HATUPIMI BANDO

30 August 2014

MAKENIKA WA GEREJI ZA BONGO

Ukiwa fundi magari hapa Bongo kuna mambo ambayo ni muhimu uyafuate ili uweze kupata fedha za kueleweka na maisha ya raha. Jambo la kwanza ni muhimu uwe unaonekana mchafumchafu. Fundi gani msafi? Ni muhimu pia ukiletewa gari kutengeneza hakikisha linatoka na alama kibao za grisi kila mahala, kwenye viti kwenye steringi, kwenye vioo, hiyo ndio itakuwa alama muhimu kwa mwenye gari kuwa kweli ulikuwa unashughulikia gari lake. Kitu kikubwa na muhimu kama makanika uwe unapendelea zaidi wateja wanawake, ila sio wale ambao ukiwa unatengeneza gari nae anashinda hapohapo gereji, anakufwata mpaka duka unalonunua spea hapana hao ni sumu katika kazi, na muhimu kuwakwepa kama mtu anae kudai. Wateja safi ni wale akina mama wanaokupigia simu na kukwambia “Njoo nyumbani uchukue gari linasumbua kweli sijui ni  nini’  na ukienda kuchukua gari swali lao moja tu, ‘Sasa itakuwa shilingi ngapi?” Hapo inakuwa wewe tu na akili yako, unatunga spea za uongo na magonjwa ya uwongo na bei za uwongo, usijisikie vibaya sana, maana unampa sevis ya kuchukua gari toka kwake, hahangaiki chochote na likiwa tayari unamrudishia, sawa tu na tofauti ya bei ya soda kati ya dukani ambako unalazimika kufwata mwenyewe utanunua shilingi mia 800/- bila glasi na ukienda hoteli za kitalii unaletewa soda kwenye glasi iliyochemshwa na mhudumu aliyevaa yunifom ya kitenge, huku ukiwa unapulizwa na kiyoyozi kikisindikizana na muziki wa kizungu kwa mbali, pembeni yako unakaa na wazungu laiv, na soda inakuwa shilingi 3000/-. Watu wakikusema vibaya Mungu atawahukumu. Achana na wajuaji, wale wanaokuja gereji eti uwafanyie sevis gari wakiwa wamekuja na kila kitu wameshanunua, mtu anakuja na oil, filta yaani kwa kweli wanakupotezea muda tu hao. Kuna wale watu ambao huwa wanajali sana magari yao, hawa mara nyingi bahili sana, hivyo akija siku ya kwanza ukaona anafuatilia kila unapogusa, tena anakushauri kabisa utasikia,'Hapo inafaa spana namba kumi', mtu kama huyu we mvumilie tengeneza tu gari kisha ingia uvunguni mwa gari na umwambie kama rafiki, ‘Mzee nadhani huku chini dampa imekaribia kwisha , ila usipate tabu inaweza ikafanya kazi miezi miwili mitatu haina haraka’, lakini wakati uko huko chini legeza nati moja au mbili, hili litasaidia kumfanya arudi mara akisikia kuna kitu kinagonga na atakuona wewe bonge ya makanika , kama gari litamharibikia  njiani bora zaidi maana atakuita na wewe utamkumbusha kuwa ulishamtaarifu kuhusu ugonjwa huo, hapo utakula hela yake kiulainiii. Ukimaliza kutengenza gari, lakini jioni na wewe unakideti na demu mpya, ambaye anahitaji usafiri wa kwenda kupeleka vitu kwa mama yake Kisarawe, hakikisha unafanya chini juu gari moja lisirudi kwa mwenyewe. Ni kweli atalalamika lakini  we mwambie kuwa we hupendi kazi za haraka haraka na kwa manufaa yake, lazima utaeleweka. Hasa ukimwambia umeona ni muhimu kucheki kama kwenye injin maunting kuna oil ya kutosha, tena utafanya bure. Ila hakikisha gari haipati mikwaruzo na usisahau kinga chini ya kiti cha gari….tutaendelea


29 August 2014

METHALI ZA KIZUNGU TOKA NCHI MBALIMBALI ZA AFRIKA

- It is only a silly cow that rejoices at the prospect of
being taken to a beautiful abattoir - Zambian Proverb
- No matter how far an eagle flies up the sky, it will definitely
come down to look for food - Zimbabwe Proverb
- An army of sheep led by a lion can defeat an army of lions
led by a sheep. - Ghanaian proverb
- The anus doesn't teach the mouth the sweetness of food -
South-African Proverb
- The man who marries a beautiful woman, and the farmer
who grows corn by the roadside have the same problem -
Ethiopian Proverb
- A short man is not a boy - Nigerian Proverb
- No matter how hot your anger is, it cannot cook yams -
Nigerian Proverb
- It requires a lot of carefulness to kill the fly that perches
on the scrotum - Ghanaian Proverb
- The frown on the face of the goat will not stop it from
being taken to the market - Nigerian Proverb
- A child can play with its mother's bosoms, but not its
father's testicles - Guinean Proverb
- He who goes to sleep with an itching anus wakes up with
smelly fingers - Nigerian Proverb

