HATUPIMI BANDO

31 July 2014

NATAKA FACEBOOK BARIDI

Jamaa yangu kaenda kule kwa watani zangu, jioni kidogo katika mizunguko akapata mwenyeji, wakaelekea bar ya jirani....wakati wa kumngojea mhudumu maongezi na mwenyeji yakawa yanaendelea;
JAMAA: Wakunyumba unatumia Facebook?
MDADA: San tu, lakini iwi baridi sana, ikiwi ya motuhuwa nalewa mapema

BREAKING NYEUSSSSSSSI --KALEWA MPAKA KATAGA MAYAI

Jamaa katoka ulevini kalewa sana kama kawaida, akanyata chumbani kwake, ili mkewe asiamke akaingia ndani ya shuka, haikuchukua muda akawa katika uingizi mzito. Ghafla akaamka akakuta kumesha kucha, ila kitu cha ajabu akakuta pembeni yake kuna mwanaume badala ya mkewe. Akamuuliza yule mwanaume, "We nani na umekujaje chumbani kwangu?". Yule mwanaume akacheka sana,'Hahahahahaha chumbani kwako? Hapa si chumbani kwako hapa ni ahera, na mimi ndie shetani mkuu Lusifa". Jamaa, "Una maana nimeshakufa?", 'Haswaaa, toka ulipotoka ulevini jana". Jamaa akakaanza kulia na kulalamika," Haiwezekani jamani mi bado kijana kuna mambo mengi nilikuwa sijamaliza, chonde chonde Mzee Lusifa nirudishe duniani japo mwaka mmoja". Lusifa akamuangalia jamaa kisha akamwambia ,"Okay lakini huwezi kurudi duniani kama binadamu, labda urudi kama kuku au panya au mjusi" Jamaa akachagua kurudi kama kuku. Basi fumba na kufumbua akajikuta yuko duniani akiwa na kuku wenzie kwenye banda. Akawa kajikunyata hajui hata aanzie wapi, ghafla akajisikia hali ya aajabu akajua anahisi kutaga yai. Akajivuta pembeni kwenye kona, na kuanza kujikamua kwa nguvu, yai la kwanza likatoka, akajisikia nafuu, kisha akajikuta anataka kutaga la pili akajikamua kwa nguvu huku akitetea, yai la pili likatoka....na ndipo hapo aliposikia kofi la nguvu shavuni na sauti ya mkewe ikifuatia,"Mshenzi mkubwa wewe, ulevi wako sasa mpaka unakunya kitandani zoa uchafu wako haraka"

BLOGU YENU YATOA TUZO LA NANILI LA DHAHABU KWA FALA WA MWEZI ..KUWA WA KWANZA KUONA VIDEO

Tuzo la Nanili la dhahabu
 Pokea tuzo hii dreva wetu Mungu akusaidie akupe akili .
Blogu yenu makini imeona impe tuzo ya Nanihii la Dhahabu dreva huyu aliyekuwa akiendesha gari huku anajirekodi alioona ujanja. Kwa barabara zetu hizi huyu alikuwa anahatarisha maisha ya watu wengine kwa ufala wake huu.

TUZO YA BLOGU KWA FALA WA WIKI

tuzo la nanihii la dhahabu
BLOGU INARUDIA ILE TARATIBU YA KUTOA TUZO LA NANIHII LA DHAHABU KWA FALA ATAKAEWEZA KUSHINDA MAFALA WENZIE .
 WIKI HII TUZO LA NANIHII LA DHAHABU LINAENDA KWA DREVA WA DALADALA HILI AMBAYE NI WAZI AKILI KAACHA NYUMBANI, KWA KUWEZA KUHATARISHA MAISHA YA ABIRIA AMBAO NAO WANASHIRIKISHWA KWENYE HILI TUZO KWA KUUNGA MKONO KWA WAO PIA KUACHA AKILI NYUMBANI NA KUTOKUPINGA KITENDO CHA DEREVA HUYU............

