HATUPIMI BANDO

29 December 2016

LEO KATIKA UKUMBI WA KING SOLOMON'S HALL NAMANGA USIKOSE MAMBO HAYA

Utakosaje?Tiketi zinapatikana sasa EATERS POINT Namanga na Masaki. Tiketi za VIP Zimebaki chache. Pia tiketi zitauzwa mlangoni kuanzia saa mbili usiku. Njoo usikilize muziki tofauti na kucheza mpaka usiku mkali
You can't miss this.Tickets are available at EATERS POINT Namanga and Masaki. Limited VIP Tickets. Tickets will also be sold at the door from 8pm. Come and enjoy different varieties of music and dance tour heart out
JOHN KITIME &WAHENGA BAND

JOHN MHINA & THE TANZANITES

TAJ MBARAKA MWINSHEHE


MUSIC MAYDAY ARTISTS

13 December 2016

NYIE MUTU YA KENYA HII NDIO PHOTOSHOP NI GANI?


UKINYIMWA UNYUMBA KASHTAKI POLISI


Na Dotto Mwaibale

WANANDOA wanaojimwa ujumba na wenza wao wametakiwa kwenda kushitaki dawati la jinsia yaliyopo vituo mbalimbali vya polisi ili kupatiwa utatuzi wa changamoto hiyo.

Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Felix Lyaniva wakati akizindua maonyesho ya dawati la jinsia na watoto katika viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam leo ambayo yalishirikisha wadau mbalimbali kutoka Hospitali ya Amana wilayani Ilala na wananchi.

"Ukatili wa kijinsia si kupigana na kutukana hata mume na mke wakinyimana unyumba pia ni ukatili wa kijinsia hivyo anayejimwa hasione aibu aende kushitaki dawati la jinsia katika kituo chochote cha polisi" alisema Lyaniva.

Lyaniva aliwataka wananchi wanao fanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenda kwenye dawati hilo kupata ushauri kutoka kwa maofisa wa polisi waliopatiwa mafunzo ya kutatua changamoto hiyo.

Katika hatua nyingine Lyaniva aliwaagiza maofisa wa polisi wa dawati hilo kutotoa nje siri za watu wanaopeleka malalamiko yao katika dawati hilo kwa kufanya hivyo ni kukiuka utaratibu wa kazi.

Aliwaasa wanandoa kuwa na mshikamano na upendo ili kuwa na familia bora na yenye maadili jambo litakalosaidia kutokuwepo kwa watoto waliokosa maadili na kujiingiza kwenye makundi ya kiovu kama panya road.

Lyaniva aliwaomba wanawake pale wanapopata mafanikio ya maisha kupata fedha au kupanda vyeo kuacha kuwadharau waume zao ili kuepusha kuvinjika kwa ndoa zao.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Temeke Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Gilles Muroto amewataka wananchi wasiogope kwenda kutoa taarifa za ukatili wa kijinsia katika vituo vya polisi kwani malalamiko yao yatasikilizwa kwa faragha na maofisa maalumu wa jeshi hilo.

Maonyesho hayo yamedhaminiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa (UN).
 Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Felix Lyaniva (katikati), ambaye alikuwa mgeni rasmi akihutubia wakati akizindua maonyesho ya dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Temeke viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Chang'ombe (OCD) Msuya, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Lucy Tesha, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Gilles Muroto na Kamishna Msaidizi wa Polisi, Vedastus Chambu kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini.

 Mkuu wa Wilaya ya Temeke,  Felix Lyaniva (Wa pili kushoto), akikata utepe kuashiria uzinduzi wa maonesho wa  maonyesho ya dawati la jinsia na watoto Wilaya ya Temeke katika viwanja vya Mwembe Yanga Dar es Salaam leo asubuhi. Kutoka kulia Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Chang'ombe (OCD) Msuya, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Vedastus Chambu kutoka Kamisheni ya Polisi Jamii Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Nchini, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACP), Gilles Muroto na Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Lucy Tesha.

 Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa (UN), Lucy Tesha akihutubia kwenye uzinduzi huo.
Viongozi mbalimbali wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Wadau na wananchi wakifuatilia hutuba za mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva.