MJINI CHA BURE SALAMU TU


Yamenikuta, yamenikuta, nani anaukumbuka wimbo wenye maneno hayo? Basi yamenikuta. Nimeingia salun kutengeneza nywele zangu, si unajua kuweka bleki, mvi zimezidi mno naonekana si mkazi wa hapa mjini. Basi nimeingia saluni, kwanza mambo sio kama enzi zilee, nimepokelewa na wadada wawili wamevaa suruali zimebana hao, sijui walizivaaje, masikioni wanahedfon  mdoni chingam, ‘Karibu mzee, karibu kiti’ Haya mapya, enzi zile vinyozi wote walikuwa wababa tu hukuti mdada kwa kinyozi, kwanza tulikuwa hatusemi tunaenda saluni, tulikuwa tunaenda kwa kinyozi; bei zimeandikwa, kwenye kibao wazii, kunyoa kipara  500/-. Amigo 700/-, Madilu 800/-  Sasa mambo tofauti kabisa, saluni ina TV, muziki toka kwenye sabufa, wadada kibao, viti vya makochi dah. Haya nikakaa kwenye kochi la kifahari, mdada mwenye suruali imebana akaja, ‘Unanyoa nywele?” Nikasema hapana napaka rangi tu.  Kanishikashika kichwa na masikio akanambia , ingekuwa vizuri upunguze kidogo ndio rangi itapendeza, mtu ukishikwa masikio akili inasimama, bila kufikiri nikajibu ndio. Akaitwa mkaka mmoja akachukua mashine na kuanza kupunguza nywele zangu, nae akauliza, ‘Vipi mustach? Itafaa upunguzwe kidogo’ Nikajibu sawa na kwa kweli niliwasifu hawa vijana wanajali mteja. Baada ya
mkaka kupunguza nywele na mustachi, akaja mdada mwingine nae kavaa kisuruali cha kubana, mkononi kashika kibakuli cha rangi ya nywele, akaanza taratibu kunipaka kwa uangalifu sana, huku ananiongelesha kwa sauti yenye mvuto, vipi skrab? Nikamuuliza ndo nini? Akanambia ni kusafisha uso, na itakuwa vizuri kama nifanye na skrab maana ntapendeza, tena akausifu uso wangu kuwa hauna vichunusi, nikakubali skrab , ilikuwa pia nataka kujua ndio nini. Nikaambiwa nihamie kwenye chumba kingine kuoshwa nywele, kule nikakuta mdada mwingine kanambia nivue shati, nywele zikaoshwa vizuri, wakawa wadada wawili mwingine kaanza kunipaka mafuta ya nywele kisha nikaanza kusafishwa uso na maji ya moto, ikaanza hiyo skrabu. Nikaanza kufikiria kuwa nilitoka kwangu kuja hapa kupaka rangi nywele tu, hawa watoto wamenipenda wamenipunguza nywele na mustach, wamenifanyia skrab, hapa ndio pa kuja kila wikiendi. Hatimae nikaambiwa tayari, nilipojiangalia kwenye kioo nimekuwa mpyaaa, nikauliza bei, naambia alfu ishirini na tano, akili ika simama kwa sekunde, kidogo nizimie. Nikaja juu, ‘Kupaka rangi nywele shilingi alfu ishirini na tano toka lini?” Mzee si umenyoa nywele, mustach, umefanya scrab, umesema tukupake mafuta yale expensive jumla ndio hiyo mzee. Mfukoni nilikuwa na hizo hizo ambazo zilikuwa bajeti ya usafiri wa kwenda kazini wiki nzima. Nikazitoa na kukumbuka neno nililiona limeandikwa kwenye gari fulani….Mjini cha bure salamu tu

AMRI KUMI ZA SOKA LA ENZI YETU


Pamoja na sheria  17 za soka za FIFA kuwepo, enzi za utoto kulikuweko na sheria za soka ambazo ndizo zilizokuwa zinatambuliwa
1.     Mwenye mpira ndie anaeamua nani atacheza.
2.     Mtoto bonge ndie golikipa
3.     Wachezaji wazuri ndio wanaochaguliwa kwanza
4.     Kukiwa na penati ruksa kubadilisha kipa
5.     Ukipiga mpira kwa nguvu au kwa mandochi mwenye mpira ana ruksa ya kukuonya au kukukataza usicheze
6.     Usipochagia hela ya kujaza upepo utapigwa marufuku kucheza
7.     Hakuna marefa wala malinzmeni, na mpira unachezwa mpaka kuzunguka goli
8.     Kumkaba mwenye mpira faulo
9.     Ukitoboa mpira unalipa
10. Mwenye mpira akikasirika au akiumia au akiitwa na mama yake ndio mwisho wa mechi

28 August 2014

KILICHOSEMWA LINGANISHA NA KILICHOANDIKWA HAHAHAHAHAHAHA

KWA KITU KAMA WIKI, CHEKANAKITIME ILIKUWA DODOMA KUFUATILIA WASANII WALIOENDA KWENYE BUNGE LA KATIBA KUKUMBUSHIA MAPENDEKEZO YAO KATIKA KATIBA MPYA....HATIMAE KULIKUWA NA PRESS CONFERENCE NA VYOMBO MBALIMBALI VILIHUSIKA, HAYA NDIO YALIYOSEMWA;

