HATUPIMI BANDO

10 May 2014

NANI ANATAKA KUOKOKA?

MCHUNGAJI alikuwa anawaombea waumini wake akauliza;
MCHUNGAJI: Wangapi wanataka kuokoka inueni mikono niwaombee.....hakuna aliyeinua mkono. Pedeshe mmoja akapita mbele na kupanda madhabauni na kutangaza
PEDESHE: Jamani mchungaji anasema wanaotaka kuokoka wanyanyue mikono juu jamani.....mtoto mmoja peke yake akanyanyua mkono, pedeshe akatoa laki tatu mfukoni akampa yule mtoto.
PEDESHE: Haya jamani ninaomba nirudie tena niwaombe wanaotaka kuokoka wanyooshe mikono juu ili Mchungaji atuombee.....watu wote wakanyanyua mikono juu, Pedeshs akamgeukia Mchungaji ili awaombee akakuta na mchungaji nae kanyanyua mkono juu.

No comments: