HATUPIMI BANDO

25 September 2014

KWETU KWAZULU NATAL

BAADA ya kuzamia Ulaya, jamaa yetu mmoja hatimaye akawa anaishi Uswisi. Lakini maisha yake yalikuwa ya kujifichaficha maana alikuwa hana vibali vya kuishi huko. Washikaji wenzie wakamwambia dawa hapa ni kufanya juu chini aoe mwanamke wa Kiswisi, hapo lazima atapata uraia.
Katika sakasaka hatimaye mama mmoja mzeemzee akaingia mkenge na kudhania anapendwa akakubali kuolewa na Mbongo. Mbongo akawa  amejitambulisha  kuwa eti yeye Mzulu............endelea HAPA

17 September 2014

MDAI MILIONI HUYO

Jamaa alikuwa anamdai mwenzie laki tano lakini kukawa na kukwepana kwenye kulipa , akaona aende kwa mwanasheria; JAMAA: Jirani yangu namdai laki tano inaonekana anataka kukwepa kulipa nifanyeje? MWANASHERIA: Una ushahidi? JAMAA: Kwa kweli sina tulipeana kindugu hatukuandikishana MWANASHERIA: Basi muandike barua mdai shilingi milioni moja yako JAMAA: Lakini namdai laki tano tu MWANASHERIA: Haswa, tunachotaka arekibishe hilo kimaandishi ili tuwe na ushahidi toka kwake mwenyewe 

KWA VICHEKESHO ZAIDI TUMEHAMIA www.johnkitime.co.tz

15 September 2014

MKE WANGU NIKIFA UTAOLEWA TENA?

Mume alikuwa kalazwa hospitali hoi, madaktari walikuwa wamemwambia uwezekano wa kupona ni mdogo sana, siku hiyo mke alikuja kumtembelea
MUME: Mke wangu nikifa utaolewa tena?
MKE:  story inaendelea huku....BONYAA

9 September 2014

BREAKING NEWWWWWWS CHEKANAKITIME YAHAMIA www.johnkitime.co.tz WAFANYAKAZI WAANDAMANA KISIRISIRI

WAMEHAMIA KIJIJI HICHO HAPO JUU, WAKURUGENZI WA BLOGU HII WAMEFUKUZWA WOTE, KASORO WALE WA KIKE BOSI KAHAMA NAO, SISI TULIOBAKI TUNADAI MAFAO YETU TUNAOMBA SERIKALI IINGILIE KATI, KWANZA BOSI KATUONEA TU, KUNA JAMAA ANAITWA MASANJA ALIPELEKA POSA PALE AMBAPO BOSI NAE ALIKUWA KALENGA, SASA KWA KISIRANI BOSI KAHAMA MJI, HII NI HAKI JAMANI? HII NI HAKI? TUNAOMBA SERIKALI IMZUIE MASANJA ILI BOSI WETU AOE ILI SISI TURUDI KAZINI. SERIKALI ISIPOTUSIKILIZA TUTAANDAMA MPAKA KIELEWEKE.
NI SISI WAFANYAKAZI TULIOACHWA SOLEMBA

NI SHEEEDAHHH PENZI LA SUPASTA NANIHII LAMKIMBIZA BOSI WETU KAAMUA KURUDI KIJIJINI

BOSI KAAMUA KUHAMA MJI ANARUDI KIJIJINI, KUKOSA PENZI LA SUPASTA KUMEMCHANGANYA, KAMA UNAVYOONA HAPO JUU KAKODI BODABODA, GUTA BAISKELI, KUJIMUVUZISHA KWENDA KWAO. KWA HIYO INGIA HUKU CHEKANAKITIME NDIO ALIKOHAMIA SASA NI SHEEEDAHHHH, YAANI HAPA NI KARIBU YA KIJIJI CHA TANANGOZI. OF KOZ HUKO KIJIJINI MAISHA BORA ZAIDI NA MAMBO MENGI YAKUFURAHISHA, ULANZI, KOMONI, WANZUKI, KIMPUMU, MNAZI, MANGURE, KANGARA, PINGU, FISI,MAMBO MSWANO SANA KARIBU SANA

6 September 2014

KISIRANI CHA BOSI KUMKOSA LULU CHAHAMIA KWENYE BLOGU

BAADA YA BOSI WA BLOGU HII KUACHA KULIA KWA UCHUNGU WA KUCHELEWA KUTOA POSA KAWEKA TANGAZO HILI MLANGONI KWAKE,,,,,,, 

KWA KITENDO CHA KUKOSA MCHUMBA BLOG HII KARIBUNI KABISA ITAKUWA WEBSITE ILI MPATE UHONDO WA ZIADA,WEBSITE ITAWEZESHA MPATE UHONDO WA ZIADA, HAKUNA KUBISHA KWANZA NINA KISIRANI SANA

