HATUPIMI BANDO

31 October 2016

ANGEKUWA TICHA ANGEFUNDISHA SOMO GANI?

JAMAA angekuwa ticha unadhani angekuwa anafundisha somo gani?

30 October 2016

BIBI HARUSI ATIMKA KATIKATI YA HARUSI NA KUKATAA KUENDELEA NA NDOA

JANA Jumamosi tarehe 29 Oktoba haitamtoka kijana mmoja ambaye alikuwa amepanga kuoa na mambo yote yakaenda vizuri , lakini katikati ya sherehe  ya ndoa bibi harusi katimka kakimbia akisema hataki tena kuolea juhudi za kijana wa watu kubembeleza hazikuzaa matunda.
Ishu nzima ilikuwa huko  Delta state in Nigeria, katika tarafa ya Udu.

29 October 2016

KIKOJOZI KAKOJOA NA NGUO KAITIA MOTO

JAMAA mmoja alikuwa na tatizo la kukojoa kitandani. Ikafikia anataka kuoa lakini aibu ikawa inamzuia hata kutafuta mchumba, akaamua kwenda kwa mganga kupata matibabu.  
MGANGA:Tatizo limeanza lini?  
JAMAA: Kiukweli toka nilipokuwa mdogo. Nimepigwa sana na wazazi wangu lakini wapi. Kila nikilala huwa ninaota mtu anakuja ananambia 'Aise twende tukakojoe' Nikiamka nimesha kojoa Mganga akamchanja jamaa chale nyingi mwili mzima na kufanya vimbwanga vingi sana kisha akatoa masharti 
MGANGA: Sasa nimeshakutibu hivyo ukiota tena hiyo ndoto, akija akikwambia tukakojoe, we mjibu kwa ukali mwambie nimeshakojoa, sawa? Jamaa akaondoka akiwa na uhakika kesha pona. Kesho yake akarudi kwa mganga, tena akarudi huku analia MGANGA: Vipi tena mbona unalia? 
JAMAA: Mzee tatizo limekuwa kubwa 
MGANGA: Kivipi?  
JAMAA: Jana nililala vizuri na yule jamaa akaja. Kama kawaida akanambia 'Twende tukakojoe" Na mimi nikakumbuka masharti yako nikamkemea kwa nguvu na kumwambia ' Toka shetani mkubwa, mimi nimeshakojoa' Si ndipo akanambia, 'Basi poa twende tukanye' Mzee chumba changu hakifai

24 October 2016

USITUME MESEJI HUMU MUME WANGU ANAWEZA KUUSOMA

WANAUME kadhaa walikuwa kwenye semina kanisani wakipewa mafunzo ya namna ya kuishi vizuri katika ndoa. Mchungaji akawauliza ni wangapi wanakumbuka mara ya mwisho walipowaambia wake zao kuwa wanawapenda. Wengine wakasema ni siku hiyohiyo wengine mwezi, wengine hawakumbuki mara ya mwisho kutamka kitu hicho. Mchungaji akawaambia kila mtu amtumie mke wake ujumbe rahisi tu. NAKUPENDA MKE WANGU. Baada ya hapo waliambiwa wabadilishane simu na kila mtu asome majibu ya simu yaliyorudishwa. Hapa chini ni baadhi ya majibu yaliyopokelewa;
1. Mume wangu umeshamtia mimba msichana mwingine?
2. Labda miaka hiyo, sio leo
3. Sina hela, ulizochukua zinatosha
4. Umefanya nini tena? Nimechoka kukuwekea dhamana
5. Sijakuelewa
6. Wimbo mpya huo?
7. Siamini lazima naota
8. Usiponambia ujumbe huu ulikuwa unaupeleka wapi, usirudi leo!
9. Mume wangu, mara ngapi nakwambia uache pombe?
10. Nani mwenzangu?