30 July 2014

MKE WANGU KUSANYA NGUO ZAKO UNIPE NIFUE

JAMAA alikuwa kagombana na mkewe, hatimae akamwambia mkewe kwa ukali, "Unajua nimechoka sasa haya kusanya nguo zako na......" Kabla hajamalizia sentensi simu ya mkewe ikalia, kumbe alikuwa ni baba mkwe. Basi mzee akaanza kuongea na binti yake baada ya salamu,  na katika kile kimya Jamaa kasikia mkwewe akisema, " Aise binti nimebahatika nimeuza ile nyumba yangu ya Moshi sasa nimeona niwatumie milioni 20 mjaribu kuanzisha mradi na mwenzio, haya mwambie ntampigia kesho, kama ana mradi mwingine nimpe fedha kidogo". Baada ya simu kukatwa mke akamgeukia jamaa akamuuliza 'Ehe ulikuwa unasema umenichoka nikusanye nguo na ni kiwe nini?' Jamaa kwa upole akajibu, " Nilikuwa nasema ukusanye nguo zako na unipe nifue"

MBWA WETU ANAJUA KUSOMA NA KUANDIKA


Tajiri wa kijiji aliyekuwa anapenda sana sifa,alifanya kila jitihada mwanae ajiunge na chuo kikuu kimoja ili awe mtu wa kwanza kijijini kuwa na digrii. Yanki alijiunga na chuo lakini baada ya miezi michache akaishiwa pesa, akawaza atapataje pesa toka kwa mzee wake? Akapata wazo, akamuandikia baba yake barua.
 'Baba mpenzi huku chuoni mambo mazuri sana, naendelea vizuri sana na masomo mpaka wanataka kunipeleka Ulaya, nia na madhumuni ya barua hii ni kukwambia baba kuwa kuna maajabu makubwa sana. Hapa chuoni kuna profesa amegundua njia ya kufundisha mbwa kuongea, baba mlete mbwa wetu BINGO na ada ya shilingi laki 5, baada ya mhula mmoja atakuwa anaweza kuongea kama binadamu. Wasalam mwanao.’
Mzee wa watu haraka akatuma mkwanja na mbwa.  haikuchukua muda mkwanja ukaisha. Denti akamtumia baba yake barua nyingine kuwa wameboresha elimu sasa wanaweza kumfundisha BINGO kusoma, mzee aongeze kamilioni tu. Mzee wa watu aliyekuwa tayari anajisifu kijiji kizima kuhusu mbwa wake atakaerudi anaongea,  haraka akauza ng'ombe akatuma mkwanja. Likizo ikafika Denti akabaki anawaza anaenda kumwambia nini baba yake kijijini, maana uwongo wake ulishafika ukingoni. Alipofika tu kwao  baba yake akamuulizia BINGO. Denti akamuita baba yake pembeni,' Baba hili nitakalokwambia sitaki mama asikie'. Baba akauliza,'Vipi tena?'. Denti akaanza,' Jumatano iliyopita tumeamka vizuri na BINGO, yeye kama kawaida yake akaenda kununua gazeti la Risasi kama kawaida yake maana alikuwa tayari ameshajua kusoma. Akarudi na gazeti akakaa kwenye kiti na kuanza kusoma, wakati huo mimi nilikuwa najitayarisha kuingia darasani, ghafla BINGO akaniita akanambia hivi, 'Baba yako huyu vipi?’, nikamuuliza ,’Kwani vipi?’ Akaniambia,’Naona babako bado anaendelea na kale kachangudoa ka kijiji pale mtaa wa pili, naona hapa wameandika stori yake yote humu, nikirudi kijijini namwambia mke wake', Baba kwa kweli  nilishtuka. Mzee akaingilia kati,'Ungemuua hapo hapo mbwa mshenzi huyu nampeleka shule yeye anataka kuniharibia mambo yangu?', Denti akajibu,'Baba na mimi lilinijia wazo hilohilo sikumchelewesha nikamtwanga nyundo ya kichwa'. Baba akamsifu mwanae'Safi sana, safi sana mwanangu, una akili sana huyu mbwa angetuharibia familia mwanangu'............IMETOKA CHEKA NA KITIME GAZETI LA RISASI JUMATANO 30/7/2014.

