HATUPIMI BANDO

30 April 2014

TUMA VOCHA UFANIKIWE

Kuna kitu cha ajabu ambacho kwa kweli hata mimi sikielewi, ila tu naweza kusema miujiza inatokea. Binti mmoja alikosea akanitumia vocha ya shilingi 500, usiku ule kaka yake aliyoko Jahannesburg amemtumia shilingi alfu hamsini. Msanii mmoja maarufu wa kike, amenitumia vocha ya shilingi alfu mbili, nusu saa baadae amepata pedeshee ambaye licha ya kutangaza kumuoa tayari amemkabidhi BMW mpya. Rafiki yangu wa huko Iringa amenitumia vocha ya shilingi alfu tano, biashara yake ya ulanzi imekuwa ghafla katika mwezi mmoja tu amekuwa wakala wa bia. Ni jambo la ajabu lakini liko wazi kuwa muujiza unakufuatia mara tu ukinitumia vocha. Nimeona niweke wazi hili jambo ili watu wengi zaidi muweze kutumia nafasi hii kupata muujiza wenu. Haya haya haya wahini kunitumia vocha maana huwezi kujua lini bahati hii itakata. 

GESTI ZA USWAZI NOMA

Gesti za uswahilini nomaaaaa;
MTEJA: Mhudumu sina taulo chumbani kwangu
MUHUDUMU: Samahani mzee subiri kuna mtu analitumia

KUMBE SINA KISUKARI


Mzee kaingia pharmacy,
MZEE: Mambo mwanangu, kuna kitu naomba uonje nitakulipa
MFAMASIA: Kitu gani?....Mzee akatoa kichupa na kijiko akaweka majimaji yaliyomo kwenye kichupa kwenye kijiko na kumwambia mfamasia aonje, mfamasia akatia yale maji mdomoni na kuyazungusha zungusha mdomoni akionja;
MZEE: Nipe jibu, ina utamu wa sukari au chumvi au pilipili?
MFAMASIA: Kama chumvichumvi
MZEE: Hakuna sukari
MFAMASIA: Sukari hakuna kabisa
MZEE: Loh asante chukua hii alfu tano nashukuru sana, dokta alinambia nipime mkojo wangu kama nina kisukari, kumbe sina asante bwana mdogo

USIDANGANYIKE NA JINA REFU LA CHEOCHAKO OHOO

Kadri cheo chako kinavyokuwa na jina refu ndivyo kinavyokuwa kidogo zaidi. Katibu Mkuu ni Mkubwa kuliko Naibu Katibu Mkuu, na Katibu Mukhtasi wa Naibu katibu Mkuu nae mdogo zaidi. Afisa usafi wa ofisi ya katibu Mkuhktasi wa Naibu Katibu Mkuu ndio yuko chini zaidi..........

28 April 2014

IGENI TU HAINA MAJOTROO


TUNACHAMBUA VICHWA VYA HABARI VYA REO REO HAPA

 We Morinyo kisa cha kutia nazi supu ya watu?

 Tumeshindwa kuchambua maana hapa Bongo, umeme waweza kuwa HIV au pombe maarufu yenye majina lukuki kama ngumu kumeza, kachaso, uzo na kadhalika, au inaweza kuwa ni huu wa Richmond, kwa hiyo tunafanya utafiti tujue nini kinaongelewa.

 okay

 Kwa tafsiri ya wakubwa wa Blog eti hawa suspended trio watapigwa risasi

Hapa mkuu wa dini tunadhani anamananisha kuwa Muungano utavunjika kutokana na ukame wa mapenzi...nani anabisha?

26 April 2014

MTIZAMO WA BLOG HII KUHUSU IDADI YA SERIKALI

Baada ya kutafiti kwa makini sana mazungumzo yanayoendelea nchini, hasa kuhusu hili ambalo linawatesa wanasiasa, swala la idadi ya serikali, blog yenu makini imefanya utafiti wa makini kwa kufuata ule usemi wa wahenga wa Ulaya unaosema 'No research, no right to speak'. Blog hii makini kwanza ilitafuta mamilioni ya fedha toka kwa wafadhili wa ndani na wa nje, ili kuwezeshwa kufanya utafiti huu ambao matokeo yake yataushtua ulimwengu wa huu wa Bongo. Watafiti wa blog walizunguka nchi nzima na kuhoji mamilioni ya watu wakiwemo wanaume, wanawake, na hawa jamaa ambao hawajulikani kama wako upande gani, pia ilihoji hata watoto wachanga. Matokeo ni kuwa asilimia 99 ya watoto wachanga waligoma kabisa kujibu, wakaonyesha dharau kwa watafiti wetu, na asilimia moja wakiamua kulia au kucheka kwa kila swali la watafiti. Tunaishauri serikali iwachukulie hatua kali watoto hawa kwani wameharibu kabisa utafiti na hivyo kuleta majibu yasiyokubalika katika utafiti. Kwa kweli blog ilipita hospitali kadhaa na kuhoji hata wale wenye matatizo ya uchizi. Hawa walisaidia sana blog hii kuwaletea majibu yetu kuhusu tafiti hii. Kimsingi tunapingana na tafiti zote za kisomi kuhusu idadi ya serikali katika nchi hii. Kwanza kuna makosa makubwa kuhusu idadi ya serikali zilizopo, bila kupepesa macho imekuwa ikisisitizwa kuwa kuna serikali mbili, utafiti rahisi uliofanyika pale Mirembe uligundua hakuna ukweli wowote wa jambo hili. Watoto kadhaa pia waliweza kututaarifu kuwa hata mtaani kwao kuna serikali. Hivyo basi ukikusanya serikali za mitaa zote, ukijumlisha na mbili zinazotajwa sana tayari una maelfu ya serikali nchi hii. Kwa msingi huu blog hii inaomba kutengeneza upya rasimu ya katiba ya Bongo. Asante. Utafiti huu utawekwa wazi karibuni

25 April 2014

MPOKI ATUA UJERUMANI NA KUANZA KUONGEA KIJERUMANI CHA NDANI SANA

Katika hali ya kushangaza msanii maarufu Mpoki ametua Ujerumani na akashangaza mamia ya Wajerumani kwa kuanza kuongea Kijerumani cha ndani kabisa chumbani, hali iliyowafanya Wajerumani wa kawaida wamshangae maana alikuwa anaongea kikwao mpaka haelelweki. Mpoki ambaye atakutana na WaBongo walioko huko, alionekana akiwa uwanja wa ndege wenye jina gumu la Kijerumani akiongea Kijerumani na binti mdogo wa Kijerumani. Mpoki aliweza kujichanganya mjini wala hakutambulika kutokana na kuwa mweupe kuliko Wajerumani wenyewe habari zaidi baadae

22 April 2014

HATIMAE BONGO YAGUNDUA KITU KIPYA KINGINE WIZI FEKI

Baada ya kupata uzoefu wa muda mrefu wa kutumia vitu feki toka Uchina, sasa Bongo nayo imekuja na ubunifu wake ambao unaweza ukawafanya Bongo Movie wakose kazi. Bongo wameweza kufanya wizi feki benki. Eti wameingia benki waka ekti kama wezi na kutoka na bulungutu la hela kumbe bulungutu feki, hakuna kilichoibiwa wala ni nini...............

KUMBE BADO UNANIPENDA

Jamaa na mkewe walikuwa ghorofani wanagombana;
MKE: Mi najirusha nife nimechoka na mambo yako........mke akiwa akakimbilia kujirusha dirishani, mume akamdaka na kumzuia
MKE: Hee maneno mengi kumbe unanipenda hutaki nife?
MUME: Aaaa wapi kulikuwa na gari limebeba masponji linapita chini, nilikuzuia lipite kwanza haya ruka

21 April 2014

NI BONGO TU DUNIA NZIMA HAWAWEZI

Unajua Bongo tuna utalaamu wa kutengeneza kitu kabla siku yenyewe haijafika. Utaalamu huu ni nadra sana uko Bongo peke yake. Wamarikani wakijua tumekwisha watataka kutunyanganya. Blog hii inaomba utaalamu huu ulindwe na Katiba mpya hii ya wanasiasa. Kama hapa unaona japo huu ni mwezi April tayari tumetengeneza vitu mwezi May Teh teh teh teh

20 April 2014

ZAWADI MURUA KWA AKINA MAMA MSIMU HUU WA PASAKA

Kwa akina mama ambao wanaume zao wanapenda michepuko, sasa kuna zawadi nzuri msimu huu wa Pasaka. Unachotakiwa kufanya ni kumsubiri kalewa na kuweka ile nani hii yake kwenye hiyo sehemu iliyowekwa soseji kisha kufunga kifuniko. Matokeao yake ni hayo hapo kwenye sahani. Kabla hujatumia inafaa umtaarifu kuwa umeshanunua kifaa hicho cha kupunguza michepuko. Wanaohitaji wanitaarifu hapo sehemu ya kukoment ili kuwaletea. Kina kuja kwa saiz tofauti wahi sasa.Zawadi hii pia hufaa kutolewa siku za harusi au kumbukumbu za ndoa.

