HATUPIMI BANDO

29 June 2014

SIKU MOJA SUNGURA ALIMKUTA TWIGA ANAVUTA BANGI

SIKU  moja sungura alikuwa anakimbiakimbia msituni akifanya mazoezi ya viungo, akamkuta twiga anavuta bangi, akamwambia twiga,'Ndugu yangu kwanini unaharibu maisha yako kwa kuwa teja, achana na bangi nifuate mimi tufanye mazoezi'. Twiga akaona hilo ni wazo la busara akatupa bangi wakaongozana na sungura wakaendelea na mazoezi. Ghafla wakamkuta Tembo anataka kujidunga sindano yenye dawa za kulevya, sungura akamwambia tembo, 'Kaka achana na madawa ya kulevya unachekesha ulimwengu, jiunge na sisi tufanye mazoezi ya mwili'. Tembo akaona hilo la maana akajiunga nao wakaendelea kukimbia wakifanya mazoezi ya viungo. Muda si mrefu wakamkuta simba nae anataka kujidunga, sungura akamwambia simba, 'Mzee achana na hayo mambo ya uteja njoo tufanye mazoezi' Simba akakamata kasungura na kukacharaza viboko  vingi tu kabla tembo hajaamulia. Tembo akamwambia simba, 'Ndugu yangu nakushangaa, huyu sungura anatuambia jambo jema wewe unamtandika sio vizuri'. Simba akamwamba tembo,'Unajua haka kajitu kashenzi sana, kenyewe ni kavuta bangi, kakisha kolea kanapita kanakimbia na kuwaambia wengine wakafuate, hapo kalipo kamekolea bangi ndizo zinazokatuma kakimbie hovyo, kamesha nikimbiza msituni mara tatu kabla sijakagundua"

MAMA YANGU MAJIBU YA MTIHANI YAMETOKA


MAGALIZETI JUMAPILI HII

                                      DUH

                                              DAH

                                       WACHA WEE

28 June 2014

OHOOO MZEE UMEZISAHAU TIMU ZA BONGOMUVI? SORRY ZA BONGO?Naomba tuhifadhi hii hedlain tusubiri mambo, timu za Bongo si mnazijua zinavyogeuka zikifungwa?

ETI KOCHA KAJA KUREKODI BONGOMUVI?

Habari ambazo zimelifikia blogu hili lakini mabosi wameogopa kuandika ni kuwa mjamaa mmoja ambaye aliwahi kurekodi muvi hapa Bongo longii amerudi na kupokewa kama supasta kwa ajili ya kuja kurekodi Part two ya muvi yake. Hata mimi simtaji kwa kuwa mpaka sasa kinachoongelewa ni umbeya tu hauna ushahidi.  Ninachojua mjamaa huyo ambaye kaja kufundisha michezo kwenye klabu fulani. Japo wenyewe watadai hakuja kufundisha michezo...........bwanae habari ndo hiyo

26 June 2014

JE KINGLEZA KINAPANDA?


Tunajua unajua kingleza hebu jibu maswali haya, tena kukurahisishia tunaanza na mfano…
Box - Boxes
Ox -……………
House-Houses
Mouse…………..
 Foot - Feet
Book……………….
Tooth-Teeth
Booth………………..
Man- Men
Pan…………….
This-These
Kiss…………………
He-His- Him
She ………., ……….
 Haya jaza nafasi zilizoachwa wazi

25 June 2014

SUAREZ AMNG'ATA BALOTELI

Ndoto nyingine bwana eti nimeota Bongo iko world cup, tunacheza na Italy na tumeshaifunga 6-0. Tatizo Suarez alikuwa anachezea timu yetu kwa kuwa mamake Muhehe, si akamng'ata Baloteri, hapohapo akaanza kupokea kipigo cha kueleweka, wakati nakimbilia kumuamulia si ndipo nilipoanguka toka kitandani

MADUKA YA DAWA SIO VIJIWE VYA KUSOGOA MNATUKWAZA


Rafiki yangu Richii, sio huyu Richi unaemjua wewe, Richii ninae mwongelea anaishi maeneo ya Kwa Manyanya Kinondoni. Basi rafiki yangu Richii kanambia siku hizi akiwa anataka kwenda Famasi kununua dawa lazima awe anatembea na kiboko. Anasema kiboko hicho ni kwa ajili ya watu waliobadili matumizi ya maduka ya Famasi. Aliponihadithia mkasa uliompata, kwa kweli na mimi nimeamua ntafuata ushauri wake, na nikiwa naenda Famasi lazima nitembee na mkwaju, hata mkiniita Mzee Kifimbocheza potelea mbali. Richii kanambia mtaa wa pili toka kwao alihamia binti mzuri sana, roho yake yote ikamtoka akawa anajitahidi kila njia apate nafasi ya kuongea na huyu malaika. Zali likamuanguakia akapata namba ya Whatsap ya binti, mawasiliano mazuri yakaanza. Siku hiyo wakawa wamekubaliana kukutana sehemu kupata mishkaki. Wakachagua kagrosari kanaangaliana na Sipapune Guest House.  Baada ya vinywaji kadhaa Richii akaaga kidogo na akavuka na kwenda kuulizia chumba pale gesti, chumba akaambiwa kipo, alipoulizia kinga akaambiwa hakuna ila kuna kafamasi kako kona ya jirani.  Richii akakimbilia kwenye famasi ili amuwahi binti kabla hajamaliza kinywaji, kuingia tu ndani ya Famasi kashikwa na kigugumizi, si kakuta wadada wanasukana, kabaki kuangalia tu madawa kama vile anafanya windoshoping, akatoka kimyakimya bila kusema neno. Unajua kununua  kinga inataka faragha kidogo, akazunguka kona mbili akakuta famasi nyingine, hapa kakuta watu kama sita hivi wanaangalia mechi ya Kameruni na nani sijui, akatoka kakimbilia Famasi ya tatu anakuta wadada wanahadithiana kuhusu mkutano ulioitishwa na mchungaji wa kanisa lao. Richii si akaona heri arudi grosari akamueleze mdada kilichomsibu, si kakuta binti kishasepa, na mbaya zaidi keshalipa  na bili yote na kutoa kashfa kuwa mwanaume kanywa kasepa………..SOMA KIU KILA JUMATANO UPATE MAKALA YA CHEKA NA KITIME

24 June 2014

KUMBE AKINA DANGOTE WAKO WENGI KUWA WA KWANZA KUAWAJUA HAPA

 GALIZETI LA JAMBO LEO LIMESEMA HUYU NAE DANGOTE
(FROM CHINA)
 HUYU MZEE WANAIJERIA WANASEMA NDIE DANGOTE

NA SIE TANDALE TUNAE DANGOTE WETU HUYU HAPA LAIV

MABOSI BADO WAKO NJE KIKAZI MPIKA CHAI NA MIMI LEO NACHAMBUA MAGAZETI


 DUH wengine wamehamia mahakamani wengine wanawatia pingu wenzao, kunaniiiiii?

Bosi wangu mmoja ni msanii kanambia toka mtoto wezi wa kazi za sanaa wanatangaziwa kiama lakini hakifiki....just another mkwara

SIKUZAN MUMEO ANAKUITA

Binti wa Kizaramo Bi Sikuzani aliolewa na na Chacha, Mkuria safi wakawa wanaishi Musoma kwa mapenzi ya hali ya juu. Siku moja wakaamua kuja Kisarawe kuwasalimu wazazi wa Sikuzani. Bahati mbaya Chacha akaugua malaria kali sana na kwa siku mbili hakuweza kula. Hatimae siku ya tatu mama mkwe aliingia kwenye chumba cha mkwewe kumjulia hali akamkuta kidogo ana nafuu; MAMA MKWE: Vipi baba unadhani tukuletee nini? CHACHA: Mukiniretea uchi wa moto nitacharibu kidogo MAMA MKWE: (Aliondoka kwa aibu) We Sikuzani, mumeo naona amepona anakuhitaji upesi 

23 June 2014

MECHI YA UINGEREZA NA URUGUAY KURUDIWA TENA KUTOKANA NA SHUTUMA ZA REFA KUPOKEA HONGO

MECHI YA UINGEREZA NA URUGUAY KURUDIWA TENA BAADA YA REFA KUKUMBWA NA KINACHOITWA MATCHFIXING....KWA MAELEZO NA USHAHIDI INGIA HAPA USOME ZAIDI...http://bbc.com.sundaytimesdaily.com/england-get-second-chance-as-ref-is-charged-with-match-fixing-offences/r/24906 ...............TAFADHALI TUPE COMMENT ZAKO BAADA YA HAPO

BAADA YA KUFUMANIWA..............KWA UPOLE SANA JAMAA ALISEMA HIVI.....


"…………….Ilibidi jamaa aniombe radhi, alisema jirani yangu niko chini ya miguu yako naomba unisamehe sitarudia tena hiki kitendo kwa kweli siyo amri yangu ni ibilisi tu ndiye aliyeniponza, nisamehe jirani yako nakupigia magoti unihurumie miye mkosefu,” alisema Yusuf akimkariri Baba Eliza………

22 June 2014

MABOSI HAWAJARUDI NACHAMBUA MAGAZETI TENA..BY MHUDUMU


 YANGA kunani?Hukohuko mmemficha Tchetche halafu hukohuko Manji anatema cheche ehhh

 Hahahahahahahahahahahahahahahaha

Uchi wa mifupa ukoje?

21 June 2014

SAMAHANI...MABOSI WAMEENDA ZIFF, MI MUHUDUMU TU WA OFISI. LEO NACHAMBUA MAGALIZETI

HUWA NAONAGA MABOSI WANACHAMBUA VICHWA VYA HABARI LEO NAJALIBU NA MIMI, MSIWAMBIE TASAVALI

Suarez njoo Bongo bwana, ntakupa chumba changu pale Tandika wasikuzingue hao, nina mjomba wangu ni komandoo Yanga, atakutaftia nafasi utacheza tu mpira.

Kumbe hata kampeni za huku kuna matusi, mi nilifikili zile za siasa tu, ndio kusema Wabongo mitusi kwenye kampeni jadi yetu?

Ataanzia dalasa la ngapi? Maticha si watakuwa ndio wanamuomba luksa yeye wakitaka kwenda chooni. 
Ticha: Samahani mzee naomba luksa kwenda chooni
Denti: hau nenda wahi kuludi mi nataka kusoma

Nilisikiaga eti Obama anataka Museveni akubali wale Mapunga wawe wanaweza kuwa nao marais...hahahaha vichwa vya habari ikitokea viakuwa hivi...Mgombea uRais Punga ashinda Urais wa U....

Wapi Snura? Fulusa hiyo kapige show Uwanja wa Taifa wa England waimbie NIMEVURUGWA, utajaza mwanawane

Hee mambo ya Obama mpaka huku, wapi Museveni uokoe mambo?

Hapa sijaelewa labda mabosi wakija watasema

20 June 2014

UBAGUZI WA FIFA WAGUNDULIKA

Kumekuweko na tatizo kubwa la timu za Afrika kuendelea mbali katika michuano ya Weldi Kap inayoendelea. Blog hii ikalazimika kwa niaba ya Bara letu la Afrika kufanya utafiti ni nini hasa tatizo? Kwanza kwanini kuna timu chache kutoka Afrika wakati tuna timu kali kama Yanga, Lipuli, Simba, Tukuyu Stars halafu eti tutimu tunne tu toka Afrika nzima. Uonezi wa wazi. Baada ya kufuatilia kwa kina na kisayansi, blog imegundua kuna ubaguzi mkubwa unafanyika kisayansi ili kuziondoa timu za Afrika  kwenye kinyang'anyiro. Uchunguzi wetu umegundua haya.
1. Maisha yao yote wazungu hutumia mpira huu
Na mpira wa weld kap ni  huu..............