4 September 2014

DARASA LA MAPENZI KWA WABONGO


Bosi wetu katoa ushauri huu na ukatoka katika gazeti maarufu la RISASI MCHANGANYIKO na kila Jumatano huwaga anaandika mambo huko......
 Mapenzi ya Kibongo ni ya aina yake duniani, hivyo nimeona leo nitoe som ili kuwasaidia mayanki namna ya kuishi kwa furaha katika mapenzi ya Kibongo. Kwanza mapenzi ya Kibongo hayashughuliki na mambo madogomadogo kama eti kupeana maua au eti kutembea beach mmeshikana mikono, hizo ishu ni za kwenye sinema tu au labda Ulaya. Hapa watu wako bize wana hangaika na maisha, mambo hayo ni ya wazungu. Wapenzi wa kibongo wa ukweli huwa hawahangaiki kuelezana eti I love you au nakupenda sana , aaa wapi, mdada akiwa  na mapenzi ya ukweli utaona anampikia mpenzi wake chakula cha ukweli, jamaa anapokula msosi anajua kuwa kweli huyu mdada ananipenda, hapo hata kama amewakaribisha mabest wake, utasikia ‘Aise huyu demu anakupenda sana kakupikia chakula kitamu hivi’.  Katika mapenzi ya Kibongo bili zote mwanaume lazima ulipe. Mkiwa mmekaa baa mmeshakula na kunywa sana hata kama mwanaume unaona mdada kaanza kushika pochi kama vile anataka kulipa jua ni geresha tu, anajua unampenda hivyo utalipa tu. Hata wale wadada waliowahi kuishi Ulaya wanajua system ya Bongo ni mwanaume kulipa.  Katika mapenzi ya ukweli ya Kibongo, mdada hata amkute bwana wake na binti mwingine, hata kama wamekaa kihasara ili kuonyesha mapenzi ni muhimu kumezea, tena unafanya kama hujaona chochote, hii itamfanya jamaa ajue unampenda sana, japo kuwa mapenzi ya Kibongo yana mipaka mdada huruhusiwi kukutwa amekaa kihasara na mkaka. Ili mwanaume wa Kibongo aonyeshe ana mpenda sana mpenzi wake wivu huwa muhimu, mwanaume yoyote, hata kama ndugu marufuku kumsalimu au kutuma mesej au kuchat kwenye simu, hasa giza likianza kuingia. Jambo lingine muhimu katika mapenzi ya Kibongo, mwanaume wa Kibongo marufuku jikoni, kwa sababu mdada anakupenda hata ukirudi saa kumi za usiku na unamkuta  ana malaria kali, lazima ajikongoje aingie jikoni, mwanaume ukikosea tu uanze kuingia jikoni  kupika ujue umeanzisha mtindo utakaokukosti akipona atadai uendelee kupika na kuosha vyombo na kadhalika. Chunga sana

KIMENUKA BOSI WA BLOGU KAMNUNIA KILA MTU OFISINI KISA LULU

Mara baada ya mesenja wa blogu kuja ofisini na gazeti hili, bosi aliposoma tu alipiga ukelele mmoja uliosikika mtaa wa pili. Watu wote ofisini tukabaki tunashangaa bosi kasoma nini, tukamsikia akilia wa uchungu, "Haiwezekani, haiwezekani, mimi nilikuwa nadunduliza tuhela nikatoe posa haka ka Masanja kwanini kamewahi? Mi sikubali naenda mahakamani kuweka pingamizi" Ndipo tukatambua kuwa Bosi nae kumbe nae alikuwa anataka kupeleka posa kwa nanilii. Kwa kweli hali ni mbaya sana hapa, bosi analia tu mfululizo, anaemfahamu Masanja amwambie amuonee huruma bosi wetu, ampishe wajameni......

2 September 2014

MZEE ZAIDI AKAE KWENYE KITI

Leo kwenye daladala wadada wawili walikuwa wanagombea siti;
KONDA: Kuweni wastaarabu wakina dada, acheni ugomvi, haya aliye mzee  zaidi kati yenu ndie akae kwenye kiti..........wote wawili wamekataa kukaa

HURUMA YANGU INANIPONZA

Wema wangu unaniponza sana, hebu ona mfano wa karibu uone jinsi huruma inavyonikosti. Lakini bahati mbaya hiyo ndio tabia yangu, siwezi kubadilika. Unajua kwa mfano isingekuwa huruma yangu ya hali ya juu leo hii ningekuwa sinywi pombe kabisaaaa unaonaee. Lakini mara nyingi nikiwa na glasi ya mwisho ya pombe, ambayo huwa najisemea baada ya glasi hii sinywi tena, utaona huruma yangu inaanza kunisuta. Maana naanza kufikiria ni watu wangapi ambao maisha yao yanategemea wanywaji kama mimi kuendelea kunywa? Kuna wakulima wa ngano ambao ikiwa wanywaji wote tutaacha kunywa na wao watakosa kipato cha kuuza mazao yao kwa watengeneza pombe, maisha ya watoto wao itakuwaje? Haya baada ya hapo kuna hizi kampuni za kutengeneza pombe, tena siku hizi ukienda kwenye makampuni makubwa kuna wakurugenzi, wakurugenzi wasaidizi, kaimu wakurugenzi, mameneja, wahasibu , wahudumu wa ofisi, madreva, wafanyakazi viwandani, watu wa masoko, wapika pombe, waonja pombe, wenye baa, wahudumu wa baa, yaani nikiwaza kuacha pombe naanza kufikiria watoto wa hawa watu wote wananitegemea mimi, halafu kitendo cha kufanya ukatili mkubwa wa kuwanyima haki yao ya kuishi kwa ajili ya ubinafsi wangu tu kinanisuta sana?  Kwa kweli huruma yangu naona ni muhimu kuliko ubinafsi wangu. na hapo ndipo huwa naagiza nne mfululizo, sio kwa sababu napenda pombe jamani ni huruma kwa hawa wote ambao maisha yao hapa mjini yananitegemea umeonaee. Tujitahidi jamani ili kusaidia wenzetu