SAGULA SAGULA YA VICHWA VYA HABARIHIVI VICHWA VYA HABARI VIWILI NANI MKWELI?

16 April 2014

WAMEKULA NYAMA YA MTU


MSAIDIENI HUYU MAMA

Kwa kweli wahariri wa blog wamelazimika kuomba msaada kuhusu hili jambo, na tunaomba wananchi mchukue muda kuacha kuangaliia TV Matusi na kujibu hili swali ambalo blog imeulizwa.
Tumepokea barua hii;

                                                                                                           Mwananyamala     
Hospito
                                                                                                           Daslmu

Mhariri,
Chekanakitime
Daslam
Manzese Darajani


Ndugu Mhariri,
 Mimi nimejifungua mtoto juzi, eti cha kushangaza ni kuwa mtoto kafanana kila kitu na baba yake. Mbona hajafanana na mimi? Inaonyesha mume wangu alikuwa anatembea na mwanamke mwingine ndio maana mi nimemzaa huyu mtoto anaefanana nae. Naomba jambo hili liwekwe kwenye Katiba wanaume wasiwe na wanawake zaidi ya mmoja. Naomba msaada wako ulifikishe hili kwa wabunge wanaotetea haki za wanawake
  Maliam

CHEZEA MAPASTA WEWE


BILA KULEWA HILI BUNGE LITAKULEWESHA


Kiukweli hili Bunge la nanihii bila kulinywea pombe utalewa bila kunywa. Watu wanaongea kwa sauti mbili, ubishi usioisha, na haraka sana watu kukimbilia kusema wanachoongea tumewatuma, tulikutana wapi? So ekchwali nakunywa hapa nikitoka hapa nakuja huko huko mnieleze hivi ndicho mnachodhani sisi tunakitaka?

WANAMUZIKI WANAVYOMKUMBUKA MAREHEMU MUHIDIN GURUMO


12 April 2014

UNAMJUA HASANI MAKOLOKOCHO WEWE?

Jamaa alianza kujisifu sana kazini kwake;
Jemsi: Wiki ijayo nafanya mtihani, ni miezi sita sasa nafanya masomo ya jioni, nimejua mengi sana, we unamjua David Livingstone?
Devi: Hapana simjui
Jemsi: Huyo ndie mzungu wa kwanza kuliona Ziwa Victoria, ungekuwa unasoma masomo ya jioni ungemjua huyu.
Jemsi akawa kero kazini kwa maswali yake.
Jemsi: We unamjua Graham Bell?
Devi: Hapana simjui
Jemsi: Huyo ndie alikuwa mtu wa kwanza kutengeneza simu, ungekuwa unaenda kuchukua masomo ya jioni ungemjua.
Siku moja Devi akamwita Jemsi;
Devi: Jemsi unamjua Hasani Makolokocho?
Jemsi: Hapana
Devi: Huyo ndie mchepuko wa mkeo kwa miezi sita sasa, ungekuwa huendi kuchukua masomo ya jioni ungemjua

BABY NINA MIMBA YAKO

MDADA: Baby nina mimba yako
MKAKA: Hee  inatafuta nini kwako? nipe upesi au usinisumbue tena

BABY NAKUJA KUMFUNZA ADHABU


Wamama wawili walijikuta magari yao yamegongana. Wakashuka kwenye gari wakaanza kutoleana kashfa, hasa yule aliyekuwa na vogue akamtukana sana mwenye Kivitz, japokuwa ndie aliyekuwa na makosa. Mwenye Kivitz akampigia mumewe simu.
MAMAKIVITZ: Mume wangu ninatatizo
MUME: Jamani niko bizy mkutanoni hebu lisov mwenyewe
MWENYE VOGUE akasema anampigia boy friend wake ndiye atakae ongea.
MWENYE VOGUE:Baby kuna mjinga mmoja kagonga gari uliloninunulia, please njoo uongee nae she is so stupid, nahisi na mume wake stupid kama yeye.
BOYFRIEND: Baby I am coming, unajua watu wa jiji hili wamechanganyikiwa ngoja nije nifunze adabu.
Muda si mrefu jamaa akaja, kumbe alikuwa ndiye mume wa MAMAKIVTZ......kila mtu amalizie sinema hii


YULE MCHORA KATUNI MCHOKOZI KING KINYA KARUDIA TENA


BABY UNAIONA HII HALI YA MVUA? NIJE KWAKO?

