PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

SIKU MOJA SUNGURA ALIMKUTA TWIGA ANAVUTA BANGI

SIKU  moja sungura alikuwa anakimbiakimbia msituni akifanya mazoezi ya viungo, akamkuta twiga anavuta bangi, akamwambia twiga,'Ndugu yangu kwanini unaharibu maisha yako kwa kuwa teja, achana na bangi nifuate mimi tufanye mazoezi'. Twiga akaona hilo ni wazo la busara akatupa bangi wakaongozana na sungura wakaendelea na mazoezi. Ghafla wakamkuta Tembo anataka kujidunga sindano yenye dawa za kulevya, sungura akamwambia tembo, 'Kaka achana na madawa ya kulevya unachekesha ulimwengu, jiunge na sisi tufanye mazoezi ya mwili'. Tembo akaona hilo la maana akajiunga nao wakaendelea kukimbia wakifanya mazoezi ya viungo. Muda si mrefu wakamkuta simba nae anataka kujidunga, sungura akamwambia simba, 'Mzee achana na hayo mambo ya uteja njoo tufanye mazoezi' Simba akakamata kasungura na kukacharaza viboko  vingi tu kabla tembo hajaamulia. Tembo akamwambia simba, 'Ndugu yangu nakushangaa, huyu sungura anatuambia jambo jema wewe unamtandika sio vizuri'. Simba akamwamba tembo,'Unajua haka kajitu kashenzi sana, kenyewe ni kavuta bangi, kakisha kolea kanapita kanakimbia na kuwaambia wengine wakafuate, hapo kalipo kamekolea bangi ndizo zinazokatuma kakimbie hovyo, kamesha nikimbiza msituni mara tatu kabla sijakagundua"

Comments