29 July 2014

UNAONA NILIKWAMBIA MUME WANGU ZUZU

Jamaa kaingia ghafla chumbani kwake akamkuta mkewe kajifunika mashuka na mwanaume mwingine;
JAMAA: Mke wangu mimi hiki sasa unafanya nini na huyu mwanaume?
MKE: (Akamwambia mchepuko wake) Si unaona nilikwambia mume wangu zuzu, si unasikia swali alilouliza?

26 July 2014

MKE WANGU UKIFA LEO NA MIMI NAKUFA


MKE: Nikifa leo hivi utajisikiaje?
MUME: nami nakufa muda huohuo
MKE:Pole mume wangu unanipenda sana?
MUME: Naona furaha itanizidia mpaka ntapata shinikizo la damu na kufa siku hiyohiyo

23 July 2014

DENI LA LAKI SITA NDIO CHANZO...KUWA WA KWANZA KUJUA

Mabosi wa blogu hii makini kuliko galizeti la nanihii, walilazimisha ufanyike utafiti eti kwanini watoto wachanga wakizaliwa tu lazima waanze kulia. Mamilioni ya fedha yalitengwa kama njia ya kuwezesha kufanya utafiti wa kina kuhusu swala hili. Kampuni kadhaa zilileta tenda ya kufanya utafiti huu lakini bosi wa tenda wa blogu si akampa mdogo wake tenda hiyo. Huyu dogo ambaye utafiti wa kamati ya tume ya utafiti umekuja gundua kuwa hakumaliza hata seven ndie aliukwaa mradi huu wa mamilioni. Dogo amekuja na ripoti ya mistari michache kuwa, kumbe ishu nzima ni deni la Taifa. Kwa kuwa deni la Taifa linaonyesha kuwa kila Mbongo andaiwa laki sita kesh, basi  we fikiria maskini kiumbe huyu anazaliwa hamjui mtu, hana nguo, wala hajaongea na mtu wala hajala cha mtu, tayari anakuta ana deni la shilingi laki sita, lazima alie na kujilaumu kwanini kazaliwa Bongo...

