HELA NINAYO HALAFU NADHARAULIKA


Yaani jamaa wameniudhi kabisa wameniondoa kwenye mudi wakati nilikuwa katika furaha kubwa. Kwa mara ya kwanza nilikuwa nimesuka dili likatiki. Unajua siku hizi milango yote imefungwa madili hayakubali kabisa, watu tuko hali mbaya kila kona mtu unadaiwa, anaekudai nae anadaiwa, yaani sijui nani anazo. Ukienda kukopa unaambiwa unaetaka kumkopa kenda kukopa ili amlipe anaemdai. Hali ngumu, sasa mimi nikawa nimecheza mchezo fulani, ukakubali, mfukoni nikawa na kitu kama laki hivi, laki ni pesa siku hizi. Kwa kuwa ilikuwa majira ya saa sita mchana, nikaona niingie kwenye baa moja maarufu ambayo mchana inakuwa restoranti, nile chakula safi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu. Nikatafuta kiti kwenye kona, gazeti langu la Risasi Jumatano nililo linunua njiani nikalikunjua na kuanza kusoma. Ilipita kama dakika kumi, sioni muhudumu, nikaangalia huku na kule na kumuona jamaa mmoa amaevaa tai nikajua yule ndie meneja, si unajua mameneja wa baa siku hizi lazima wavae tai, hata kama joto liko kiasi gani, basi ile kumuuangalia tu, hapo hapo akajua tatizo liko wapi akamtuma binti mmoja aje kunisikiliza. Binti alipokuja akaniuliza nikaagiza chakula na kinywaji na kuanza kusubiri, nikaendelea kusoma gazeti langu, ghafla akaja mdada mwingine na mopu la kupigia deki, akaniomba ninyanyue miguu apige deki. Sikuwa na makuu nikanyanyua miguu wakati nimenyanyua miguu, akaja mdada mwingine na bakuli la maji na kitambaa akanambia ninyanyue mikono anataka kufuta meza, hee nikanyanyua gazeti langu juu. Hapo ndipo nilipojua kuwa na mimi naweza sarakasi, nilikuwa nimekaa kwenye kiti, huku nimenyanyua miguu na mikono. Wadada hawa ambao walionekana wamegombana maana walionyesha wazi kila moja hana mpango wa kuongea na mwenzie lakini waliweza kunipa amri hizi kali. Huwezi amaini ilionekana eti wameamua kufanya usafi kwenye meza yangu tu, mmoja anapiga deki chini mwingine anasafisha meza. Hatimae wakaniruhusu nishushe viungo vyangu, wakaondoka. Muda ukawa unayoyoma simuoni wakuleta chakula wala kinywaji. Nikaanza kujiuliza mimi nina mkosi gani mbona jamaa waliokuja baada yangu walikuwa tayari wamepewa chakula? Hela ninayo, na nilikuwa nimejipanga kula vizuri hawa jamaa hapa wameamua hawanipi chakula wala kinywaji. Nikaamua kulianzisha…..si unajua kabila letu huwaga hawajui kuongea, tukisema neno ‘swela’ hapo ujue ni kipigo tu. Nilipomaliza kazi nikaondoka na tai ya meneja. Sipendagi ujinga mimi.

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.