MKAKA:Hello baby unaiona hii hali ya hewa?
MDADA: Yaanii
MKAKA: Mi nawasha gari nakuja kwako Baby
MDADA: Aise ntafurahi kitu, lakini si unajua leo tarehe ngapi? Siko vizuri, 
MKAKA: Kivipi?
MDADA: Niko kwenye siku zangu
MKAKA: Dah aise nilisahau jana nilivyopaki gari kumbe mafuta yalikuwa yameisha kabisaa na sina hela 
MDADA: Nakutumia kidogo kwenye Tigo Pesa
MKAKA: Nilisikia kuna kitu kinagonga kwenye injini nadhani injini imenoki. Its ok ntakuja siku nyingine
MDADA: Unajua nini hata mimi sio kwamba niko kwenye siku zangu ila tarehe zenyewe ndio hizi.
MKAKA: Ahh  ok basi nitajitahidi niazime gari kwa rafiki yangu nije
MDADA: Ok pitia pharmacy uniletee na towels kinaweza tokea kitu muda wowote
MKAKA: Huyu jamaa nimempigia hapokei simu sijui kwa nini. Basi tena bye kwa leo

WEEKEND PICTURES ENJOY

MDADA KUTOKA KWA PREZZO AJIELEZA -KUWA WAKWANZA KUMSIKILIZA


SIMBA WAIFANYIA NJAMA YANGA ISIJENGE STADIUM YAKE KUWA WA KWANZA KUONA USHAHIDI

Kwa kile ambacho mwenye macho haambiwi ona, wala mwenye upele haambiwa kuna, wachunguzi wa mambo wa blog hii chini ya Mhariri wake feki, wamegundua kuwa Mnyama akiwa na mtima nyongo kafanya kila mbinu kuhakikisha Yanga inashindwa kujenga uwanja wa kisasa wa soka pale Jangwani. Wapenzi wa Mnyama walionekana wakiwa na ndoo wakibeba maji toka baharini na kuyajaza kwenye sait ya kujengea stadium ya Kimataifa, hatimae maji kujaa kama inavyoonekana laiv kwenye picha. Mmoja wa Wachina ambaye alikuwa aombe tenda ya kujenga uwanja huo alisikika akisema haya,'Chiu fyu chu ha hwing hong kung fu'. Mkalimani mmoja alidai kuwa Mchina akilalamika kuwa atawapiga Kung Fu wote walioharibu hilo dili. Wakurugenzi wa Blohg hii wanaangalia uwezekano wa kuomba tenda ya kunyonya maji yale ili pale mahala pawe pakavu. Ni kitu rahisi uategeshea pamp halafu unafunga mpira wa maji mpaka baharini. Pampu inavuta maji yanapelekwa baharini, kwa muda wa masaa machache patakuwa pakavu kabisa.

11 April 2014

SAMAHANI NIMETUMIWA MESEJ HOME KUNA ISHU


Urafiki na watu matajiri una adha zake, siku ukimtembelea anakupokea kwa furaha kubwa;
MTAJIRI: Ahhhh bwana John karibu sana karibu, sijui tukae nje au ndani?
JOHN: Naona joto labda tungekaa nje
MTAJIRI; Huku chini ya miti kwenye gaden au kibarazani?
JOHN:Kibarazani
MTAJIRI: Vipi tukalie makochi au viti
JOHN: Makochi
MTAJIRI: Safi sana karibu bwana. Utakunywa nini? Juis, Chai, Kahawa, Soda, Whisky, Bia au wain?
JOHN: Chai
MTAJIRI: Ya rangi au ya maziwa
JOHN: Maziwa
MTAJIRI; Maziwa fresh,ya kopo, au ya unga?
JOHN : Freshi
MTAJIRI: Na sukari?
JOHN: Ndio
MTAJIRI: Sukari kawaida au super sugar?
JOHN: Samahani nawahi home wamenitumia mesej kuna ishu