Ndugu waandishi wa habari, katika mfumo wa sanaa wa nchi yetu wasanii wamegawanyika katika makundi makuu manne, ambayo yanaendeshwa na Mashirikisho ya vyama mbalimbali vya sanaa. Mashirikisho hayo ni;
i.                Shirikisho la Filamu TAFF
ii.              Shirikisho la Sanaa za Maonyesho
iii.             Shirikisho la Sanaa za Ufundi
iv.             Shirikisho la Muziki
 Tuliopo mbele yenu ni viongozi na wasanii kutoka vyama na Mashirikisho ya sanaa yaliyotajwa hapo juu. Kundi hili limekuwepo hapa Dodoma kwa siku mbili kukutana na wajumbe wa Bunge la katiba ili kufuatilia maslahi ya wasanii katika katika mchakato wa  Katiba mpya ya nchi yetu Tanzania.  Hii si mara ya kwanza kwa kundi hili kukutana na Wabunge wa Bunge hili la Katiba, bali hii ni mara ya tatu kundi hili limefika hapa Dodoma. Mchakato uliotufikisha leo hapa ulianza kwa Mashirikisho kukutana na kutengeneza Baraza la katiba ambapo mashirikisho yalitoa mapendekezo kadhaa yaliyofikishwa kwenye Tume ya Katiba. Lakini hakukuweko jambo lolote lililotokana na mawazo hayo ambalo lilichukuliwa na kuingizwa kwenye Rasimu ya Katiba. Mashirikisho yalituma majina 36, (tisa kutoka kila shirikisho)  katika kupendekeza wawakilishi katika Bunge la Katiba. Katika hili mjumbe mmoja, Paulynus Raymond Mtenda aliteuliwa na hivyo kubeba uwakilish wa kundi zima la wasanii Tanzania. Siku ya Ijumaa 14/2/2014 Mashirikisho yote ya sanaa yalikutana BASATA na kumkabidhi rasmi mapendekezo yao Mbunge huyu, ili ahakikishe kundi hili haliachwi katika mchakato wa Katiba.
Muda mfupi baada ya hapo kundi hili lilikuja Dodoma, na kukutana na Wabunge mbalimbali wa Bunge hili la Katiba, tulikutana na Wabunge wa kambi zote na kufanya nao mikutano mingi, ambayo mingine ilifika mpaka saa nane za usiku. Wabunge wa kambi zote walionekana kuunga mkono hoja za wasanii na tulianza mawasiliano mbalimbali na Wabunge yakiwemo ya ana kwa ana, simu na email, Wabunge wakihitaji documentation mbalimbali kuhusiana na mapendekezo yetu katika Katiba mpya.  Katika kipindi hiki tulikuja wakati hata Mwenyekiti wa Bunde la Katiba hajachaguliwa. Ujumbe huu ulikuja tena …. Na hii ni mara ya tatu.
Ujumbe huu toka awali ulikuwa na maombi mawili tu.
i.                Wasanii kutambuliwa kama kundi maalumu kama yalivyotambuliwa makundi ya wakulima wafugaji, wavuvi. Sababu za kutaka kutambuliwa huku, ni kuwa kundi hili ni kubwa kuliko hata makundi mengine yaliyotajwa hapo juu. Takwimu za Baraza la Sanaa la Taifa za mwaka 2006 zinaonyesha kuwa wasanii nchini walikuwa kiasi cha milioni 6. Leo ni mika minane imepita na si siri kuwa kundi hili limekuwa na hivyo kukaribia robo ya Watanzania, si haki kutolitambua.
ii.              Milikibunifu (Intellectual Property) itajwa rasmi kama moja ya aina za mali zinazohitaji kulindwa katika katika Katiba
Tumekuja pia na mapendekezo ya namna ya kuingiza hoja zetu hizi zilizosahauliwa, hatujaja na  Ibara mpya kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyoonekana kutuhumu katika magazeti ya juzi. Mapendekezo yetu ni kuwa katika Ibara ya 30 iongezwe  aya moja tu ya. Na ibara ya 37 inayoongelea Haki ya ulinzi wa mali, itambue kuwa pamoja na mali zinazohamishika na zisizohamishika, pia kuna mali isiyoshikika.
Tumepata faraja kubwa kupokelewa na Bunge hili,  Na kuweza kuzunguka kwenye kamati 9 kwa hizi siku mbili kukumbusha mapendekezo yetu haya, ambayo hayabebi tu wasanii bali pia wavumbuzi wa kiteknolojia, kibailojia, wasomi watafiti, na wananchi wote kwa ujumla. Pendekezo letu la pili ni muhimu katika kulinda na kuendeleza uchumi wa Tanzania. Na sisi kama Watanzania tumeona ni muhimu kutumia nafasi hii adimu kuhakikisha tunatoa mawazo yetu katika Bunge hili kwani tusipotumia nafasi hii tutakuwa hatukujitendea haki wala kuvitendea haki vizazi vijavyo vya Tanzania.


SIMON MWAKIFWAMBA-SHIRIKISHOLA FILAMU TANZANIA (TAFF)


JOHN KITIME….MTANDAO WA WANAMUZIKI TANZANIA (TAMUNET)

SASA CHEKI KILICHOTOLEWA KWENYE GALIZETI MOJA LILILOKUWA NA MUWAKILISHI KWENYE PRESS CONFENCE HIYO.....

22 August 2014

MKE WANGU ANA BAHATI SANA


Enzi zangu za kwenda bar zilinifanya nisikie mambo mengi sana ambayo kama huendi bar hutayasikia popote pale pengine, siku moja walevi watatu walikutana kaunta ya baa na kama ilivyo kawaida ya walevi haikuchukua muda mrefu wakawa marafiki na kuanza kuhadithiana mambo mengi mengine ya siri kabisa. Kwanza wakatambulishana majina, Joni, Pizo na Kulwa, urafiki wa kaunta ukaanza rasmi. Kadri vinywaji vilivyokolea na hadithi nazo zikazidi. Mhudumu mmoja aliwasumbua kwa kuchelewesha vinywaji basi hili likamfanya Joni kuanzisha mada moja ya ajabu kidogo, akawaambia wenzie kuwa jirani na mtaa anao ishi kuna baa nzuri sana, pale ukinunua chupa nne mwenye baa anakuongezea moja bure. Pizo akakumbuka kuwa aliwahi kungia baa moja ambayo ukinunua chupa moja mwenye baa anakununulia ya pili. Ubishi ukawa mkali mada ikiwa baa gani bora kuliko nyingine katika hizo mbili, na kujiuliza mwenye bar anapataje faida? Kulwa ambaye ni mkimya kidogo japo kuwa ndie aliyekuwa amelewa zaidi akaomba kuzungumza, yeye akawaeleza kuhusu baa ambayo mkewe ndiyo aliigundua. Katika baa hiyo wanywaji wote waliokwisha nunua zaidi ya bia mbili wanaingizwa kwenye bahati nasibu inayoendeshwa na meneja wa bar, ikitokea bahati ukashinda, basi meneja anakununulia pombe unywe mpaka ulewe, halafu anakutafutia chumba kwenye gesti ya jirani, kisha anakutafutia na mpenzi uhangaike nae mpaka asubuhi. Hapo ndipo ubishi ukapamba moto, kuwa hakuna kitu kama hicho Tanzania, Kulwa kwa mara ya kwanza aliongea kwa kupaza sauti na kutetea maelezo yake, kuwa anasema ukweli na ushahidi anao kwa kuwa kisha kunywa mara nyingi kwenye baa hiyo  na akashiriki katika bahati nasibu hiyo, bahati mbaya ana mkosi hivyo hajabahatika kushinda bahati nasibu hiyo, lakini ana wafahamu watu walioshinda bahati nasibu hiyo. Wenzie wakamuomba awatajie hata mmoja kati ya watu walioshinda bahati nasibu hiyo ya ajabu. Kulwa akashusha sauti na kuanza kuwahadithia kwa busara kuwa mke wake mwenyewe amewahi kushinda hiyo bahati nasibu mara mbili tena katika wiki mbili mfululizo, kitu kinachodhihirisha kuwa bahati nasibu hiyo haina upendeleo na inafanywa bila kubagua jinsia wala nini?

MI SINA VIJIKO

Jamaa kenda hospitali anakohoa, daktari kampa dawa ya maji;
DOKTA: Utakunywa dawa hii vijiko viwili kila baada ya masaa sita
MGONJWA: Dokta hiyo itakuwa ngumu kidogo
DOKTA: Kwanini tena?
MGONJWA: Dokta mie nyumbani nina kijiko kimoja tu

JE WEWE NI MBAYA? JUA DALILI ZA MDADA MWENYE SHEPU NA SURA MBAYA


Blog yenu imechukua muda wa miezi miwili kufanya utafiti huu ambao utawasidia sana wadada ili wengine wapunguze muda wa kujiangalia kwenye kioo na kufanya shughuli nyingine, pia kuwapunguzia muda wa kwenda saluni na kupoteza pesa ambazo wangeweza kulipia kodi ya nyumba zao.  Blog yenu imeweza kupata utafiti utakaoweza kukusaidia mdada ujijue kama wewe ni mbaya au mzuri. Kama we mbaya kwanini uhangaike tena sijui, saluni, kujinyima msosi ili uwe slim, kuhangaika kununua kioo, yote haya utakuwa huna haja nayo na fedha unayoipata ukaitumia kwa shughuli za maendeleo kama vile kufuga kuku au kilimo cha kufa na kupona. Sasa utajijuaje kama wewe ni mbaya?
1.     Ukiona umejipiga ‘selfie’ au hata picha yoyote ukaiweka kwenye facebook na kutag watu mia ukapata ‘likes’ mbili tu ni dalili ya wazi kuwa we mbayaaa.
2.     Ukiona wakaka wanapenda sana kampani yako lakini kila mara wanakuuliza ushauri juu ya kuwapata wadada wengine , ujue wewe ni  mbaya, maana wanajiona kama vile wanaongea na mwanaume mwenzao
3.     Ukiwa na wasichana wenzio halafu mnataka kupiga picha ya pamoja ukona wanang’ang’ania wewe ndio uwapige picha ni dalili ya wazi hawataki uwaharibie picha yao kwa sura yako mbaya.
4.     Jina lako instagram na facebook  pia ni dalili tosha kuwa na wewe unajijua ni mbaya, majina kama sexydiva, sweetylicious, cutebaby na kadhalika, ni nja ya kisaikolojia ya wabaya kutaka kuonekana wazuri.
5.     Ukiona utafiti huu umekuudhi na una ulaani hiyo ndio dalili ya ukweli kuwa wewe mbayaaaaa

21 August 2014

MAFALA WAKO WENGI


VICHWA VYA HABARI

 Wahezaji?