MATUMIZI BORA YA SIMU KWA WENYE MICHEPUKO


Jamaa zangu wengi sana wanapata taabu sana kwa sababu ya simu. Kidude hiki ambacho kinatakiwa kitupunguzie shida katika maisha chenyewe ndio kimekuwa shida kubwa. Mtu unakuwa huna raha kabisa shauri ya kidude hiki why? Jamani Why? Kuna hii ishu ya kuwa na mchepuko, kimsingi hili jambo gumu kumalizika , kwa hiyo sihangaiki kuwambia watu wache, huko ni sawa na kukataza jua lizizame, na pia hayanihusu. Mtu anakuwa na mchepuko wake, na sijui kwa nini michepuko ina tabia ya kuwa haina taimingi, pale mazahaus ndo uko nae, mchepuko ndo unapiga simu.  Ili kukwepa maswali watu wanaweka simu kwenye silent, wengine vibrashen, chondechonde usiweke kwenye vibreshen, mazahaus wote wana machale kishenzi, lazima utasikia ‘nani huyo? mbona hupokei?’ Maswali la hatari sana usikubali yakutokee, hivyo daima weak simu  kwenye silent. Japo tatizo la michepuko mingine usipopokea ndio haachi kupiga.
 Ukiwa na mchepuko we sevu jina lake mjomba, au shangazi au ba mdogo, usiandike fundi majeneza au fundi pikipiki, imeshapitwa na wakati hiyo, utastukiwa. Ni vizuri kufanya mazoezi ya kuekti kwenye kioo ili wakati unasema uongo uso uwe umetulia kabisa wakati unajibu uongo, maana unaweza kulazimika kupokea simu ya mchepuko, mazahaus yuko mbele yako, ikalazimika uanzishe kujibu simu za kujidai unaongea biashara ya kuondoa kontena lililokwama, hapo lazima uekti vizuri kuliko msanii wa Bongomuvi. Ili kupunguza mitihani hii, jamaa yangu mmoja wa Kiluvya amempangia mchepuko muda wa kupiga simu hii imemuondolea adha ya kulazika kupokelea simu chooni na bafuni.  Kwa hiyo tafadhali wandugu tena chonde sana yale mnayochati futeni, hata kama lilikuwa neo tamu kama I love you my Chokoleti futa usitake sifa, au litakukosti ohoo. Amri kuu ya simu ukiwa na mchepuko ni kuwa unatakiwa kuibeba popote utakapokuwa, bafuni chooni, msibani harusini usingizini, ukimuachia nafasi mazahaus aibebe umekwisha. Pia kama una mchepuko, ni muhimu sana umpe semina na warsha na kongamano mchepuko wako kuhusu nini cha kusema ikiwa kwa  bahati mbaya simu ikiangukia mikononi mwa mazahaus. Asianze samahani nimekosea namba, hiyo imepitwa na wakati. Yeye cha kufanya ni kuongea kwa konfidens kabisa na kuulizia kwanini hujakamilisha ripoti ya kazi, au kama we fundi gereji aulize gari lake mbona breki na taa hazifanyi kazi, au kama wewe ni dokta aombe ushauri kuhusu dawa ya pumu kwa ajili ya bibi yake aliyeko kijijini. Kikubwa asipaniki. Somo hili litaendelea ,,,,,,,,,,,,,,,,,,TOKA CHEKA NA KITIME..GAZETI LA RISASI 23/7/2014

LAPTOP ILIYOIBIWA IMESHAUZWA ZAMBIA

Mkuu wa manjago alikwenda acha  gari lake lioshwe  sehemu fulani. Aliporudi akagundua haioni laptop yake. Akawapigia askari wake wakaja wakawakusanya waosha magari wote pale jirani na kuondoka nao. Kesho yake asubuhi mkuu akapigiwa simu na Mchepuko wake kumkumbusha kuwa toka jana yake alikuwa kaacha laptop. Mkuu ndio akakumbuka kosa lake akawapigia askari wake na kuwaambia wawaachie wale waosha magari. Askari wakamjibu, 'Mkuu mbona umechelewa? Wote tumeshawapeleka mahakaman maana baada ya kuwahoji usiku kucha wamekubali kuwa waliiba hiyo laptop na wameshaiuza kwa mfanya biashara wa Kizambia. 

22 July 2014

KAMCHAKATO KA VAZI LA TAIFA


HIVI 2+2=?


Kulikuwa na tangazo la kazi, watu watatu, mwanafuzi, mhasibu na mwanasiasa wakapeleka maombi, siku ya usaili wakafika tayari kwa usaili;
MSAILI: Je 2+2 ni ngapi?
MWANAFUNZI: 4
MSAILI: Haya nenda tutakujibu, niitie mwenzio
MSAILI: Je, 2+2 ni ngapi?
MHASIBU: Kwa ujumla ni 4, inaweza ikazidi kidogo au kupungua kidogo kwa asilimia kama 10 hivi lakini ni 4
MSAILI: Duh haya nenda tutakuita, niitie mwenzio
MSAILI: Je 2+2 ni ngapi?
MWANASIASA: Kitu kikubwa hapa ni kuangalia mwenendo wa wapiga kura, haya mambo unaweza ukajibu kwa harakaharaka ukakuta mambo yamebadilika yakakukosti kwenye uchaguzi. Kimsingi kwanza ni muhimu kujua msimamo na muelekeo wa Chama chako, na pia kuangalia je jibu lako  lina matokeo gani katika muktadha mzima wa swala lenyewe.
MSAILI: Hebu jibu swali 2+2 ni ngapi?
MWANASIASA:(Kwa sauti ya chini) We unataka iwe ngapi bosi?

