. Bosi wake akamuuliza, ‘Kwanini hukumruhusu huyu mzee kuniona?’ wakati huo akazunguka kuangalia mdada alikuwa na afanya kazi gani. ‘Yaani we uko kwenye fesibuku Mzee wangu umemchelewesha kuingia, unajua kuwa mali yote hii nilipata kwa hirizi za huyu mzee?’ Bosi akanigeukia mimi, ‘Mzee wangu kosa ni la huyu binti mi siwezi kukuvunjia heshima, unanijua toka niko mdogo sijawahi kukuvunjia heshima mzee wangu nisamehe’. Nikamuangalia yule binti kisha nikajibu tu ‘ Usiwe na wasiwasi kijana wangu nimekusamehe, ila kuhusu huyu binti ntakapozungumza na mizimu leo usiku ndio ntaambiwa cha kufanya, kama nimuoe au awe sadaka ntapata jibu kwa mizimu’ Kwa jinsi uso wa yule binti ulivyokuwa, sidhani kama atamdharau mgeni atakaekuja kuja pale tena.