PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

WABRAZILI WASABABISHA NDOA IYUMBE


OFISI ya blog hapakukalika jana , palikuwa hapafai, Wabrazil wameleta matatizo makubwa. Kabla ya mechi, Bosi Mkuu na Bosi wa Blogu hii na Bosi wa matangazo ya Blogu (ambayo hayapo), waliwekeana dau kuhusu gemu la Ujerumani na Brazil. Bosi Mkuu asema Ujerumani itashinda, bosi wa matangazo kaaapa Wabrazili wataiadhiri Ujerumani kwa bao mbili. Tatizo wakawekeana dau, Bosi mkuu akaahidi kutoa alfu hamsini, bosi wa matangazo katangaza kuwa wakishinda Wajerumani, atamtoa mkewe kwa usiku mzima kwa bosi mwenzie. Matokeo mnayajua. Kibembe kikaanza Bosi Mkuu kung’ang’ania ahadi itimizwe, mke aletwe kati, ajifaidie usiku kucha. Kelele kubwa ikazuka, ngumi zikakunjwa japo hazikurushwa, hatimae ikaonekana mke apigiwe simu kuelezwa kuhusu ahadi ya mumewe (ambaye wakati huo alikuwa akilia na kusema Nilikuwa natania tu sikumananisha kikwelikweli). Mamaa kupigiwa simu, kuwa anatakiwa akalale kwa mubosi usiku mmoja, akajibu bila mawimbi, ‘ Kama mume wangu aliona poa kuniweka rehani basi wacha nitangulie kwa bosi kulipa deni”

Comments