HATUPIMI BANDO

19 June 2014

MASHABIKI WA SPAIN WAONDOKA BRAZIL KUPITIA NJIA ZA PANYA

Blog yenu makini ambayo ilikaa siti moja na MKUDE SIMBA kule Brazili kuangalia mechi kati za Chile na Spain, iliweza kuona kipigo cha mbwa mwizi kilichowafadhaisha wapenzi wa timu ya Spain. Kutokana na tabia ya manazi wa timu siku hizi kujipaka mpaka rangi za timu, ilikuwa kazi kwa wengine kujificha wakati wenzao wengine walivua tu jezi na kujidai hawashabikii timu yoyote. Mzee wa Blog eti ghafla akajidai yeye ni Mzee wa timu ya Lipuli hivyo hahusiki na kipigo cha Spain. Kwa kuwatumia rafiki zake Mkude ambao ni wapiga picha maarufu, tuliweza kuwafuatilia wapenzi wa Spain ambao walikuwa wameamua kutembea kwa mguu toka Brazil hadi makwao huku wakificha sura zao kwa aibu na kukwepa kupanda ndege.
Picha hiyo hapo chini ni siri sana, blog hii inaweza kulipuliwa na El Shabab ambao ni wapenzi wa Spain


No comments: