PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

KUWA UYAONE


Kuwa mzee kuna shida zake nakwambia. Kuna wakati unakaa unawaza halafu unacheka peke yako. Vijan wa siku hizi wanajifanya wajuaji lakini ukiona wanayofanya unachekea tumboni maana wakijua unawacheka wanaweza kuanzisha timbwili la dada yao Asha Ngedere. Leo asubuhi nilikuwa nawaza hii ishu ya ndoa siku hizi, nikaanza kucheka peke yangu, mjukuu wangu kaniuliza nacheka nini nikamwambia nimekumbuka sinema za Chale chapmlin. Kwanza enzi zetu si mwanaume wala si mwanamke wazazi wako waliweza kukuchagulia mwenza wako. Unaweza kuwa umekaa nyumbani baba yako anakuja anakwambia, “Mwanangu nimemuona binti ya rafiki yangu mmoja nimeona anakufaa, nimekwisha ongea na rafiki yangu na amaekubali muoane” Mchezo unaisha hapo mzee atafanya shughuli zote za kulipa mahari na kadhalika wewe kazi yako ni kuvuta mke ndani. Siku hizi sasa, ubishi umezidi basi wazee tumewaachia kazi hiyo wahusika ndio hapo kila siku kijana akitoka klab anakuja na mchumba mpya.  Siku akiaamua kuwa kapata anaemfaa basi linaanza sekeseke la kuwambia mumchangie eti kwa ajili ya sherehe, sasa kuoa umeoa wewe kwa kupenda mwenyewe, huu mzigo wa kugharamia harusi yako kwanini uwachangishe watu? Enzi zetu hutukuchanga lakini watu walialikwa kwenda kula na utakula vizuri chakula kilichotengenezwa na bibi harusi mtarajiwa, siku hizi unachanga halafu hata chakula hupati, ukipata chakula chenyewe utadhani ni kwa ajili ya wanafunzi wa boding, kibaya kweli. Mke unafika nae nyumbani kumbe hajui kupika, mnaishia kula chips zege cha baa kila siku, jamani kwanini nisicheke? ni halali nitoe machozi

Comments