PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

DAWA YA WANAOLETA SIASA NDEEEEEFUUU MPAKA HARUSINI


Duniani kuna binadamu halafu kuna wanasiasa. Binanamu wengi huwa wajitahidi kuwa wanasiasa na siku hiozi kila kona wamejaa na wanaboa kweli. Kazi kubwa ya mwanasiasa ni kuongea, wakitumia mdomo wao wanaweza kukufanya uamini kuwa wao ndio wanajua kila kitu. Tena wanasiasa wengine huwa wanafikia kuamini wanajua kila kitu. Ukimuuliza kuhusu kilimo anajua, uvuvi anajua, teknolojia yoyote anajua, we anzisha mada mwanasiasa anajua na atakupa majibu ya namna ya kuboresha kila kitu hata kama hajawahi kukifanya wala kukisikia. Huyo ndio mwanasiasa na wako wengi, kwa kuwa fani yao ni kuongea ukikosea ukawaruhusu waongee utajuta kuzaliwa, wao hawajali muda gani unawasikiliza  wao wataongea tu. Lakini leo nataka niwapeni dawa yao. Hawa wanasiasa wako kila mahala, mradi wakijua kuna watu wanawasikiliza basi hufungua maktaba ya ujuzi wao, na siku hizi wameingia kwenye sherehe na misiba.  Mtu anaalikwa mgeni rasmi kwenye sherehe, kabla ya chakula anaombwa azungumze, hilo linakuwa kosa. Kitu cha kwanza ukitaka  kujua anaeanza kuongea ni mwanasiasa, utasikia wana kasentensi kao wanako anazia utasikia,”Ndugu zangu hapa kwa kweli si mahala pa hotuba kwa hiyo sitasema mengi…….” Akianza hapo  ujue nusu saa itapita bado anaongea. Au kwenye sherehe za harusi baba mzazi akiambiwa atoe usia basi tabu imeanza ataongea historia toka alipokuwa mtoto mpaka alipooa na hatimae kuzaliwa wanooana  na ataendelea hamalizi. Dawa yao nimeipata, Siku hizi kuna watu wanaalikwa kutoa machache msibani, kabla ya mazishi au baada ya mazishi, basi ndio utajua kuna mwana siasa, ataongea mambo kibao hayana hata uhusiano na msiba. Dawa yao leo nakupatia. Ukishasikia mtu kaanza kale kasentensi kao kanakoanzia, “Hapa sio mahala pa kutoa hotuba…..” ujue mwanasiasa kaanza kaanza kazi yake. Ukiona kaongea anakuchosha, au anaongea kabla ya chakula mpaka chakula kinapoa haachi hotuba, au anaongea mno kabla ya mazishi na muda unapita bila sababu, dawa yake ni hii. Chukua karatasi andika maneno manne tu , kama mwanasiasa ni mwanaume mwanaume  andika SAMAHANI MZEE ZIPU IMEFUNGUKA… kama mwanasiasa ni mwanamke andika….SAMAHANI MAMA  SIDIRIA  IMEACHIA….hakikisha kijikaratasi hicho kinapita mpaka kumfikia mwanasiasa wako. Sekunde mbili baada kusoma kikaratasi hicho, Utasikia “Kwa hayo machache namalizia hapo”….MAKALA KAMA HII HUTOKA KILA JUMATANO KWENYE GAZETI LA RISASI

Comments