PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

ENZI ZA BABU YAKE MWENYE BLOGU HII...............DENGU ILIKUWA......

- Enzi za babu yake mwenye blog hii, DENGU na ilitumika kutengeneza bagia. Na watu walijisifu kuwa na DENGU nyingi, hata wengine kuomba kupewa dengu. Pia ilijulikana Wahindi ndio mabingwa wa mapishi ya dengu….LEO HII MHHHH
- Enzi za babu yake mwenye blog hii, mtu msagaji alikuwa ni yule mtu aneyependa kudharau na kubeza vitu, akasifiwa kuwa anasaga sana. Na watu walijisifu kuwa wao wasagaji wakubwa. Pia ilijulikana kuwa watu husaga mahindi ili yawe unga na kulikuwa na shirika kubwa la umma likijulikana kama National Milling Corporation lililohusika na usagaji…..LEO HII MHHHHHH
- Enzi za babu yake mwenye blog hii, unga ulikuwa chakula bora, ambacho kilitumiwa na kila nyumba hapa nchini. Na watu walijisifu kwa kuwa na unga mwingi, na hata kuwa na unga wa aina mbalimbali, muhogo, mahindi, ngano na mtama. Pia unga ulikuwa ukiuzwa kwa bei ndogo kwa kupima kwenye mizani hadharani…..LEO HII MHHHH
-Enzi za babu yake mwenye blog hii, wacheza mpira walikuwa wakisifika sana pale wanapo piga mabao timu pinzani. Na watu walijisifu hadharani kwa kuweza kupiga mabao mengi kila kunapokuwa na mechi. Pia kupiga bao ilihusika na kwenda kuagua kwa waganga na kupewa utabiri…..LEO HII MMMHHHHH
JE NI SABABU YA UDIJITALI?
-

Comments