PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

BLOG MAKINI YAMFUKUZA KAZI MPIGA PICHA WAKE, NA KUMPIGA MARUFUKU ASISHIKE KAMERA MAISHA YAKE YOTE NA BAADA YA MIAKA KUMI

Wapenzi wa soka wakiangalia mpira kwa makini
 Mhariri wa blogu hii feki aliona amtume mpiga picha wake mkuu aende na simu yake ya mkononi kwenda kufuatilia mechi kati ya timu ya wananchi na timu kutoka nchi ya farao. Alitumwa kazi rahisi sana, alitakiwa kuleta picha za mashabiki wakiangalia mpira, maana tayari taarifa za siri zilikuwa zimeliki kuwa kuna mashabiki wa timu moja yenye ofisi sehemu zinapouzwa TV na redio feki wameanza kusherehekea ushindi wa farao kwa kung'oa vigoda vya uwanja mkuu wa paredi. Sasa huyu mpiga picha akarudi na kipicha (Hichohapo juu)  aliochodai kuwa aliwakuta mashabiki wa soka wakiangalia mpira. Mhariri kidogo apate presha ya kushuka, Hivyo kamfukuza kazi na kumpiga marufuku kushika kamera maisha yake yote na miaka kumi baada ya hapo.

Comments