MAGALIZETI
21 July 2014

HAHAH VICHWA VYA HABARI VYA MAGALIZETI YETU HAHAHAHAHA

                                             DAH

                                               DUH

                                           LOH

                                        HEE

 KWA HIYO KABAKI NA SHAVU MOJA TU?

 ITAKUWA NGUMU WATATUMIA KUFULI GANI?

                                   NDIO KUSEMA?

                                          OHOO

 KULE KWA WAZIRI MKUU CAMEROON!!!!!!!!!!!

                                            AMANI?

                               IS ENGLISH IS HARD

20 July 2014

KIDIJITALI ZAIDI....MGANGA ATUMIA GUGO KUAGUA WAGONJWA

Mdada alienda kwa mtaalamu amuangalie mambo yake maana aliona mumewe ameanza kupunguza mapenzi. Baada ya kujieleza, mganga akatoa Laptop yake akaunganisha intanet kisha akaanza kugugo. Baada ya dakika kadhaa akiwa anaongea mwenyewe na kuonekana akiperuzi fesibuku na twira akainua kichwa;
MTAALAM:Mdada, tatizo lako nimeliona linahitaji fedha kiasi cha laki na nusu.
MDADA: He jamani hela yote hiyo ya nini?
MTAALAM: Mama mambo yamebadilika sana, siku hizi ili kuwasiliana na mizimu lazima uwe na intanet sasa  mimi hapa nimeweka WIFI na ni gharama maana ili kuskype na mizimu inaweza ikanichukua hata wiki kumpata muhusika. Sasa hapo hiyo hela mama ni ya kulipia internet tu ili kupata maelelzo ya matibabu yako
MDADA: Mzee nimeshindwa mimi.

19 July 2014

UNAMJUA ALIYEGUNDUA KUJIPIGA SELFIES? KUWA WA KWANZA KUMUONA

STAILI YA KUJIPIGA PICHA MWENYEWE MAARUFU KAMA SELFIE KWA SASA NI KITU CHA KAWAIDA. Je unajua nani aligundua kujipiga selfie? Ni huyu hapa

HELP ME PLEASEEE


DOKTA NINA MAUMIVU MAKALI

JAMAA: Dokta nipe dawa nina maumivu makali
DOKTA: Maumivu yameanza lini?
JAMAA: Yaani toka jirani yangu kanunua Bodaboda roho inaniuma sana

18 July 2014

HAYA WOTE TOKENI NJE


Bonge ya mnuso ulikuwa unaendelea tatizo likawa WAZAMIAJI  ndio walikuwa wengi zaidi, mwenye shughuli akaskuut atawatambuaje, akasimama akatangaza.
MWENYEJI: Wale ndugu wa bibi harusi simameni hamieni viti karibu na lango ili mpokee zawadi maalumu.....jamaa kama 20 hivi wakahamia huko
MWENYEJI: Wale ndugu wa bwana harusi nao wahamie viti jirani na hao wenzao....watu kama 30 wakahamia.
MWENYEJI: Haya wote nyie tokeni nje maana hii ni birthday party yangu hakuna harusi hapa

