PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NAUFUNGA MDOMOWANGU

NAUFUNGA MDOMOWANGU
NAUFUNGA MDOMO WANGU

MKE WANGU ANA BAHATI SANA


Enzi zangu za kwenda bar zilinifanya nisikie mambo mengi sana ambayo kama huendi bar hutayasikia popote pale pengine, siku moja walevi watatu walikutana kaunta ya baa na kama ilivyo kawaida ya walevi haikuchukua muda mrefu wakawa marafiki na kuanza kuhadithiana mambo mengi mengine ya siri kabisa. Kwanza wakatambulishana majina, Joni, Pizo na Kulwa, urafiki wa kaunta ukaanza rasmi. Kadri vinywaji vilivyokolea na hadithi nazo zikazidi. Mhudumu mmoja aliwasumbua kwa kuchelewesha vinywaji basi hili likamfanya Joni kuanzisha mada moja ya ajabu kidogo, akawaambia wenzie kuwa jirani na mtaa anao ishi kuna baa nzuri sana, pale ukinunua chupa nne mwenye baa anakuongezea moja bure. Pizo akakumbuka kuwa aliwahi kungia baa moja ambayo ukinunua chupa moja mwenye baa anakununulia ya pili. Ubishi ukawa mkali mada ikiwa baa gani bora kuliko nyingine katika hizo mbili, na kujiuliza mwenye bar anapataje faida? Kulwa ambaye ni mkimya kidogo japo kuwa ndie aliyekuwa amelewa zaidi akaomba kuzungumza, yeye akawaeleza kuhusu baa ambayo mkewe ndiyo aliigundua. Katika baa hiyo wanywaji wote waliokwisha nunua zaidi ya bia mbili wanaingizwa kwenye bahati nasibu inayoendeshwa na meneja wa bar, ikitokea bahati ukashinda, basi meneja anakununulia pombe unywe mpaka ulewe, halafu anakutafutia chumba kwenye gesti ya jirani, kisha anakutafutia na mpenzi uhangaike nae mpaka asubuhi. Hapo ndipo ubishi ukapamba moto, kuwa hakuna kitu kama hicho Tanzania, Kulwa kwa mara ya kwanza aliongea kwa kupaza sauti na kutetea maelezo yake, kuwa anasema ukweli na ushahidi anao kwa kuwa kisha kunywa mara nyingi kwenye baa hiyo  na akashiriki katika bahati nasibu hiyo, bahati mbaya ana mkosi hivyo hajabahatika kushinda bahati nasibu hiyo, lakini ana wafahamu watu walioshinda bahati nasibu hiyo. Wenzie wakamuomba awatajie hata mmoja kati ya watu walioshinda bahati nasibu hiyo ya ajabu. Kulwa akashusha sauti na kuanza kuwahadithia kwa busara kuwa mke wake mwenyewe amewahi kushinda hiyo bahati nasibu mara mbili tena katika wiki mbili mfululizo, kitu kinachodhihirisha kuwa bahati nasibu hiyo haina upendeleo na inafanywa bila kubagua jinsia wala nini?

Comments

kiezera Alfred said…
Hahaha kulwa kaibiwa mzgo
kiezera Alfred said…
Hahaha kulwa kaibiwa mzgo
kiezera Alfred said…
Hahaha kulwa kaibiwa mzgo