PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

MDADA MWENYE JINO BOVU, ATAKA KUMBAKA DOKTA WA MENO KIBAHATI MBAYA


MGONJWA WA MENO
“Mimi nimekuja kung’oa jino, linaniuma leo sijui siku ya ngapi? Lakini huyu daktari nimefika akanitaka kimapenzi. Nilidhani anatania, baadaye nikagundua kuwa amedhamiria,” alisema mwanamke huyo ambaye alikutwa ameshavua dera.

UTETEZI WA DAKTARI
Hata hivyo, daktari huyo hakumwacha mgonjwa wake huyo atambe kiasi hicho, alijibu mapigo kwa kusema kuwa, alimpokea mwanamke huyo kama mgonjwa wa jino na kumwingiza kwenye chumba cha kung’olea meno lakini ghafla alimwona akianza kuvua nguo zake kisha kumvua na yeye shati na baadaye kutaka kufungua zipu ya suruali.
Akiendelea kuzungumza mbele ya Polisi wa Kituo cha Kigamboni waliofika kwenye sakata hilo ndani ya chumba cha matibabu ya meno, daktari huyo alisema:
“Mimi sikuwa na nia mbaya, nilijua ni mgonjwa anataka tiba ya kung’olewa jino.
“Sasa nikiwa katika maandalizi ghafla nikamwona anavua nguo na kisha akanivaa mimi na kuanza kunivua shati. Nashangaa sana anaposema nilimtaka kimapenzi, si kweli jamani.”

Comments