BAADA YA KICHAA CHA SELFIE, SASA KIMEONGEZEKA CHA GROUNDIE

BAADA YA SEMINA BOSI ANUNUA SURUALI MPYA

BAADA YA KUHUDHURIA SEMINA YA KIZUNGU, BOSI KANUNUA SURUALI MPYA

17 July 2014

BOSI WA BLOGU HII SI KAZAMIA MKUTANO WA WATAALAMU TOKA MARIKANI..KUWA WA KWANZA KUJUA MATOKEO


Huyu Bosi wetu Mkuu ana mambo, juzijuzi si walikuja wataalamu wa muziki toka majuu kuja kufundisha ujanja wa kupata hela kwa wasanii wa Bongolend mjini. Wasanii muhimu wakakaribishwa mahala kupata ilimu. Basi mubosi wa blogu hii nae eti akafoji kuwa nae msanii akajitoma kwenye ukumbi, na suruali yake iko nusu mlingoti, na kikofia cha Mungu usinione kakigeuza nyuma mbele, ungemuona ungeamini nae msanii supasta, maana hata kutembea akawa anatembea kama chupi inabana. Si akakaa kwenye kona moja kimyaa, huku kavaa hedfon kama anasikiliza kitu kumbe hedfon zimeishia mfukoni hazijaunganishwa popote. Ndio wakaingia wataalamu, kuwacheki kumbe waswahili tu, akacheka kimoyomoyo, na kujitayarisha kuwauliza maswali magumu, kwa mfano alitaka kujua je, Puff Dady kuwa anajichora tatuu za mademu zake? Je akiachana nao inakuwaje? Au je, Tupac anaweza kuja kupafom ukumbi wa Kihesa Kilabu Kihesa Iringa mjini?
 Shida ikaanza wataalamu walipoanza kuongea, salaleeee wakaanza kuongea kikwao, mubosi kila akisiliza hola, kila akisikiliza hola, anaishia kusia “ya men”. Sijui nini na nini wanaishia ‘Ya men”. Kila akiangalia pembeni kumezunguka masupasta wa Bongolendi wanapiga makofi wanacheka, konyesha kuwa mubosi peke yake ndio haelewi kitu. akawa anangojea kachansi aulaze, ile alivyosikia, ‘Jamani kuna chai twendeni kunywa” Aliondoka bila swaga wala kuaga huyoooo kaja kujifungia ofisi ya blog kanuna huyo, nasikia anatafuta chuo cha kujifunza Kiinglish….msimwambie ohoooo

MAVAZI YALIYOKATAZWA aka FORBIDDEN DRESSES

Kutokana na ubishi wa watu wengine imelazimika kuweka ubao huu wenye maelezo yaliyowazi kabisa. So sisi kama blog makini tumeona tukumbushie hii ishu ili wale wabishi wanaopitia blog hii wajirekebishe. Ubishi ukiendelea tutaomba tenda ya kucharaza watu viboko pale getini au vipi?

AFANDE KWANI BANGI NDIO NINI?

Dogo kakamatwa na polisi akiwa na bangi mfukoni;
POLISI: Kijana unatembea na bangi, hii ni jinai
DOGO: Afande mi naona nimelogwa hiyo bangi kila nikiitupa chooni unakuta imerudi mfukoni mwangu
POLISI: Acha kunifanya mie fala twende kituoni
DOGO: Kama huniamini afande tumbukiza chooni utaona imerudi mfukoni mwangu toka jana inanisumbua....
POLISI: Natumbukiza tuone ukinidanganya ndipo utakapojua Dola maana yake nini......afande akatumbukiza bangi chooni
POLISI: Haya hebu toa hiyo bangi sasa mfukoni
DOGO: Bangi? bangi gani?
POLISI: Si ile ulisema inarudi mfukoni mwako?
DOGO: Afande mi sikuelewi kabisaa, mi na wewe tulizungumza wapi kuhusu bangi? Mi naijulia wapi bangi? Au unataka kunibambikiza kesi ya bangi afande?

16 July 2014

ANATAKA KUGOMBEA URAIS LAKINI ANA TATUU, BLOGU HII YAJITOKEZA KUMSAIDIABlog yenu imegundua kuna  jamaa zetu wengi wamejikuta wakiwa na tatuu ambazo wakati wanazichora walijiona wajanja saaaaana. Wengine waliandika mjina ya wapenzi wao wengine walichora picha na kadhalika. Sasa shida imeingia mapenzi yamekwisha hawana haja tena ya tatuu hizo, wengine wanajiona sasa umri umekuwa mkubwa tatuu zinawafanya waonekane hawana akili, bosi wa hii blog  anataka kutangaza nia ya kugombea urais 2015, tatuu itamharibia dili, njooni kwetu blog imenunua  mashine ya kuondoa tatuu toka China kusini katika jimbo la Toa Ta Tu, mashine hii ambayo inaendeshwa na mtaalamu mwenye digrii ya Saikolojia ya Uchizi , ataweza kukutoa tatuu katika kipindi cha dakika tatu tu.

KULIMA LAMI DILI KUBWA


Siku moja nilikuwa nasikiliza wimbo mmoja wa Malkia wa Mipasho Bi Khadija Kopa, alikuwa anawapasha wakuja kuwa wasije na majembe mjini watalima lami. Nikacheka sana na kujiuliza fala gani atakuja mjini kulima lami? Si atakufa kwa njaa jamani. Sasa juzi nimebadili mawazo, nimegundua kumbe kulima lami ni bonge ya dili. Kuna kabarabara fulani kako mitaa ya ndani ndani kule Kijitonyama Dar es Salaam mjini. Haka kabarabara kama miezi sita iliyopita hivi kakafungwa kama wiki kadhaa kakapakwa lami. Miezi miwili badae lami si ikaanza kubanduka, lile bonge la mvua lililoanguka baada ya hapo ndio likafuta kabisa kale kalami. Si ndio likaja hili dili la kulima lami. Jamaa flani wakaanza kufunga barabara upande mmoja wanalima lami kwa siku mbili tatu kisha wanafungua barabara  upande huo wanafunga upande mwingine wanaendelea kulima lami huko, ushafika mwezi wa pili sasa gemu hilo linaendelea, vibarua na vijamba koti vya rangi za kung’aa wanalipwa kwa kulima lami, lazima aliyewaajiri anachukua mpunga mzito, toka kwa wenye barabara. Jamaa hawa wakitaka kokoto za kujaza walipolima, wanakodi hivi visuzuki  vilivyokaa kama viloli vya kuchezea, ambavyo madereva wake wanaendesha utadhani wanaendesha vibajaji, wanakodi halafu wanaenda kuomba kokoto sehemu kuna mtu kamaliza ujenzi, wanakuja fukia pale walipolima. Kwa hiyo na mimi hili dili sitaki linipite, nina mpango wa kununua majembe manne, sululu mbili, na vile vijamba koti vyenye rangi ya kung’aa vinne, nikipata hivyo naanzisha kampuni natafuta kazi ili nami niwe naingiza mkwanja kwa kulima lami. Hili dili liko wazi kabisa.......makala hii ilitoka kwanza gazeti la RISASI JUMATANO 16/7/201

15 July 2014

BREAKING NEWS PATA TAARIFA YA HONG KONG HAPA

HONG KONG  ndio mji pekee duniani ambao jina lake unaweza kutamka bila kuchezesha ulimi wala midomo.....hahahahahahaha
cheki sura yako inavyokuwa kama huyu mchina unapofanya mazoezi ya kusema Hongkong

UKIJIFICHA BANA KILA KITU SAUTI ISITOKE


HALLOOOO NANI MWENZANGU?

MDADA: Baby mambo? Uko poa?
MKAKA: Poa baby vipi ushafika kwenu?
MDADA: ndio baby lakini kuna tatizo
MKAKA: Nini tena?
MDADA: Nilipofika nikaweka simu yangu kitandani, mume wangu kaichukua si akasoma mesej zako zote, sasa kanifukuza kanambia nije kwako, baby uko nyumbani nakuja
MKAKA: Halloo, Haloo, nani mwenzangu? Hallooo, netwek inasumbua hawa tigo hawa

YALIYOJITOKEZA MAGALIZETINI


 Sasa hiki nini tena mtu mzima kuongea na miti?

 Yashindwe na yalegee, kemea mzee

 Dah wakiwa wakubwa poa tu

 Ehhhh haya tena, mbeleko lazima iwe kubwa sana

 Wanauzwa au kukodishwa?

Kwa kiswahili ni kuwa Tanzania inaenda Golf ya maMiss Junior BISHA

11 July 2014

MAGALIZETI YA LEO
TOA MAONI..................


SAMAHANI MUDA UMEISHA

MZEE mmoja alikuwa hoi kitandani akajua anakufa akamwita mwanae wa kwanza wa kiume;
MZEE: Mwanangu mi nakufa chukua pisto yangu, hiyo itakufanya unikumbuke.
MWANA: Baba unajua mi sipendi mambo ya silaha, we nipe hata hiyo saa yako itatosha kwa kumbukumbu
MZEE: Pumbavu mkubwa unadhani mi mjinga kukwambia uchukue pisto? Iko siku utamfumania mkeo, sasa ukiwa na saa utafanya nini? Utaishia kumwambia mgoni wako, saa hizi saa 6 samahani ondoka muda umekwisha?

SUKUMA MKE WANGU

MUME:Sukuma kwa nguvu
MKE MJAMZITO: Mwanaume gani katili wewe
MUME: Sukuma bwana acha maneno
MKE MJAMZITO: Mungu atakulaani
MUME: We  sukuma bwana, usiposukuma ujue gari hili haliwezi kuwaka na wewe unatakiwa uwahi hospitali kujifungua, haya sukuma nshtue

10 July 2014

NANI KAKWAMBIA WAZUNGU HAWAJUI NDOMBOLO?


BREAKING NEWS NEYMAR AIKIMBIA NCHI YAKE AENDA KUJIFICHA KWENYE KIJIJI CHA TANANGOZI IRINGA

YULE  mchezaji nyota wa Brazil ambaye alikuwa majeruhi wakati wa mechi iliyoitia aibu nchi yake kaamua kukimbilia Iringa na kujificha huko huku akifuga ndevu asitambuliwe. Waandishi makini wa blogu hii waliweza kumkuta huko kwenye kilabu kimpja cha ulanzi na haya ndio yalikuwa mahojiano laiv
CHEKANAKITIME: Aise  Neima kamwene
NEYMAR:Kamwene
CNK: Vipi unaweza kututaja jina lako wasomaji wetu makini wakutambue na unafanya nini huku?
N: Jina langu Neima Sandoz huku nimejificha ili Wablazili wenzangu wasinisumbue
CNK: Naona umefuga na ndevu kabisa
N: Hata Kihehe nimejifunza halakahalaka siludi kule kalibuni mbaka mechi ziishe watu wasahau
CNK: Vipi ulanzi naona una bakuli kubwa sana?
N: Ulanzi unanifanya nipoteze mawazo naupenda sana, nikirudi kwetu ntaanzisha biashala ya ulanzi mpila sasa basi
CNK: Haya tunakutakia heri na baraka, umeshawasiliana na Maximo?
N: Hapana nikiona nataka kucheza mpila ntajiunga na Lipuli ya hapo Ilinga
CNK: Kila la heri
N: Adios Amigos

KUMBE KOMBE LA DUNIA LIKO BONGO...KUWA WA KWANZA KULIONA

Kisa cha Brazil kufungwa , kumbe walikuwa wanasusa, kombe la dunia lililoko kule kumbe feki, kombe lenyewe la ukweli limeonekana Bongo. Baada ya utata wa kombe kugundulika Wabrazil wakaamua kudharau mechi kwa kisirani.