HATUPIMI BANDO

18 June 2015

DILI LA KULA BATA MIAKA MITANO MFULULIZO

Ndugu zangu baada ya kutangaza nia wiki iliyopita, na kutokana na kuwa nilikiri sina vipaumbele wala vipaunyuma, nimeungwa mkono na watu wengi sana kisirisiri, nimeungwa mkono na wasomi na wasomaji, viongozi wa makundi mbalimbali yakiwemo ya akina mama na akina baba na wale ambao ni vigumu kuelewa kama ni akina baba au akina mama, pia na makundi mengine hata hayaeleweki maana viongozi wao walikuwa wakivuta sigara ambazo ni wazi hazijatengenezwa kiwandani. Lakini kimsingi waliuliza je, nini kikubwa nitakachokifanya? Maana yote wagombea wengine wameshaahidi watayafanya. Kiukweli ndugu wananchi mimi ndio nafaa, kwanza niseme kwa kiingereza, “I love is my country’ yaani naipenda sana nchi yangu, hivyo siku saba tu za kwanza mtaona mabadiliko ambayo hayajawahi kutokea katika Bongoland yetu. Cha kwanza ni kuwa nitafuta Wizara mizigo nyingi tu, hii itapunguza matumizi ya serikali yangu kwa zaidi ya asilimia 70. Nitabinafsisha wizara kadhaa na kuzifanya ziwe kampuni nakutoa tenda kwa wawekezaji.............inaendelea BONYA HAPA

16 June 2015

MJUE JOHN KITIME

Kitime-191x300 
NAME: John Kitime  
Aka: Anko
HOBBIES: Kung’oa meno simba walio hai bila ganzi wala nini kwa kutumia koleo. pia napenda mchezo wa kukwepa risasi, au kuzidaka kwa meno.  
GREAT ACHIEVEMENT: Nilikuwa mtu wa kwanza kutua kwenye jua, japo nifanya hayo usiku wakati kidogo joto limepungua. Pia naweza kuzungumza lugha mbalimbali10,956.  
JAMBO KUBWA LA KIJINGA NILILOWAHI KUFANYA: Kuogelea kwenye volkeno nilibabuka sana.
EMBARRASSING MOMENT: Nilishindwa kusukuma treni ili washtue iwake.
JAMBO LA KUJISIFU: Nyoka mwenye sumu kali aliniuma akafa yeye. SIFA ZANGU BINAFSI: SPENDI KUJISIFU
Kujua mambo yangu zaidi kila mara soma www.johnkitime.co .tz

10 June 2015

NDUGU ZANGU NATANGAZA NIA

Ndugu zangu ninaomba niwataarifu kuwa nimeamua kutangaza nia. Wahenga walisema, msema kweli mpenzi wa Mungu, na mimi ndugu zangu nitakuwa mkweli kuhusu azma yangu hii ya kutangaza nia. Kwanza nianze na ukweli kuwa hakuna mtu hata mmoja aliyekuja kuniomba kutangaza nia, ila mimi mwenyewe kwa kiherehere changu siku hizi, hata nikilala naota nimekuwa kiongozi mkuu wa Bongoland. Huwezi kuamini hata ninapotembea hili wazo linanijia kichwani hivyo nimeona nichukue maamuzi magumu nitangaze nia.......inaendelea huku