11. Samahani usitume ujumbe kama huu kwenye simu hii, mume wangu anaweza kuusoma, ntakupa namba yangu ya siri

20 October 2016

NASEMA NTAMTOA MTU KONGOSHO OHOOO


Ndugu zangu leo nimekasirika. Kuna watu wameniudhi nimeshindwa hata kunywa chai asubuhi. Kiukweli sasa hii imevuka mipaka nasema hii siikubali kabisa. Mambo kama haya ndio yanaweza kumfanya mtu akaamua kurudi kijijini kwao kuomba msaada wa mizimu ya kwao kulipa kisasi au kama ni mtoto wa mjini kuchukua uamuzi wa mwendokasi na kuruka vichwa sehemu za heshima. Yaan najiuliza bado nini hiki? Nauliza tena nini hiki sasa? Hivi kweli mnaona mnafanya jambo la kawaida kabisa? Nasema kiukweli baada ya muda mfupi nitamtoa mtu kongosho, mi sio mtu wa mchezomchezo, ulizeni jamani, ulizeni mtaani kwetu watawaambia kuwa huwa sipendi utani. Kwanza kabila letu hatupendi maneno sisi ni kazi tu, sasa nauliza nani amebadilisha sauti ya mwito wa simu yangu? Nikipigiwa simu mdada mmoja anawahi kimbelembele anaanza kujibu eti, ‘Asante kwa kumpigia malkia, malkia ni mke wa mfalme. Malkia atapokea simu yako sasa hivi’ Aise mie malkia? Nauliza na ndevu na mustachi huu mnaniita mie malkia? Nawaona wengine mnacheka mnacheka nini? Kuna la kucheka hapo wakati mwanaume mzima naitwa malkia? Huu utani sasa umevuka mipaka namsaka huyu aliyewaambia naitwa Malkia na pia mtaniambia kwanini hamkuniuliza mpaka mkaamini kuwa naitwa Malkia na kuruhusu kila anaenipigia anatangaziwa kuwa mie ni Malkia. Dah najisikia kulia kwa hasira.  Nimeanza kuchekwa mtaani, yaani karibu kila mtu mpaka vitoto vikiniona vinacheka, ndugu zangu wananiuliza lini nimebadili jina, wengine nawaona wananiangalia kiajabu ajabu wanashangaa kwanini najiita jina la malkia. Sasa sikilizeni naenda kulala nikiamka nikute mmefuta hako katangazo kenu kanakoniita mie majina ya ajabu. Sitaki kurudia tena, mi mbayaa ohh shauri zenu. Nasema tena nikiamua kurudi kwetu kuongea na babu nimtaarifu kuwa mjukuu wake anaitwa malkia, kitakachowatokea mi simo. Haya kwa usalama futeni hako kasauti. Sipendagi ugomvi.

13 October 2016

HELA NINAYO HALAFU NADHARAULIKA


Yaani jamaa wameniudhi kabisa wameniondoa kwenye mudi wakati nilikuwa katika furaha kubwa. Kwa mara ya kwanza nilikuwa nimesuka dili likatiki. Unajua siku hizi milango yote imefungwa madili hayakubali kabisa, watu tuko hali mbaya kila kona mtu unadaiwa, anaekudai nae anadaiwa, yaani sijui nani anazo. Ukienda kukopa unaambiwa unaetaka kumkopa kenda kukopa ili amlipe anaemdai. Hali ngumu, sasa mimi nikawa nimecheza mchezo fulani, ukakubali, mfukoni nikawa na kitu kama laki hivi, laki ni pesa siku hizi. Kwa kuwa ilikuwa majira ya saa sita mchana, nikaona niingie kwenye baa moja maarufu ambayo mchana inakuwa restoranti, nile chakula safi kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefu. Nikatafuta kiti kwenye kona, gazeti langu la Risasi Jumatano nililo linunua njiani nikalikunjua na kuanza kusoma. Ilipita kama dakika kumi, sioni muhudumu, nikaangalia huku na kule na kumuona jamaa mmoa amaevaa tai nikajua yule ndie meneja, si unajua mameneja wa baa siku hizi lazima wavae tai, hata kama joto liko kiasi gani, basi ile kumuuangalia tu, hapo hapo akajua tatizo liko wapi akamtuma binti mmoja aje kunisikiliza. Binti alipokuja akaniuliza nikaagiza chakula na kinywaji na kuanza kusubiri, nikaendelea kusoma gazeti langu, ghafla akaja mdada mwingine na mopu la kupigia deki, akaniomba ninyanyue miguu apige deki. Sikuwa na makuu nikanyanyua miguu wakati nimenyanyua miguu, akaja mdada mwingine na bakuli la maji na kitambaa akanambia ninyanyue mikono anataka kufuta meza, hee nikanyanyua gazeti langu juu. Hapo ndipo nilipojua kuwa na mimi naweza sarakasi, nilikuwa nimekaa kwenye kiti, huku nimenyanyua miguu na mikono. Wadada hawa ambao walionekana wamegombana maana walionyesha wazi kila moja hana mpango wa kuongea na mwenzie lakini waliweza kunipa amri hizi kali. Huwezi amaini ilionekana eti wameamua kufanya usafi kwenye meza yangu tu, mmoja anapiga deki chini mwingine anasafisha meza. Hatimae wakaniruhusu nishushe viungo vyangu, wakaondoka. Muda ukawa unayoyoma simuoni wakuleta chakula wala kinywaji. Nikaanza kujiuliza mimi nina mkosi gani mbona jamaa waliokuja baada yangu walikuwa tayari wamepewa chakula? Hela ninayo, na nilikuwa nimejipanga kula vizuri hawa jamaa hapa wameamua hawanipi chakula wala kinywaji. Nikaamua kulianzisha…..si unajua kabila letu huwaga hawajui kuongea, tukisema neno ‘swela’ hapo ujue ni kipigo tu. Nilipomaliza kazi nikaondoka na tai ya meneja. Sipendagi ujinga mimi.

11 October 2016

TUWE NA HURUMA JAMANI, INGAWAJE INAUMA

Kuwa na huruma sana inaponza sana, kwa mfano wa karibu ni mimi. Unajua mimi ni mtu mwenye huruma sana, na hii inanikosti. Lakini bahati mbaya hiyo ndio tabia yangu, siwezi kubadilika. Unajua kwa mfano isingekuwa huruma yangu ya hali ya juu leo hii ningekuwa sinywi pombe kabisaaaa unaonaee. Lakini mara nyingi nikiwa na glasi ya mwisho ambayo huwa najisemea baada ya glasi hii sinywi tena, utaona huruma yangu inaanza kunisuta. Maana naanza kufikiria ni watu wangapi ambao maisha yao yanategemea wanywaji kama mimi kuendelea kunywa? Kuna wakulima wa ngano ambao ikiwa wanywaji wote tutaacha kunywa na wao watakosa kipato cha kuuza mazao yao kwa watengeneza pombe, maisha ya watoto wao itakuwaje? Haya baada ya hapo kuna hizi kampuni za kutengeneza pombe, tena siku hizi ukienda kwenye makampuni makubwa kuna wakurugenzi, wakurugenzi wasaidizi, kaimu wakurugenzi, mameneja, wahasibu , wahudumu wa ofisi, madreva, wafanyakazi viwandani, watu wa masoko, wenye baa, wahudumu wa baa, yaani nikiwaza kuacha pombe naanza kufikiria watoto wa hawa watu wote wananitegemea mimi, halafu kitendo cha kufanya ukatili mkubwa wa kuwanyima haki yao ya kuishi kwa ajili ya ubinafsi wangu tu kinanisuta sana? Tena siku hizi unakuta mpaka wasanii toka nje wanatakiwa kuja kuponea fedha zangu ili watoto wao waende shule, kwa kweli huruma yangu naona ni muhimu kuliko ubinafsi wangu. na hapo ndipo huwa naagiza nne mfululizo, sio kwa sababu napenda pombe jamani ni huruma kwa hawa wote ambao maisha yao hapa mjini yananitegemea umeonaee. Tujitahidi jamani ili kusaidia wenzetu

