HATUPIMI BANDO

19 August 2014

NDUGU MHARIRI NINA TATIZO

Ndugu Mhariri wa Blog naomba msaada.
Mimi ni mke wa mtu. Mume wangu ana miaka 40 mimi nina miaka 36, maisha yetu kwa kweli ni mazuri na yalikuwa na raha mpaka baada ya tukio ntakalo hadithia. Leo asubuhi niliamka kuwahi kazini nikamuacha mume wangu na msichana wa kazi nyumbani, mume wangu alinambia kuna kazi anafanya nyumbani kabla ya kwenda kazini kwake. Nimeondoka na moja ya gari zetu tatu sikufika mbali gari ikaanza kuchemsha  hivyo nikalazimika kurudi kubadilisha gari. Nimefika kwangu  nimemkuta mume wangu chumbani kwetu na msichana wa kazi , nimechanganyikiwa naomba ushauri, nifanye nini?
Mama Siwema.
JIBU
Mama Siwema ,
Kwa kweli umetumia busara sana kuuliza nini cha kufanya. Mimi kama mhariri wa Blog hii nakusifu kwa umakini wako na pia kukusifu kwa kujua wazi swala gumu kama hilo jibu lake litaweza kupatikana kupitia blog hii makini. Sasa tuanze na chanzo cha tatizo.  Gari lako lilianza kuchemsha, hii ni wazi kuwa aidha maji yameisha kwenye redieta, au redieta inavuja, au uliwahi kutembea bila maji sasa silinda hed imepinda. Ushauri ni kuwa ni vizuri upeleke gari kwa  fundi. Kuna jamaa pale Mwananyamala anaitwa Fundi Hamisi huyu ataweza kukutatulia tatizo bila wasiwasi yuko nyuma ya soko , we ulizia tu fundi Hamisi watakuonyesha gereji yake. Nategemea jibu hili litakuwa limekumalizia tatizo lako 
Aksante
Mhariri

No comments: