HATUPIMI BANDO

13 May 2014

MA DOMOZEGE WANAHARIBU MAMBOKatika jamii ya binadamu wa Bongo kuna hawa wanaoitwa ‘DOMO ZEGE’.  Kutokana na ubaguzi wa hali ya juu wa kijinsia  jina hili linahusu wanaume tu. Wamama wenye tatizo hili husifiwa  kuwa na staha na ni watulivu!!!!!!!!. DOMOZEGE ni mkaka ambae anaweza kumuona mdada anaempenda lakini kila akikutana nae mdomo unakuwa mzito  kujieleza ishu yake, kinyume cha jina lenyewe DOMOZEGE si kwamba hawawezi kuongea, aa wapi wanawezakuwa waongeaji saaaana wakiwa na wenzao wa jinsia yao, tena wana stori nyingi sana kuhusu uwezo wao kunako nanihii, lakini ikifikia kueleza hisia zao kwa mdada wanaempenda akili ina siz. Si mara moja domo zege hunyang’anywa tonge mdomoni. Cha ajabu wakishanyang’anywa eti ndio wanaanza kufunguka,’Ohh unajua anti mi nilikuwa na mipango mingi sana na wewe sasa naona bradha kaniwahi’, na mara nyingi hujibiwa,’Jamani kwa nini hukusema?” Kutokana na tatizo hili kuwa kubwa, maana kipimo cha ukubwa kinakuja kutokana MADOMOZEGE siku hizi wamechukua staili ambayo inaleta fujo kwenye fani, wameanza kumwaga zawadi za bei mbaya. Utakuta DOMOZEGE anatoa iPhone5 mtaa huu, mtaa mwingine SAMSUNG S6, kule chini anamwaga minoti mingi tu,  eti ndio iongee kwa niaba yake, au siku hizi kuna staili ya kununulia watu Verosa maana katikati hapo walikuwa wanahonga viVITZ sasa vimekuwa vingi mno, sasa huu ni ukorofi katika fani, watu wenye uwezo wa kuongea wamekuwa hawana thamani. Eti hapa mkwanja tu stori peleka kwa Shigongo. Watu wenye hasira wameanziasha shule maalumu kwa ajili ya MADOMOZEGE. Shule hizi  zinaanzishwa ili kuwa saidia wenzetu hawa, na kutokana na maendeleo kutakuwa pia na masomo kwa ajili ya akina mama ambao wanaona nao UDOMOZEGE unawakwaza, mitaala inapangwa na siku za karibuni tutawataarifu wahusika wakutane wapi…. UMEONAEE

No comments: