HATUPIMI BANDO

27 September 2016

SISTER ETI WE MSAGAJI?


  Jamaa kaingia bar akiwa kishalewa. Akaenda kaunta akaagiza kiroba, ghafla akamuona mdada mmoja kakaa peke yake pembeni;
 MLEVI: Oyaa kaunta hebu mpelekee kinywaji yule mdada pale nataka kuongea nae
KAUNTA:  Hakufai huyo, demu huyo msagaji  
MLEVI: Wewe mpe kinywaji mi namuibukia, tena hawa wasagaji ndio niliokuwa nawatafuta........mlevi akamsogelea yule mdada  
MLEVI: Mambo sister,
MDADA: Poa
MLEVI: Mi naomba tuongee biashara
MDADA: Ongea
MLEVI: Mimi nina gunia zangu kumi za mahindi, nasikia wewe ni msagaji, mashine yako ya kusagishia iko wapi nilete mahindi yangu?  MLEVI BADO YUKO HOSPITALI WIKI YA PILI SASA

MIPANYA NYUMBA HII INAVUTA HATA BANGI

Mmama alikuwa ndo kwanza kamaliza kupakua pilau lake aanze kula mara akasikia;
MGENI: Hodiiii..........(Haraka akaficha pilau chini ya kochi)
MMAMA: karibu jamani, karibu mgeni...(mgeni akaingia akakaa kwenye kiti ghafla akaona mvuke unatoka chini ya kiti)
MGENI: He jamani mbona kuna moshi unatoka chini ya kochi?
MMAMA: We acha tu mwenzangu, mipanya ya nyumba hii utaiweza? Ujue hapo imeshaanza  kuvuta bangi?

25 September 2016

UTUMBO WOTE NIMERUDISHIA NDANIJamaa fulani alikuwa na tabia ya kutoa ushuuz kwa nguvu kila aamkapo asubuhi. Mkewe alikerwa sana na tabia hiyo, alimkataza akachoka, siku moja akamwonya kuwa iko siku badala ya ushuzi, utumbo utakuja kumtoka. Jamaa alicheka sana kusikia hilo. Siku moja mke alilazimika kuamka alfajiri awatengeze kuku kwa ajili ya sherehe, alipowatoa utumbo wale kuku akakumbuka alichowahi kumwambia mumewe akaamua kumtisha, akamnyatia mumewe ambaye alikuwa bado amelala na kumuwekea utumbo kwenye pajama lake na kurudi jikoni. Muda si mrefu mwanaume aliamka akaachia ushuzi kwa nguvu kama kawaida yake, lakini akahisi kitu cha baridi ndani ya suruali, ile kuvuta si akakuta utumbo. Akapiga ukelele,’Mama yangu nimekufa’. Mke wake aliposikia akacheka peke yake, akajua jamaa kashaukuta ule utumbo. Kimya cha kama nusu saa kilipita. Hatimaye jamaa akamfuata mkewe jikoni akiwa amelowa jasho pajama nzima.
JAMAA: Mke wangu yale uliosema leo yametokea.
MKE: Yepi jamani?
JAMAA: Mke wangu ulisema nikiendelea kujamba utumbo utatoka, leo utumbo si umetoka kama ulivyosema
MKE: Pole mume wangu, sasa imekuwaje?
JAMAA: Namshukuru Mungu, nimejitahidi nimeusindilia na vidole na nimeweza kuurudisha ndani wote.
MKE: Mungu wangu umefanyaje wewe?

22 September 2016

MTOTO WA KITANGA AMENIVUNJA MGUU


Mikasa mingine huwa ukisimuliwa unacheka badala ya kumuonea huruma aliyekumbwa na mkasa huo. Jamaa yangu mmoja huko Tanga juzi alivunjika mguu akakimbizwa hospitali na wasamaria wema. Akapokelewa vizuri, daktaria akamuuliza jamaa yangu kimetokea nini mpaka akavunjika mguu. Kwa mshangao wa daktari jamaa akaanza, ‘Dokta mkasa huu ulianza miaka kumi iliyopita’ Dokta akashangaa, akamwambia  jamaa yangu sitaki kujua yaliyopita nataka kujua imekuwaje ukavunjika mguu?’ Jamaa yangu akasisitiza ‘ Dokta nisikilize kwanza nikuhadithie mkasa mzima sasa. Miaka kumi iliyopita nilikuwa nafanya kazi ya upishi kwa bosi moja kule Ngamiani. Yule mzee alikuwa na watoto watatu mmoja msichana. Huyu binti alikuwa mzuri sana, vijana wote mtaani walikuwa wakijaribu kupata nafasi katika roho yake lakini haikuwa rahisi kwa kuwa alikuwa akichungwa sana na baba yake na kaka zake. Mimi sikuwa na tatizo lolote maana tulikuwa tukishinda nae pale nyumbani masaa mengi, akinisaidia katika shughuli mbalimbali za mapishi jikoni. Kila mara jioni alikuwa anakuja chumbani kwangu tunaongea mengi, na kila mara kabla hajatoka chumbani kwangu alikuwa akiniuliza kama nahitaji kitu chochote, nilikuwa namjibu sikuwa nahitaji kitu. Na kila baada ya jibu hili, alikuwa akicheka sana na kuondoka zake. Kwa kweli nilikuwa nina uhuru wa mkubwa ndani ya nyumba ile, na mshahara wangu ulikuwa mzuri sana, hivyo sikuona kama kuna kitu zaidi nilikuwa nahitaji. Na hili liliendelea miezi mingi. Nikiri kwa kweli nilikuwa na mimi nampenda sana binti huyu wa Kitanga, lakini nilikuwa naogopa kumtamkia hili, tuliendelea kuishi hivi mpaka siku baba yake alipompeleka nje ya nchi kusoma, roho iliuma sana kumkosa. Sasa dokta leo nilikuwa nimekwea mnazi nikiwa juu si ndio kumbukumbu ikanijia kuhusu yule binti, na lile swali alilokuwa akiniuliza kila alipomaliza mazungumzo  ndipo akili iliponijia kuwa lile swali kumbe mimi nilikuwa mjinga sikuwa nimemuelewa binti yule miaka ile, alichokuwa anataka kunipa kumbe ndicho nilikuwa nakiota siku zote, kwa bahati mbaya nikajisahau na kuachia mikono na kuanguka na kuvunjika mguu’.

19 September 2016

UNAITWA NANI WEWE?

BOSI mmoja mmama alipata cheo katika ofisi mpya. Siku moja akamuita mmoja wa wafanyakazi ofisini kwake;
MMAMA: Unitwa nani kijana?
KIJANA: Naitwa Joni
MMAMA: Sikiliza mimi huwa siiiti mfanyakazi wangu kwa jina la kwanza inaleta kuzoeana kusiko na maana. Hivyo huwa kila mara natumia jina la pili, kama ni Mushi, Maganga au Mwakipesile. Haya jina lako la pili nani
KIJANA: Naitwa Mpenzi. John Mpenzi
MMAMA: Ok sasa John unaweza kurudi mahala pako pa kazi nitakuita badae

8 September 2016

FACEBOOK INGEKUWA YA MBONGO

Mark Zuckerberg mmiliki wa Facebook akikutana na mtu kwa mara ya kwanza anajitambulisha kirahisi tu na kusema 'Mimi ni Mark'. Sasa ngoma ingekuwa nzito kama Mbongo ndie angekuwa mmiliki wa Facebook, jina lake lingekuwa Mkurugenzi Mkuu Mzee wa Facebook Mzee wa Kufesibuka, Mutu ya Whatsapp Mark mwana wa Zuckerberg, mtoto wa ndama ya tembo. Kula pesa kufa kwaja