BOSI WA BLOG HII, MZEE WA MICHEPUKO, AUMBULIWA NA MNADA WA SIMU BEI NUSU

Hii ni siri sana, maana Bosi wa hii bulogu kachanganyikiwa, hajui la kufanya. Michepuko inamponza. Ishu yenyewe iko hivi, wajanja wa mujini fulani juzi kati wakatangaza watakuwa na fiesta ya kuuza simu bei nusu, sasa bosi wetu alikuwa kasha ombwa simu na michepuko miwili si akaona hapa ndipo pa kupata simu mbili kwa bei ya simu moja, maana hesabu zinasema kama simu moja bei nusu, basi simu mbili bei kamili. Bosi akanituma niende duka la jirani kuulizia Nokia X bei gani? Kule wakanambia simu moja ni shilingi laki mbili salasini. So nikamwambia bosi, akachekelea kweli namuona kanyanua simu kamwambia mchepuko wa kwanza bebi unataka Nokia X? bebi wa kwanza wa kwanza akakubali. Bosi kapiga simu kwa bebi wa pili, akamumuliza kwa msisitizo, "Hani you want a Nokia X?” Hani nae akakubali, maana bosi alikuwa na laki mbili na hamsini si  akajua ataua simu mbili kwa jiwe moja.
Bosi huyoooooo mpaka kwenye fiesta ya simu za bei nusu, akakuta mambo yamepamba moto, kuna mdada na mkaka walikuwa wanatangaza kwenye maspika ‘Njooni reo simu ni bei nusu, Samsung, nokia, huaiwei, na kazarika, hii ni nchi ya Mwarimu Nyelele’ hawa watangazaji walikuwa na kale kaugonjwa kakusema Raa penye Laa, na Lee penye Ree, si mnawajua aina yao?. Mubosi akaenda stret kwenye kibanda cha kuuzia simu, akakuta misimu ya Nokia X kibao, kwa mbwembwe kasema, ‘Nifungie Nokia X mbili” . Wakamkaribisha sana na haraka simu zikatolewa bosi akaombwa mkwanja, si akatoa laki mbili na nusu na akawa anangojea chenji, wakamchenjia yeye, ‘We mzee vipi tena, mbona pesa pungufu?” Bosi akaja juu,”Pungufu vipi? Nokia X shilingi laki mbili salasini uswahilini hapa si mmesema bei nusu so si shilingi laki moja kumi na tano?”, ‘We mzee usituzingue bwana Nokia X shilingi laki mbili leta au sepa” Bosi mkojo ukambana…..'Jamani si mlitangaza punguzo asilimia hamsini, hiyo maana yake si nusu bei?' ‘We mzee hayo yako laki mbili kwa Nokia X moja”…Bosi wangu ili asiumbuke akalazimika kununua simu moja na saa hizi hapokei simu ya bebi wala hani maana hajui atampa nani simu…hii habari ni siri lakini msimwambie Mubosi

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.