HATUPIMI BANDO

7 June 2014

PICHA ZA BOSI WA BLOGU AKIWA NA..... ZAVUJA ..MWENYEWE ATOA TAMKO ZITO-kuwa wa kwanza kusoma

Bosi wetu akiwa katika mkao tata na Rihanna
FUTA delete kabisa, yaani watu wenye nia ya kuniangusha kibiashara wameniphoto windowshopping eti niko na Rihanaa, jamani mimi huyu Rihana nimekutana nae mara moja tu pale Maisha club akaniomba soda ndio nikamnunulia, akaomba lifti nimpeleke Mango akacheze Twanga, hiyo picha ni pale alipokuwa akicheza wimbo wa Dunia daraja mi nikawa nyuma yake namlinda ndio baadae akaniomba nimpeleke Coco akapunge upepo maana alikuwa kaloa jasho, ndio mimi kwa moyo wangu wa ukarimu nikampeleka sasa watu wanasema ooo sijui nini na nini, jamani kwanini? kwanza shati nililovaa wala si langu kwanini mnataka kuniharibia hivi? Mke wangu saa haizi tayari yuko Ice cream..eeee samahani ICU amekwenda kumwangalia mgonjwa, nyinyi huku mnasambaza picha zangu. Nailaumu serikali ya mtaa wangu kwa sababu kiongozi wetu hatutetei sie wanyonge tunaoanikwa mambo yetu kwenye mitandao. Nimejaribu kuwasiliana na Rihanna atoe tamko bahati mbaya simu yake haipatikani inawezekana ni mtandao maana alinambia anaenda Iringa kujaribu kuingia ubia na wajasiria mali wanaouza ulanzi, akirudi wote walioshiriki kwa namna yoyote ile katika hili  tutawafikisha pabaya.

1 comment:

Anonymous said...

lol