 Umeona ee tumeendelea sana, tunacheza kwa kutumia umeme

 Wanawake wenzio watapumua sasa

DUH

MWALIMU KASEMA TUJIHESHIMU

MAMA: We mtoto mbona kila asubuhi unajiangalia kwenye kii harafu unajiamkia shkamoo?
DOGO: Mwalimu kasema lazima tujiheshimu

20 August 2014

ZAMU YAKO NIFUKUZE NA MIMI

Mgonjwa kwenye hospitali ya machizi alikuwa kaokota kisu, akaanza kumfukuza daktari mmoja kisu mkononi macho yamemtoka kwa hasira, daktari kapaniki akakimbia hatimae akafika kwenye geti akakuta limefungwa akasimama akiwa amekata tamaa, chizi akaja spidi na kisu kanyanyua, alipofika kwa daktari akashusha kisu;
CHIZI: Haya sasa zamu yako chukua kisu anza kunifukuza na mimi

NIMEMPA MATONE YA DAWA YA MACHO

Dokta mmoja alikuwa amepata dharula akamwambia mlinzi wa hospitali yake ahakikishe hospitali inabaki wazi. Baada ya masaa mawili akarudi;
DOKTA: Vipi hapa salama?
MLINZI: Salama tu mzee,  alikuja jamaa mmoja akasema anaumwa kichwa nikampa panadol
DOKTA: Safi sana
MLINZI: Akaja mwingine akasema anaumwa tumbo nikampa flajil
DOKTA: Aise we mkali safi sana
MLINZI: Wakati nataka kufagia ofisi amekuja binti mmoja mzuri sana wa Bongomuvi kaingia fosi kavua nguo zote, kapanda kwenye kitanda cha kupimia wagonjwa kalala, akaniambia, nimsaidie hajamuona mwanaume mwezi wa sita na hawezi kuvumilia zaidi, basi nikamnyunyizia machoni matone ya dawa ya macho
DOKTA: Duh

HAYA NINONG'ONEZE SIKIONI...........

Dogo alikuwa kanisani na mama yake, mkojo ukambana;
DOGO: Mama mi nataka kukojoaaa
MAMA DOGO: Nyamaza ukiwa kanisani usiwe unasema unataka kukojoa sema nataka ninong'one, mi ntaelewa unasikia wewe?
Wiki inayofuata Dogo akaenda kanisani na baba yake, ghafla;
DOGO: Baba mi nataka ninong'one
BABA DOGO: Haya ninong'oneze sikioni

19 August 2014

NDIO LAZIMA TUPATE KATIBA MPYA

Jamaa alikuwa kakaa kiti cha nyuma kabisa kwenye daladala, pembeni yake kuna binti mzuri akaanza kumpa maneno matamu, binti akawa anamkatalia, jamaa hakukata tamaa , na binti hakubadili mawazo, hatimae binti akawa amekasirika, akamwambia jamaa kwa ukali na sauti ya juu basi zima wakasikia,'We baba vipi? Kwani lazima?" Jamaa akajibu nae kwa nguvu, 'Ndio ni lazima tupate Katiba mpya maana hii ya sasa imepitwa na wakati'

BEFORE AND AFTER


NDUGU MHARIRI NINA TATIZO

Ndugu Mhariri wa Blog naomba msaada.
Mimi ni mke wa mtu. Mume wangu ana miaka 40 mimi nina miaka 36, maisha yetu kwa kweli ni mazuri na yalikuwa na raha mpaka baada ya tukio ntakalo hadithia. Leo asubuhi niliamka kuwahi kazini nikamuacha mume wangu na msichana wa kazi nyumbani, mume wangu alinambia kuna kazi anafanya nyumbani kabla ya kwenda kazini kwake. Nimeondoka na moja ya gari zetu tatu sikufika mbali gari ikaanza kuchemsha  hivyo nikalazimika kurudi kubadilisha gari. Nimefika kwangu  nimemkuta mume wangu chumbani kwetu na msichana wa kazi , nimechanganyikiwa naomba ushauri, nifanye nini?
Mama Siwema.
JIBU
Mama Siwema ,
Kwa kweli umetumia busara sana kuuliza nini cha kufanya. Mimi kama mhariri wa Blog hii nakusifu kwa umakini wako na pia kukusifu kwa kujua wazi swala gumu kama hilo jibu lake litaweza kupatikana kupitia blog hii makini. Sasa tuanze na chanzo cha tatizo.  Gari lako lilianza kuchemsha, hii ni wazi kuwa aidha maji yameisha kwenye redieta, au redieta inavuja, au uliwahi kutembea bila maji sasa silinda hed imepinda. Ushauri ni kuwa ni vizuri upeleke gari kwa  fundi. Kuna jamaa pale Mwananyamala anaitwa Fundi Hamisi huyu ataweza kukutatulia tatizo bila wasiwasi yuko nyuma ya soko , we ulizia tu fundi Hamisi watakuonyesha gereji yake. Nategemea jibu hili litakuwa limekumalizia tatizo lako 
Aksante
Mhariri

JE NI KWELI? AU THI KWELI?

Kwa muda mrefu kumekuwa na stori kuwa wale jamaa dhetu wanaoishi karibu na Moshi huwa wanakula ugali kwa picha ya thamaki. Blogu yenu tata ilituma timu ya wapelelezi kwenda kufukunyua kuhusu hili. Nyumba ya kwanza kuingia tu, wapelelezi wetu walikaribishwa msosi huu laiv. Bado ushahidi hautoshi upelelezi unaendelea

MKE WANGU MIMI KAZI BASI

Mke alikuwa kaenda mjini kwenye shughuli zake ghafla akapata wazo amtembelee mumewe ofisini. Ile kufungua mlango wa ofisi ya mumewe si kamkuta sekretari kamkalia mumewe pajani. 
MUME: Karibu mke wangu mpenzi karibu. Unajua mimi sasa kazi kwenye kampuni hii nimeshindwa, hebu ona wamebana matumizi wanatuambia wafanyakazi wawiliwawili tutumie kiti kimoja na kompyuta moja. Yaani nilikuwa nirudi leo nikwambie kuwa mimi kazi basi tuangalie mbele yajayo.

16 August 2014

MUUJIZA YULE DADA ALIYEKUFA KAFUFUKA

MKE: Ulilala wapi? Unadharau sana unanirudia mie alfajiri, leo lazima unambie huko ulikolala
MUME: Mke wangu mpenzi jana nilichanganyikiwa, si unamfahaamu rafiki yangu Joshua, basi jana dadake kaanguka kafariki ghafla basi nimelazimika kulala huko kumliwaza
MKE: Ok naoga na mie nikawape pole........(akaenda kuoga)
MUME: Yaani maajabu makubwa yametoea, muujiza laiv
MKE: Kivipi?
MUME: Ulipoenda kuoga, Joshua kanipigia simu eti kuna mchungaji kaja kumuombea yule dadake aliyekufa sasa kafufuka hivyo wameondoka kuelekea kijijini kwao kuwaona wazazi wao, yaani muujiza

KUNA LIMBABA LINANIBAKA..........


Mdada aliyekuwa anabakwa akafanikiwa kuishika simu yake, akapiga simu polisi;
POLISI: Haloo polisi hapa tukusaidieje?
MDADA: Polisi nisaidieni, kuna libaba linanibaka, nisaidieni mje mlikamate kesho

NAKEMEA PEPO LIKUTOKE

MCHUNGAJI: Nakemea pepo la wizi likutoke
MUUMINI: Amen
MCHUNGAJI: Nakemea pepo la uwongo likutoke
MUUMINI: Amen
MCHUNGAJI: Nakemea pepo la uasherati likutoke
MUUMINI: Ngoja kidogo mzee, hilo utalikemea kesho

ANGALIA TEMBO WAKIKATA NYONGA -VIDEO


TUMEYAONA MAGALIZETINI

Hii kali Wahehe na wamasai ruksaaaaaa.
_______________     _________________  _________


TUMEINYAKA TOKA GAZETI FUDENGE........Tukio hilo lilitokea Jumamosi iliyopita katika mji wa Naivasha uliopo Nairobi nchini humo ambapo mwanadada huyo alipopanda jukwaani akiwa amevaa sketi fupi iliyokuwa imeacha sehemu kubwa ya mapaja wazi, wanaume wakware walianza kumvutia chini kwa nguvu......MJI WA NAIVASHA ULIOPO NAIROBI.....TEH TEH TEH TEH

HATARI HATARI WIZI MPYA WAINGIA MJINI.......TAKE CARE

Blogu yenu siriaz ingependa kuwataarifu wasomaji wote kuhusu wizi mpya ambao unaendelea mjini. Wizi huu hufanywa na vibinti vinavyovutia sana, na wanaume tu ndio huibiwa, hivyo akina mama tafadhali muwambie waume zenu na maboifrend wajihadhari. Wizi huu hutokea kule baharini maeneo ya Koko, ukipaki tu vibinti viwili vizuri huja na kuanza kusafisha kioo cha gari lako, wakati wakifanya hivyo hujiachia viblauzi na visidilia vyao unajikuta huwezi kuacha kukodolea macho. Vikimaliza usafi husema havihitaji malipo ila vinaomba lifti kwenda Msasani. Ukikubali vinapanda kiti cha nyuma na kuanza kukushika shika shingo na masikio, kamoja kanahama kiti na kuja kiti cha mbele na kuanza kukula denda wakati kenzie kanakuibia mkwanja wako. Bosi wetu kaibiwa juzi, jana tena kaibiwa na leo keshatupigia simu kuwa kaibiwa, na kesho ni wazi ataibiwa. Tunaomba mjihadhari sana
Aksante

14 August 2014

WAKUBWA WAZIMA MNAAMINI MAZIMWI


Mheshimiwa mmoja baada ya kupata cheo si akapewa nyumba mitaa ya watu wenye pesa, akahamia huko akiwa na mke na mwanae. Siku moja mwanae aliyekuwa kazoea maisha ya Uswazi akawa anawinda ndege na manati kwenye uwanja wa jumba lao, bahati mbaya jiwe likapitiliza na kwenda kuvunja kioo cha nyumba ya jirani. Mheshimiwa na mkewe wakaamua kumfuata mwenye nyumba wakamuombe msamaha. Walipogonga mlango akafukua mbaba mmoja akawakaribisha kwa heshima, wakaingia na kuanza kujieleza. ‘Samahani sie tumehamia karibuni hapo nyumba ya pili, mwanetu kavunja kioo chako kwa bahati mbaya, tumekuja kuomba msamaha na kuona kama tunaweza kutengeneza’. Mwenyeji wao akawaomba wakae  kisha akawaambia, ‘Naomba niwahadithie kitu. Kwanza mimi nawashukuru nyinyi na mtoto wenu. Mwenye nyumba hii ni mchawi mkubwa sana, mimi ni ZIMWI alikuwa amenifungiwa kwa zaidi ya miaka 200 kwenye kichupa ambacho kilikuwa kwenye  dirisha lililovunjwa na chupa nayo ikavunjika nami nimekuwa huru, kwa hiyo kwa shukurani ombeni chochote mtakacho nitawapa, nina uwezo huo’ Hapo hapo muheshimiwa akauliza tena,’Yaani kitu chochote?’ Akajibiwa ‘Ndio’. Basi pale pale akasema, ’ Mimi naomba niwe bilionea mpaka nife’ Akajibiwa ,’ Hilo jambo dogo sana kwangu, umepata na kesho utaamka tajiri’ Mama nae akaomba vyake, ‘Mi nataka niwe na nyumba kila nchi duniani na niwe na biashara Dubai na China na HongKong’ Akajibiwa, ‘Umepata mama, kuanzia kesho hayo ni yako. Mimi nawashukuru kwa uhuru wangu lakini nina kaombi kadogo’. Mheshimiwa haraka akajibu, ’Sema tu wewe ni kama ndugu yetu sasa’ Basi ZIMWI likasema, ‘Naomba mkeo abaki hapa kama masaa mawili tu, unajua kifungo nilichofungwa kilinizuia kila kitu, hata mke sijapata kipindi chote hicho. Nikimaliza tu hilo ntaondoka kurudi kwetu Uzimwini hamtaniona tena, itakuwa siri yetu’. Mme na mke wakajadiliana wakaona utajiri waliopata ni mkubwa sana, na hilo jambo ni dogo sana la mara moja tu tena kwa siri, wakakubali sharti. Mke akabaki pale kwa masaa kadhaa.  Shughuli ilipokwisha, mama wa watu akiwa anajitayarisha kurudi kwa mumewe kichwani akiwaza utajiri, ZIMWI likakohoa kidogo na kumuuliza yule mama, ‘Samahani una miaka mingapi na mumeo ana miaka mingapi?” Mama wa watu akajibu, ‘Mie nina miaka 40 mume wangu ana miaka 46’ Yule Mbaba akacheka sanaa, ‘Sasa nyinyi wakubwa wazima mpaka leo mnaamini stori za MAZIMWI?