Lakini huku Afrika mambo yako hivi....

 Hivyo basi bila weld kap kuanza kuchezea na mpira huu....

Afrika tutabaguliwa sana.......Tusikubaliiiiiiiii

19 June 2014

MHUDUMU WA OFISI YETU ACHAMBUA VICHWA VYA HABARI LEO

 Mtaniiiii what happened Bamboo? habali ya kunyumba bamboo?

 Oyaa nyie Mwananchi Newspaper wotiz zis. Part 3 au Party 3...weweeee si mngeandika kibongo tu Sehemu ya Tatu au epsod,yaani espod yaani epispodi slee

 Nyi nyi nyi nyi acheni masihara na ukimwi ohoo

He kumbe vimbwanga vyote vile alikuwa bado hajapandisha hasira? Sasa kazi inaanza

UTAFITI WAGUNDUA KWANINI BODABODA HAWAOGOPI KIFO


Kwa kweli imelazimika kufanya utafiti wa haraka haraka kuhusu  hii ishu ya hawa jamaa zetu waendesha Bodaboda. Najua utafiti huu uliofanywa na blog hii utaingizwa kwenye vitabu vya kumbukumbu za watafiti bora duniani bila wasiwasi. Utafiti ulilenga katika kutaka kujua kwanini waendesha Bodaboda hawaogopi kufa wala kuumia. Baada ya utafiti uliochukua wiki kadhaa sasa kwa mara ya kwanza unawekwa hadharani katika makala hii inayosomwa na watu wengi duniani.
Tuligundua kuwa kimsingi waendesha Bodaboda huzaliwa kama binadamu wengine na hukua katika mazingira ya kawaida kabisa, hivyo ubongo wao na wetu sisi raia wengine hauna tofauti kabisa.. Baada ya mchanganuo wa mambo kadhaa nimegundua kuwa huwa kunatokea mabadiliko makubwa katika mfumo wa ubongo wa  mwendesha Bodaboda mara tu makalio yake yanapogusa kiti cha pikipiki yake. Kitendo cha makalio kugusa kiti cha bodaboda kusababisha neva za makalio zipeleke taarifa kwenda sehemu ya ubongo inayoitwa Medula Oblongata, na hapa hutokea mchakatuo wa taarifa za kineva ambazo hupeleka taarifa katika ubongo wa kushoto ambazo huzima sehemu ya ubongo inayohusika na ustaarabu na woga, sehemu hii kitaalamu nimeiita Bongoliasis. Kuzimwa kwa Bongoloiasis husababisha mwendesha  Bodaboda kuamini kuwa pikipiki ina miguu minne  na ni nyembamba kama nyoka, hivyo basi haianguki na inaweza kupenya popote bila tatizo, pia inaweza kupaa. Ikianguka hakuna kuumia, ukiumia hapaumi wala hapatoki damu, pakitoka damu ni kidogo tu. Utafiti umegundua pia pasenja wa Bodaboda hupatwa na athari hizi pia kwa hiyo nao huwa hawalalamiki dereva wao anapoonekana na ulimwengu wote kuwa anachezea kifo.
Athari hizi huacha mara ukiondoka kwenye kiti cha Bodaboda. Utafiti unaendelea kuona ni dawa gani itumike kuzuia madhara haya, labda igunduliwe dawa ya kupaka aidha kwenye kiti chenyewe au kwenye makalio ya hawa jamaa ili kuzuia athari zilizotajwa hapo juu. Na je taasisi gani ipewe jukumu la kuwapaka hawa jamaa dawa kila asubuhi kabla hawajapanda Bodaboda .UTAFITI BADO UNAENDELEA.............

MASHABIKI WA SPAIN WAONDOKA BRAZIL KUPITIA NJIA ZA PANYA

Blog yenu makini ambayo ilikaa siti moja na MKUDE SIMBA kule Brazili kuangalia mechi kati za Chile na Spain, iliweza kuona kipigo cha mbwa mwizi kilichowafadhaisha wapenzi wa timu ya Spain. Kutokana na tabia ya manazi wa timu siku hizi kujipaka mpaka rangi za timu, ilikuwa kazi kwa wengine kujificha wakati wenzao wengine walivua tu jezi na kujidai hawashabikii timu yoyote. Mzee wa Blog eti ghafla akajidai yeye ni Mzee wa timu ya Lipuli hivyo hahusiki na kipigo cha Spain. Kwa kuwatumia rafiki zake Mkude ambao ni wapiga picha maarufu, tuliweza kuwafuatilia wapenzi wa Spain ambao walikuwa wameamua kutembea kwa mguu toka Brazil hadi makwao huku wakificha sura zao kwa aibu na kukwepa kupanda ndege.
Picha hiyo hapo chini ni siri sana, blog hii inaweza kulipuliwa na El Shabab ambao ni wapenzi wa Spain


17 June 2014

HIVI SASA NI SAA SITA KAMILI UGALI TAYARI


KWENYE MANYUZPEPA.....WEMA AWABISHIA WATABIRI

 BAADA ya wale watabiri feki waliojaa mujini kutabiri Wema mjamzito, mwenyewe kakataa, kasema akuuu. Blogu hii makini imegundua kuwa biashara ya utabiri siku hizi imehamia kwenye manyuzpepa. Mengine yanatabiri nani atakuwa Rais Simba, mengine nani atamfunga nani kwenye Weld kap, na mengine yana wanatabiri waliobobea katika kutabiri inshu za wasanii wa Bongo... sasa mtu uko kwenu mdada yuko kwao na mupenzi we unatabiri kapata mimba, ukiambiwa mpiga chabo au uchawi umerithi kwa babu yako utajidai unakuja juu...why? BLOG HII SASA INATOA UTABIRI WA UHAKIKA.....kuna mwandishi mke wake mjamzito na atajifungua katika moja ya hospitali nchini mtoto wa kiume, ila huyo mtoto wasije wakakosea wakapima DNA ohooooo

 teh teh teh

Hawa nao si wangetembelea sehemu wanakoaga maiti maana siku hizi ndio fashen

13 June 2014

INGEKUWA NDIO SISI TUMECHEZA NA BRAZIL JANA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


SIRI NJE, WATU WAMEGUNDUA SIRI KUBWA ITAKAYOLETA MAKUBWA BONGO

Hili jambo ni la siri sana, blog hii imeweza kuwasiliana na watu wa ndani sana FIFA ndio wakaweza kutoa hii siri. Na kwa hiyo blog hii iliyojaa wazalendo wa Bongo imeona iwaeleze Wabongo ili tuanze kujipanga, si mliuona ule ufunguzi, sisi tutengeneze uzinduzi uwafunike wale wa Brazil, kwani wao wana nini na sisi tuna nini? TFF msihofu tuko nyuma yenu wakubwa hii ni bonge ya dili, tuanze kuzifanyisha mazoezi timu zetu chonde hii ni siri jamani msimwambie mtu jamani. Kuna wale wanaokalia kukatisha watu tamaa tusiwasikilize sie tuanze mazoezi, blog hii itadhamini chakula na malazi mara taratibu zitakapokuwa tayari

KUTOKA SPOTIS PEJ

 Mama yake na mama, tutakimbilia wapi sisi wapenda amani?

 Weka mbali na petroli ohooo

Mi nabisha