SAMAHANI ZIPU YAKO IKO WAZI

Mheshimiwa mmoja aliombwa kutoa hotuba fupi kabla watu hawajaanza kula. Sasa si mnajua wanasiasa wakipewa kanafasi kakuongea, wanaanza na kasentensi kao maarufu,'Ndugu zangu mimi sina mengi ya kusema" Halafu wanaongea weeeeeeeee, kisha wanaweka kale kasentensi kao kengine,' Ndugu zangu najua nimeongea sana lakini nina mawili ya mwisho" Halafu wanabwabwaja weeeee. Jamaa mmoja alipoona maneno yanazidi chakula kinapoa, akachukua kikaratasi akaandika ujumbe mfupi na kuomba watu wamfikishie mheshimiwa. Mheshimiwa aliposoma tu ujumbe akakatisha hotuba kwa kuwaruhusu watu waanze kula. Watu wakamuuliza jamaa ulimpelekea ujumbe gani? Nilimuandikia,'Samahani zipu yako iko wazi'.

KUNA HABARI NZURI NA MBAYA

JUZI MCHUNGAJI KASEMA HIVI KANISANI: Leo nina habari nzuri na mbaya kuhusu michango ya ujenzi wa kanisa letu jipya. Habari nzuri ni kuwa tunazopesa za kutosha kumaliza ujenzi huo. Habari mbaya ni kuwa pesa hizo bado ziko mifukoni mwenu

KAMA KAWA IGENI


10 April 2014

HAYA IGENI
KING KINYA NI MCHOKOZI SANA..


UKIKOHOA TU UNAHARISHA

Jamaa alikuwa anakohoa kwa muda mrefu sana, kila dawa akipewa anatulia siku mbili kisha anaanza tena. Siku hiyo akaenda kwa daktari ambaye akamwambia atampa dawa itakayomaliza matatizo. Baada ya hapo dokta akampa dawa fulani;
DOKTA: Oyo sikiliza nimekupa dawa kali sana ya kuharisha JAMAA: Dokta mi nakohoa sasa unanipa dawa hii si kila nikikohoa ntakuwa najiharishia? DOKTA: Haswa, sasa ole wako ukohoe

KAMBUSU DEMU WAKO WA FESIBUKU

MKAKA: Mpenzi tabu yako we una wivu sana
MDADA: Aka mi sina wivu hata kidogo
MKAKA: Una wivu bwana
MDADA: Nilikuwa na wivu zamani sasa nimejifunza mwanamke mwenye wivu hujiharibia mwenyewe
MKAKA: Nibusu basi
MDADA: Umbusu nani? Toka hapa nenda kambusu demu wako uliye m'like' kwenye facebook

NOTI YA SHILINGI ALFU SABA

Tapeli moja mjingamjinga alikuwa na nia ya kutengeneza noti bandia za shilingi alfu kumi, si akakosea kaandika 11,000. Akastuka tayari ana noti kibao za shilingi alfu 11, akaona hata hivyo ajaribu bahati yake aende benki akazichenji, ili apate fedha halali. Akatoa pesa kaunta akaomba chenji ndogondogo, pesa zake zikapokelewa akapewa chenji ya noti za shilingi alfu saba saba

VICHWA VYA HABARI VYA MAGALIZETI YETU

 JAMANI KWANI LEO SIKUKUU YA WAJINGA? wacheni hizo

 Tehehehehehe inshu ya wabunge kuvuana nguo hii kali, ukiwa na elimu chini ya kiwango unapata watendaji chini ya kiwango

 Hahahahahahahahahahahahahahahahah duh no comment jamaa wana kamtindo ukicoment wanakusubiri ukienda Ulaya wanakuweka mtu kati,' Ehe we si ulijidai shabi sasa umekuja kwetu, siku ile ulisema nini?' unaanza,'Yu si ina aflikan tredishen, is not alaud ze men tu slip wiz ze men, bekoz zey will not get small childs, zeafo we stik tu awa tredishen'

Dogo ulchofanya sio kabisa kama kweli

KINGA SAIZ NDOGO ZAMKOSESHA BATA MHARIRI WETU

Mhariri asiye mkuu wa blog yetu hii amejikuta katika wakati mgumu jana usiku baada ya kujikuta kanunua kinga ambayo ilikuwa ndogo kuliko maelezo. Mhariri wetu mwenye matatizo ya kupenda kula bata kama hana akili nzuri na anyependa kununua vitu vya bei rahisi, maarufu vya Kichina, alijikuta akikataliwa kula BATA na mshiriki mwenzie katika ulaji huo wa BATA. Asubuhi hii ya leo ameingia ofisini akiwa na kisirani na kutuonyesha sempo ya kinga iliyomharibia siku yake. Jopo la wanataaluma na wasomi wa shule zenye elimu iliyoshuka wa blog hii wamekuwa na msimamo huu, ambao wameazimia kuufikisha kwenye Bunge la Katiba ili uingizwe kwenye Katiba, kuwa, Kwa kuwa huwa tunapima nguo dukani, kabla ya kununua , na kwa kuwa kama nguo haitoshi huwezi kununua, Katiba itamke wazi kuwa wenye maduka ya kinga waruhusu anaetaka, kupima ile kitu kama inamtosha kabla ya kuinunua.

