BOSI WA BLOGU HII SI KAZAMIA MKUTANO WA WATAALAMU TOKA MARIKANI..KUWA WA KWANZA KUJUA MATOKEO


Huyu Bosi wetu Mkuu ana mambo, juzijuzi si walikuja wataalamu wa muziki toka majuu kuja kufundisha ujanja wa kupata hela kwa wasanii wa Bongolend mjini. Wasanii muhimu wakakaribishwa mahala kupata ilimu. Basi mubosi wa blogu hii nae eti akafoji kuwa nae msanii akajitoma kwenye ukumbi, na suruali yake iko nusu mlingoti, na kikofia cha Mungu usinione kakigeuza nyuma mbele, ungemuona ungeamini nae msanii supasta, maana hata kutembea akawa anatembea kama chupi inabana. Si akakaa kwenye kona moja kimyaa, huku kavaa hedfon kama anasikiliza kitu kumbe hedfon zimeishia mfukoni hazijaunganishwa popote. Ndio wakaingia wataalamu, kuwacheki kumbe waswahili tu, akacheka kimoyomoyo, na kujitayarisha kuwauliza maswali magumu, kwa mfano alitaka kujua je, Puff Dady kuwa anajichora tatuu za mademu zake? Je akiachana nao inakuwaje? Au je, Tupac anaweza kuja kupafom ukumbi wa Kihesa Kilabu Kihesa Iringa mjini?
 Shida ikaanza wataalamu walipoanza kuongea, salaleeee wakaanza kuongea kikwao, mubosi kila akisiliza hola, kila akisikiliza hola, anaishia kusia “ya men”. Sijui nini na nini wanaishia ‘Ya men”. Kila akiangalia pembeni kumezunguka masupasta wa Bongolendi wanapiga makofi wanacheka, konyesha kuwa mubosi peke yake ndio haelewi kitu. akawa anangojea kachansi aulaze, ile alivyosikia, ‘Jamani kuna chai twendeni kunywa” Aliondoka bila swaga wala kuaga huyoooo kaja kujifungia ofisi ya blog kanuna huyo, nasikia anatafuta chuo cha kujifunza Kiinglish….msimwambie ohoooo

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.