PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NILISIKIA KAMA UMENISALIMIA

PEDESHE mmoja kapanda basi Ubungo akiwa anaelekea Moshi, akajikuta kapata kiti kimoja na binti mzuri ambaye alikuwa na novo yake na simu kali anatuma ujumbe kwenye whatsapp.
PEDESHE: Binti hujambo? naona tuko siti moja..... Binti kamuangalia jamaa toka juu mpaka chini kisha kwa dharau akashusha mawani yake ya jua na akavaa headphone zake na kuendelea na shughuli zake. Msafara ukaenda kwa masaa kadhaa hatimae karibu na Korogwe gari likasimama ili watu wakale. Kabla ya kuinuka Pedeshe akatoa bulungutu kubwa la noti na kutoa kumi mbili ili kununua chakula, binti kuziona tu macho yakamtoka, akavua headphones na kumuangalia Pedeshe kwa jicho la mahaba.
BINTI: Nilisikia kama umenisalimia, mi sijambo, shkamoo dadii karibu kiti

Comments