8 April 2014

WAHENGA WALISEMA


MKUU WA IDARA YA HISTORIA WA BLOG HII AMEFANYA UCHUNGUZI NA KUGUNDUA MAMBO MAKUBWA YA KIHISTORIA YALIYOFICHIKA.....KUWA WA KWANZA KUSOMA  misemo na mawaidha ya busara yaliyowahi kutolewa na viongozi wetu wa zamani;
1.     Ukizubaa kwenye whatsapp vita itakupita…..Chief Mkwawa 1852
2.     Katakata ya maji itatuuwa………….Kinjekitile  1904
3.     Kila mwananchi anastahili kuwa na Fridge…..Chief Rumanyika 1882
4.     Marufuku kunitumia sms……Chief Songea 1887
5.     Tumieni Mkorogo …….Karl PetersHII TSHIRT INALETA UTATA MTAANI


7 April 2014

ETI BABA MTU STUPID YUKOJE?

DOGO: Eti baba mtu stupid yuko je? DADDY: Hilo ni swali zuri sana, a very good kweshen kwa kweli I am praud of you, you see mwanangu, mtu stupid ni yule ambaye akiulizwa just a simpo kweshen, yaani swali dogo sana basi huanza kulinyumbulisha na kuongeza mofimu na fonimu katika hilo swali, kuanza kutafuta, tena infact bila mantiki yoyote basis ya swali,na baada ya hapo kufanya mchanganuo na hatimae kukam up na solushenz ambazo in prinsipo hazikuweko katika swali husika kiasi cha kwamba aliyeuliza swali anakuwa haelewi hata kitu, umeelewa DOGO: Hapana

NILIBADILISHA VICHWA

Mama mmoja alifiwa na mumewe, akaenda mochwari kucheki maiti ya mumewe kwa mara ya mwisho, akakuta mumewe kavalishwa suti nyeusi akalalamika sana kuwa mumewe aliomba azikwe akiwa amevaa suti ya bluu. Muhudumu wa mochwari akajitahidi kumpoza na kumwambia atajitahidi kuona la kufanya. Kesho yake siku ya mazishi wakati wanaaga maiti yule mama akapata furaha ya mshangao alipokuta maiti ya mumewe imevalishwa suti ya bluu. Akamaliza shughuli za mazishi kwa shukrani kubwa akaazimia lazima akamzawadie mhudumu wa mochwari. Kesho yake akaenda mochwari, akamkuta muhudumu na kumshukuru sana kwa kuwezesha mumewe kuzikwa na suti ya rangi aliyokuwa anataka.  
MAMA: Asante sana uliwezaje kumbadili nguo? MUHUDUMU: Mama ulipotoka tu si akaja mama mwingine kumbe mumewe alivishwa suti ya bluu, japo alikuwa anataka kuzikwa na suti nyeusi. Nikaona jibu kumbe rahisi sana, nikabadilisha vichwa.!!!!!

HOTELI YETU HAINA PANYA

MHUDUMU: Hoteli yetu haina panya kabisa MTEJA: Ina maana ni safi sana basi MHUDUMU: Hapana chakula cha hapa hotelini ni kibaya sana mpaka panya wamekimbia

NIMEKUMBUKA WIMBO WA DR REMMY-USINGIZI SIRI YAKE NINIIII?


NGUMI ZA WEMA NA KAJALA... MHARIRI ANAPINGA

Mhariri wetu mkuu ambaye ni mpenzi mkubwa wa bendi ya Njenje amepinga vikali kuwa Wema na Kajala wameshawahi kurushiana ngumi Njenje. Mhariri wetu feki anadai kuwa hata hajawahi kuwaona watu hawa huko kwenye muziki wa Njenje. Kwa hiyo habari ndio hiyo Wema na Kajala hawajawahi kurushiana ngumi Njenje