MZEE MHARIRI NAOMBA MSAADA

Kwa Mhariri,
Cheka na Kitime Blog
Bongolendi
Manzese Mjini.

 Mzee Shkamoo
 Mzee mimi naitwa Jaklin, tunakaa Boko, zamani tulikuwa tunakaa Magomeni sasa baba alipopata hela za kustaafu akajenga huku Boko ndio tumehamia. Nimemamliza fom six niko nyumbani nangoja majibu. Kuna kitu naomba mnisaidie.
Tarehe 1 April nilimwambia baba yangu kuwa nimechaguliwa kujiunga na chuo kikuu cha Oxford Uingereza. Baba alifurahi sana akaagiza kuku wawili wachinjwe na mama apike pilau. Baada ya hapo kila siku amekuwa akirudi nyumbani kalewa anaimba kuwa mwanae ninaenda Uingereza. Juzi nimegundua kauza kipande cha ardhi jirani na kwetu ili aanze kukusanya fedha za mimi kuishi Uingereza. Pia nasikia ameshakopa hela Saccoss ili ajumlishe kwenye nauli yangu ya kuendea Ulaya. Pia alitoa shilingi laki tatu kanisani kama sadaka ya shukrani kwa mimi kuchaguliwa kwenda Uingereza. Mzee naomba unisaidie ntawezaje kumwambia baba kuwa siku ile nilikuwa namtania ilikuwa sikukuu ya wajinga?
Naomba msaada haraka au nitoroke kwetu?

Jaklin

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.