9 August 2014

THE SPIRIT OF THE NATION


KAUNTA YA JUMAMOSI

NAGAWA FRIJI BURE KARIBUNI

BOSI wetu alinunua friji jipya, akawaza namna ya kuondokana na lile la zamani lililokuwa bovu na haliuziki, basi akaliweka nje ya nyumba yake na kuandika kibao ANAE TAKA KUCHUKUA ACHUKUE BURE, watu wakawa wanapita wanafungua lakini kila mtu akawa anaogopa kuchukua maana hakuna aliyeamini mtu anaweza akagawa friji zima bure. Baada ya kuona wiki imepita halijachukuliwa, akaandika FRIJI INAUZWA LAKI 3, usiku uleule likaibiwa

MICHEPUKO SIO DILI UNAONA SASA

HUYU KAMA MZEE WA MICHEPUKO VILE, KATAITIWA NA WAKUU WA BARABARA

7 August 2014

FUDENGE UNGEMEZA SIMU USINGEACHWA

Katika pita pita za wakubwa wa Blogu hii isiyo makini si wamekuta blogu moja ikiwa na stori kuwa supasta Fudenge kakutwa na simu ina meseji toka kwa mchepuko, kukawa na heka heka zilizoishia kukwanguana makucha. Sasa blogu yenu baada ya kutafakari imekuja na njia ya kuzuia maboiflend kusoma mamesej ya kwenye wasap, au badoo na kadhalika. Ushauri ni kufanya kile alichofanya binti mmoja ili kuhakikisha boiflendi hasomi kitu, alimeza simu. Ukiona mambo yanataka kuwa magumu meza simu. Ni vizuri sasa watu kuanza kutembea na visimu vidogo vinavyowezakumezeka kirahisi.

6 August 2014

NAOMBA KAZI YA ULINZI


MENEJA WA KAMPUNI
DASLAMU

Mheshimiwa naomba kazi ya ulinzi

Jina langu naitwa Kubomakutali aka Bulaza Kei, huwa najiburudisha kwa kung’oa meno simba  wakiwa hai, na kukwepa risasi. Kila siku huwa nakimbia napanda mlima na kushuka mara tano. Kwa kumbukumbu zangu mambo yaliyowahi kunipa sifa ni pale nilipopigana na nyati na nikamvunja shingo kwa kabali. Nimewahi kuzama majini kwa dakika ishirini bila kupumua, siku ya idi nilizamia pale coco bich kwa dakika kumi ndipo nikaibuka na kupumua. Kati ya mambo ninayoweza kuyaita ni sifa kwangu ni pale nilipoumwa na nyoka mwenye sumu kali,na huyo nyoka akafa palepale. Sifa yangu kubwa ni kuwa huwa sipendi kujitapa hovyo.

Ni mimi Bulaza K

Kwako Mzee wa Cheka na Kitime


Kwako Mzee wa Cheka na Kitime,
Dar es Salaam.
Salaam nyingi zikufikie popote ulipo, sisi huku ni wazima kabisa. Nimekuwa nikisoma makala zako na kugundua kuwa wewe ni mtu mwenye busara sana. Namuomba Mungu akuzidishie uhai.
Nia na madhumuni ya barua hii ni kukuomba ushauri kwa tatizo langu. Kiukweli ndani ya moyo wangu nina wasiwasi mke wangu si muaminifu ndani ya ndoa. Yeye kaajiriwa Sinza Mori kwenye kibanda cha simu, sisi tunaishi Gongo la Mboto.
Kila siku huwa anachelewa kurudi nyumbani,  na kila siku anarudi na taxi, mi najua mshahara wake hautoshi kugharamia hilo ndiyo maana nakwambia nimeanza kuwa na wasiwasi. Hebu fikiria wiki iliyopita nilijaribu kugusa simu yake alikuwa mkali kwelikweli kidogo aniue, nikashangaa sana ukali wote huo wa nini?
Ila niwe mkweli, sijawahi kumuonyesha dalili zozote  kuhusu wasiwasi wangu, sitaki kumuudhi bila kuwa na ushahidi. Lakini mzee, jana niliamua kumfuatilia mke wangu hukohuko kazini kwake, nijue nini kinaendelea. Nikajificha mahali ambapo ilikuwa rahisi kumuona anapotoka kazini bila yeye kuniona.
Muda wa kufunga kazi ulipofika nikamuona anatoka kazini kwake akisindikizana na mwanaume mmoja mrefu hivi akiwa kamshika mkono wanacheka. Moyo ukaanza kunikimbia, nikaona niliyokuwa nahisi inawezekana ni kweli. Ili niwe na ushahidi mzuri nikaona niangalie saa ili nijue ni saa ngapi walitoka, wakati wa kesi kila kitu kiwe na ushahidi.
Mzee wangu nilipoangalia saa si ndiyo nikagundua saa yangu imesimama. Mzee saa yangu ni aina ya Rolex, na saa za aina hii ni bei ghali sana. Hii saa nilirithi kutoka kwa baba yangu, yeye aliniambia alinunua Uswisi wakati alienda kule kwa ajili ya kusindikiza mgonjwa aliyeenda kutibiwa huko na aliniambia kuwa ilikuwa na gerentii haitasimama kamwe, sasa ile kuona imesimama ilinichanganya sana.
Je, unanishauri vipi?  Niitengeneze kwa mafundi wa hapa Dar au nigharamie ikatengenezwe Uswisi? Au unanishauri ninunue nyingine?

4 August 2014

WAKATI KULE MADOLA WANARIADHA WANANANIHINO, NA HUKU STARS NAO IVOIVO


BREAKING NYEUSSSSSSSSSSSSSSIII BONGO KUOKOTA MEDALI KIBAO KATIKA MICHEZO YA MADOLA

MWANDISHI  mahiri ambaye blogu hii ilimtuma aende kuandika mambo yanayotokea kwenye michezo ya Madola Glasgow, ameweza kujipenyeza ndani kabisa ya timu kutoka Bongo iliyotuwakilisha huko, amepata taarifa ambayo blogu hii makini kuliko maelezo na chenji inarudi imeona kuwa taarifa hii inatupa matumaini kuwa wawakilishi wetu watarudi na medali nyingi sana kuliko tulivyotegemea. Baada ya timu yetu kukosa medali katika mashindano ambayo kwa kweli hayakuwa fea kabisa, yaani hebu we fikiria mtu unaambiwa ushindane na yule Husain Bolt, je hii ni haki? Nauliza ni haki kweli? Ingetakiwa wabongo tushindanishane sisi wenyewe, na wengine washindanishane kivyao ili japo aweko mtu wa kwanza na wa pili toka huku Bongo. Michezo mingine haijulikani kabisa Bongo au ilikuwa inachezwa enzi za Nyerere sasa hiyo  ni haki kweli kutuweka kwenye makundi hayo? Kwa msingi huo kamati kuu ya mashindanshano haya imekubali timu ya Bongo kufagia viwanja vyote vya michezo hivyo kuweza kubahatisha kuokota medali ambazo nchi nyingine zitakuwa zimetupa hovyo kwa kuwa hawana haja nazo, na hivyo na Wabongo wetu waweze kurudi na medali na kupokelewa Tandale kama Diamond. Tunasubiria picha ili mujionee wenyewe laiv

1 August 2014

SAMAHANI NATAFUTA DEREVA WA TAXI AMBAYE.....................

Jamaa alikuwa anaumwa akapita kituo cha taxi akaikuta taxi moja, akamuomba sana taxi dreva ampeleke hospitaji lakini fedha yake ilikuwa ndogo, kitu cha ajabu dreva alimporomoshea jamaa matusi ya nguoni na kumwambia akapande bodaboda kama hana hela. Wiki mbili baadae jamaa akawa amepona na anapesa mkononi, akaenda kituo cha taxi akakuta taxi nne ikiwemo ya yule dreva aliyewahi kumtukana, akamwendea dereva wa kwanza;
JAMAA: Samahani natafuta dereva wa taxi shoga niondoke nae ntamlipa laki
DEREVA 1: We mwenda wazimu nini hebu toka hapa kabla sijakuwasha vibao, yaani unaona mie shoga?    Jamaa akenda taxi ya pili
JAMAA: Samahani  natafuta dereva shoga niondoke nae ntamlipa laki 2
DEREVA 2: Pumbavu mkubwa toka hapa. Hatimae jamaa akaenda kwa yule taxi dreva aliyewahi kumtukana
JAMAA: Aise nahitaji nikodi gari yako kwa shughuli za mzunguko kama wa masaa mawili hivi inawezekana?
DEREVA: Kwanini isiwezekana hiyo ndiyo kazi yangu, ingia tutaelewana tu.
JAMAA: Haya twende....wakati wanaondoka jamaa akahakikisha anapungia mkono wale madereva waliobaki kituoni huku akionyesha alama ya kidole gumba. Akiwaacha midomo wazi

MAGALIZETINI WAMESEMA ETI......................

 Itakuwa alikuja na moka mazoezini huyu...

 Nani anabisha? hahahahahahahahahahahaha

 No COMENT


BREAKING NEWS SHILOLE KUGOMBEA UBUNGE WA IGUNGA.........

SIO MIMI NILIYESEMA NI GALIZETI