Maofisa Wanawake wa Jeshi la Polisi  Dawati la Jinsia wakiwa kwenye Maonyesho hayo. 


 Wananchi na wadau wengine wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi
 Wananchi na wadau wengine wakiwa kwenye maonyesho hayo.

 Mrakibu wa Jeshi la Polisi, (SP), Faidha Suleiman (kushoto), ambaye anashughulikia dawati la jinsia Makao Makuu ya jeshi hilo akimkabidhi Mgeni rasmi DC wa Temeke machapisho mbalimbali ya ukatili wa kijinsia ikiwemo miongozo ya uanzishaji wa dawati la jinsia na watoto ndani ya jeshi hilo.
  Mrakibu wa Jeshi la Polisi, (SP), Faidha Suleiman (kushoto), akimuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Temeke kuhusu kazi kubwa inayofanywa na jeshi hilo kwenye idara ya dawati la jinsia.
Wananchi wakipata machapisho mbalimbali.

10 December 2016

NDOA BILA SENDOFF ETI SIO NDOA

Unajua hapa Bongo kuna watu wakorofi sana, kuna watu wanajifanya wao wako kama serikali. Yaani wakisikia chochote kimefanywa na serikali na wao wanataka kufanya pia, sijui wakoje? Tabu yake mambo wanayofanya ndio yale wastaarabu wanaita kudandia treni kwa mbele, mambo ya uchizi uchizi tu. We fikiria, juzi zilienea habari kuwa kama hukusoma fom siksi, basi diglii yako feki, sasa imekuwa tabu mtaani nakwambia. Binamu yangu kaenda kuomba kazi ya ulinzi kaulizwa kiwango cha elimu yake, akawambia alimaliza la saba, akaulizwa kama alisoma nasari, alipowaeleza kuwa hakupitia huko, wakamwambia hawezi kupata kazi maana cheti chake cha darasa la saba kitakuwa feki. Jamani nasari na cheti cha darasa la saba wapi na wapi? Kama sio uchizi ni nini hicho? Kali zaidi imetokea huko kijijini kwetu, ndugu yangu Abuu alikutana na binti mrembo wakapendana na wakapanga kuoana. Abuu akaanza mipango ya ndoa kwa kufuata taratibu zote za awali, akajitambulisha kwa wakwe, kisha akatafuta mshenga na kukamilisha kutoa mahari, baada ya muda si mrefu harusi ikafanyika wapenzi hawa wawili wakawa mtu na mkewe. Katika kutafuta maisha Abuu akaamua kuhamia mjini kutafuta kibarua, Mungu si Athumani akapata kibarua, akapata chumba cha kupanga kwa mama mmoja mwenye maneno mengi, akaona bora amuite mke wake mpenzi maisha yawe ya furaha zaidi. Kitendo cha kumleta mkewe kikaanzisha maneno toka kwa mama mwenye nyumba. Akanza kulalamika kuwa nyumba yake inageuzwa dangulo. Awali jamaa yangu hakujua kuwa yale maneno yalimhusu yeye. Ila siku moja ikawa dhahiri kuwa vijembe vile ni vyake. Akaona amuulize mama mwenye nyumba kwanini ana mnyanyasa vile. ‘Mama vipi nasikia unalalamika kuwa nimegeuza nyumba yako kuwa dangulo, sijakuelewa’ . Yule mama akawa utadhani ndio alilokuwa akilingojea maisha yake yote. ‘Ehee baba nilikupangisha chumba nikakuona wewe ni mtu mtulivu sasa naona umeleta changudoa nyumbani kwangu’. Jamaa akaja juu,’Mama nitake radhi huyo ni mke wangu nimemuoa kwa taratibu zote huwezi kumuita changudoa’. Ilikuwa kama vile yule mama hakuamini, akauliza ‘Ndoa yenu ilikuwa a sendoff?’ ‘Sendoff ya nini? Kijijini kwetu hakuna kitu kama hicho’ Looo hapo ndipo uchizi ukaingia, yule mama akapiga kigelegele, ‘Unaona nilijua tu, hapo hakuna ndoa. Ndoa bila sendoff ni ndoa feki’ Dahhh kweli uchizi unaongezeka

8 December 2016

BWANA USIHANGAIKE SANA

JAMES alikuwa anatokwa na jasho, alikuwa kachelewa mkutano muhimu na alikuwa kesha zunguka sana anatafuta nafasi ya kupaki gari lake. Basi akanyanyua mikono juu na kuomba. "Bwana ukinipatia nafasi nitakuwa naenda kanisani kila Jumapili sikosi'. Ile kumaliza tu mbele ikatoka gari moja akapata nafasi ya kupaki, basi akanyanyua mikono juu tena, 'Bwana usihangaike nimeshapata nafsi'

7 December 2016

BAJAJ ZINAPATA TABU SANA


SIKUBALIANI NA BARUA YAKO


The Human Resource Manager,
KUBOMA  MIKUSU LTD Co.
IRINGA
7 Dec, 2016

Mheshimiwa,

YAH: KUKATAA MAOMBI YANGU YA KAZI

Mheshimiwa nakiri kupokea barua yako ya  tarehe 3 Novemba 2016, ambayo ulinitaarifu kuwa maombi yangu ya kazi yamekataliwa. Naomba nikutaarifu kuwa sikubaliani kabisa na yaliyoandikwa katika barua yako ya kunikatalia kazi kwenye kampuni yako. Wewe ni HR wa saba kuniandikia barua ya namna hiyo, sasa nimechoka, mmeona kila mkijibu hivyo nanyamaza tu mnaona mi ni mnyonge sana sasa nasema nimechoka. Kwa maandishi yako mwenyewe umekiri kuwa vyeti vyangu ni vizuri sasa tatizo liko wapi?
Kwa hiyo pamoja na sifa kubwa ya kampuni yako, na uzoefu unaouonyesha wa kukataa kuajiri watu, nimeona naikataa barua uliyoniandikia na kwa taarifa yako tafadhali tayarisha kiti na meza yangu, kwani Jumatatu tarehe 12 Desemba nakuja kuanza kazi. Nategemea ushirikiano mwema toka kwako na viongozi wengine
Mi si mtu wa mchezo mchezo
Ndimi mtiifu

John  Mnyalu

5 December 2016

MKUTANO MKUU WA TANZANIA BLOGGERS NETWORK WAZINDULIA LEO....

MABLOGA wa Tanzania chini ya chama chao Tanzania Bloggers Network leo wamezindua Mkutano Mkuu wao ambao umeanza kwa elimu mbalimbali kuhusu shughuli yao. Shughuli nzima ilizinduliwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Maelezo, Dr Hassan Abbasi. Blogu hii hewa iliwakilishwa na Bosi wake. Picha na maelezo ya shughuli ilivyokuwa ni kama ifuatavyo;
Wapiga Picha wakijitahidi kumziba mgeni wa heshima ili sisi watu wa kawaida tusimuone.
Hai tebo
Afisa wa NMB akiwashauri mabloga faida za kuweka mkwanja wao benki

Vigogo wa tasnia

Maxence wa Jamii Forums akitoa ushuhuda
Bosi wa blogi hii akifuatilia kipengele muhimu cha Mkutano


1 December 2016

TANGAZO TANGAZO TANGAZO...JE UNA CHETI CHA DARASA LA SABA WAKATI HUKUPITIA NASARI? SOMA HAPA

TANGAZO KWA WAFANYAKAZI WOTE WA CHEKANAKITIME BLOG
WALE WOTE AMBAO WAMEPATA CHETI CHA DARASA LA SABA KUMBE HAWAKUPITIA NASARI, WAJITAYARISHE NAKUJA KUWATUMBUA HUKO HUKO MLIKO. KWA USALAMA WAKO KAJIUNGE NA NASARI HARAKA UPATE CHETI CHA KUMALIZA NASARI KISHA UFANYE MTIHANI WA DARASA LA NNE HATIMAE NDIO UPATE CHETI CHA LA SABA NDIO HAPO TU SIKUTUMBUI. SIRUDII TENA TANGAZO HILI