5 October 2016

NDEGE MPYA NDIO ZISHAFIKA


HAYA tena ndege mpya hizo, hatimae tutaweza kusafiri kwenda makwetu kwa kutumia ndege, makofi tafadhali. Mambo si ndiyo haya, siku ya uzinduzi na mimi nilikwenda eapot, nizione zile ndege zetu kwa macho yangu, ujue nimechangia kununua zile ndege, si unajua zimenunuliwa na kodi za wananchi na mimi ni mwananchi. Kimsingi ilitakiwa jina langu nalo liandikwe kwenye kadi ya ndege, ya kuonyesha mwenye mali lakini nimeikabidhi serikali kodi yangu hivyo nimeiruhusu serikali iandike jina lake kwa kipindi cha mpito.  Siku Mkuu wa Kaya anazindua ndege, nilikuwa mmoja wapo wa wananchi ambao tulipanga foleni kuingia ndani ya ndege na kukagua kama kodi yetu imenunua kitu sahihi, nashukuru kila kitu kipya, viti vyake raha full kunesa. Kwa sasa nangojea ratiba itoke nijue ndege zitakuwa zinaenda wapi, hapo ndipo ntatafuta safari. Lazima nipande ndege mwaka huu. Nina rafiki zangu Mwanza, Njombe, Singida, Ntwara, Thame, Arusha Chini, kote lazima niende na ndege. Ila kuna kitu muhimu niwataarifu, ndege sio kama mabasi haya ya kwenda mikoani, ndege kitu kingine bwana , ndege kitu cha heshima, wakati unapanda ndege mtu lazima ujitayarishe kisaikolojia na pia kuwataarifu ndugu na jamaa na mtaani wajue ishu hiyo. Ngoja nikupe mfano, ukiwa unapanda daladala za kwenda kule kwa wale jamaa ambao huwa wanaingilia madirishani, utakuta kuanzia konda kavaa hovyo, dereva kavaa hovyo, basi halijaoshwa mwezi wa pili sasa, viti vibovu, hivyo msafiri na wewe ukiwa hovyohovyo poa tu. Halafu kuna mabasi siku hizi unanunua tiketi mapema, ukiingia kuna konda wa kike msafi, dereva kavaa tai, basi safi hivyo na wewe unajipanga usije kuchafua basi la watu. Sasa ndege ni kitu kingine, kila kitu kisafi mara kumi, wahudumu warembo, mapailoti mahendsam, unaweza ukapata bahati ya kuoa au kuolewa kutokana na safari moja tu ya ndege, sio mchezo. Hivyo basi siku chache kabla ya kupanda ndege lazima kuanza matayarisho. Unafanya shopping ya ukweli viatu vipya, pafyumu kali, sanduku jipya la magurudumu, kimsingi kila kitu kipya cha kupandia ndege mpya. Suti kali kwa wanaume, akina mama saluni ni muhimu, unaingia kwenye ndege unapendeza, ila onyo tafadhali madera sio fresh kwenye ndege mpya. 

4 October 2016

KWA MASWALI ZAIDI YA KUUDHI SOMA HAPA


i. Shilingi 1000/-ni bei gani?- Kisa wa Mbeya
JIBU:Ndugu yangu swali lako zuri sana, uchumi kwa kuwa umepanda na wewe chukua ngazi uufwatie hukohuko maana ukiwa juu alfu ni kama shilingi 900/- lakini ukiwa chini bei ya alfu ni shilingi 600/-
ii. Niko chuoni nasomea unesi, je unadhani nikimaliza shule nitaweza kufanya kazi gani?- Nene wa Kondoa
JIBU: Ukimaliza utakuwa polisi...KUENDELEA KUSOMA MASWALI NA MAJIBU HAYA YA KIFALA KABISA INGIA.... HAPA

HAINAGA SHEMEJI

Jamaa karudi ghafla nyumbani si akasikia sauti za ajabu toka chumbani kwake, akapiga ukelele na kuvunja mlango akamkuta mkewe akitetemeka;
Jamaa: We vipi?
Mke: Presha imepanda mume wangu, jamaa akakimbia sebuleni ili apige simu ambulensi ije wakati anahangaika kutafuta namba, mwanae akaja akamwabia,'Baba anko yuko uchi kwenye kabati chumbani kwenu', jamaa akatupa simu na kurudi chumbani alipofungua mlango wa kabati akamkuta mdogo wake kabatini bila nguo nae anatetemeka ,
Jamaa: Na wewe vipi unazubaazubaa bila nguo unamtisha mtoto wakati shemeji yako  ameshikwa na presha. Vaa upesi kaite ambulance