HATUPIMI BANDO

31 March 2014

NAOMBA LITA MOJA YA KUKU

Gulo na binamu yake Fulo waliingia kwenye bucha;
GULO: Naomba lita moja ya kuku wa kizungu......watu waliokuweko walipigwa butwaa kidogo kisha wakaanza kucheka kwa nguvu. Fulo nae akaanza kucheka mpaka machozi yakamtoka
GULO: Sasa na wewe Fulo unanicheka mi mwenzio kwa kosa gani?
FULO: Nacheka kwa kuwa umeomba lita moja ya kuku, sasa huoni tumesahau kuchukua chupa? Tutawekea wapi? hahahahaha

POZI LA WIKI


WAHENGA WALISEMA......


Ukimkuta baba mwenye nyumba kaka kwenye  mkeka, kamwe humuombi akuletee kiti.

28 March 2014

MAN U...TUJIPANGE UPYA..ushauri wa bure


Kutokana na upenzi wa BLOG hii kwa timu yangu ya Man U, imeonelea kwa kipindi hiki cha mpito timu isajili watu wafuatao.

 KIPA: Superman
MABEKI: Undertaker, Randy Orton na Big Show
VIUNGO: Jackie Chan na Jet Lee
MASTRAIKA: CM Punk, Spiderman, Mike Tyson, Rambo, Rooney

KOCHA: RAIS wa Korea kaskazini  

 Maamuzi magumu kwa wakati mgumu. Tunatanguliza shukrani.

JE UNATAKA KUJA DAR ES SALAAM? ZIJUE STAILI ZA KUVUKA BARABARA KWANZA

Kwa kweli blog hii asubuhi hii imeona itoe ushauri kwa ndugu wananchi ambao wanaopanga kuja katika jiji la Dar es Salaam aidha kutembea au kuhamia au hata kuja kufanya kazi ya uhauzgelo. (Siku hizi blog hii imegundua kuna mahauzgelo kadhaa wanaoisoma ili kuongeza akili.)
Ndugu mwananchi, ukifika Dar katika moja ya mambo ambayo yatakuchanganya ni namna ya kuvuka barabara. Kwanza kuna  barabara za aina nyingi sana, kwa mfano kuna nyembamba za njia moja, ziko nyingine ni njia mbili, kuna hata moja inatoka Moroko hadi Mwenge ambayo hata wanasayansi wa kimataifa wameshindwa kujua kama ni ya njia 3,4,5 au 6. Ni hatari sana kuvuka barabara hii ya Mwenge Moroko.
Ukifika Dar kabla hujavuka barabara kwanza angalia kushoto, kisha kulia, kisha kushoto, kisha kulia chonde chonde usianze kuvuka hata kama hujaona kitu pia tumia masikio kusikiliza kama kuna kitu kina kuja, kuna hawa jamaa wa bodaboda na bajaj, huwa wanazuka kama majini ghafla unawakuta wako mguuni kwako ni muhimu sana kuhakikisha hawako jirani, bado usinyanyue mguu kuvuka angalia juu kwanza, hapa Dar kumekuwa na mchezo wa kujenga ghorofa kwa kutumia mchanga wa baharini ili kupunguza matumizi, ghorofa kadhaa zimekwisha dondokea vichwani mwa watu hapa mjini, hivyo angalia juu pia kucheki kama ghorofa la jirani liko poa? Wakati huohuo angalia nyuma, mji una vibaka huu balaa. Kama una mtindo wa kizamani wa kuweka pochi mfuko wa nyuma ni muhimu uwe na jicho huko usije ukavuka barabara kumbe wenzio wamchukua pochi. Kama uko mitaa ya Tandika, Manzese, Kinondoni Mkwajuni wakati unataka kuvuka ukisikiaa  ghafla mtu anakwambia "mdudu huyo, mdudu huyo", we endelea kuvuka usiogope hao ni matapeli wanataka kukuchanganya wakuibie simu. Baada ya hapo kama kila kitu kiko poa, Mungu akusaidie anza kuvuka huku ukikwepa magari kwa staili ya Rambo anavyokwepa risasi. Hii staili ya kukwepa risasi inaweza kukusaidia sana maana pia unaweza kuwa unavuka barabara ukakuta kuna jamaa wameamua kutembeza risasi kwenye shughuli zao za ujambazi. Hata hivyo wanyalukolo wenzangu  karibuni Dar

27 March 2014

DUH CHAMBUACHAMBUA YA VICHWA VYA HABARI LEO

WAZIRI WA CONSTITUTIONAL REFORM WA ITALY MARIA BOSCHI

Kila nchi ina taratibu zake za uvaaji, na msianze hapa kuvaa hivyo kila sehemu eti kwa kuwa waziri wa Italy alivaa

UNATOKA WAPI NA KANGA MOJA?

Jamaa karudi home kalewa njwiiii, kiasi cha saa nane usiku.
JAMAA: Mke wangu fungua
MKE: Sifungui utalala hukohuko
JAMAA: Basi najitumbukiza kwenye hili shimo la maji machafu nife..........Jamaa akafunua tenki la maji machafu akatumbukiza jiwe... Mke akafungua mlango akatoka nje haraka na kanga moja, jamaa akaingia ndani na kufunga mlango
MKE: Nifungulie we mpumbavu
JAMAA: Lala hukohuko
MKE: Napiga kelele
JAMAA: Piga halafu watu wakija utawaambia unatoka wapi saa hizi na kanga moja

26 March 2014

WAMENIBAMBIKIA KESI MKUU

Mshikaji alijikuta yuko mahakamani kwa kosa la kuiba gari.
HAKIMU: Mshtakiwa unamaelezo yoyote?
MSHKAJI: Mzee, hawa jamaa wamenibambikia kesi, ishu nzima ilianza nilipokuwa pale masikani kwetu naosha magari kama kawa. Wakati nalamba yule maza pale akaja na ndinga lake la nguvu, akaniambia nilioshe, mi nikalipiga maji kisawasawa, huyu maza akanambia niiingie kwenye gari yake kuna ishu muhimu, akanichukua mpaka pale Sinza Madukani, akaniambia nichague viwalo, nikachagua nguo za nguvu akalipa, akanambia nimsindikize home kwake, tukasepa, nikafika kwake, mjengo wa nguvu, akanambia nioge nikaoga fresh, ile natoka bafuni akanipa msosi wa nguvu nikashushia na mzinga wa Nyagi, kisha akaniita chumbani kwake, akasaula akajitosa kitandani, kisha akanambia,
MAZA: Mpenzi nimekupenda sana, nimekuridhia kila kitu, chukua unachotaka.  Basi kusikia hivyo mzee wangu nikacheki kushoto , nikacheki kulia nikaziona funguo za ndinga lake, nikaona poa ngoja nichukue mkoko. Nikachukua nikasepa, sasa hawa polisi wanasema nimeiba gari how kam mzee wangu?
HAKIMU: Kaaazi kwelikweli mbombo ngafu.

NINACHOHITAJI SASA NI MWANAUME TU

Sugarmummy kakutana na kiserengeti boy cha nguvu, akaona kapata bwana smart na handsome. Akamtoa out, wakala, wakanywa na kuhave good time, baada ya chakula safi vinywaji kwa wingi, hatimae wakiwa hoi kwa ulevi wakafika nyumbani kwa Sugarmummy. Wakiwa chumbani wamepumzika;
SUGARMUMMY: Ninachohitaji sasa ni mwananume tu
KISERENGETI BOY: Hata mimi

VAA UPESI KAITE AMBULENSI


Waifu karudi ghafla nyumbani toka kazini, si akasikia sauti za ajabu toka chumbani kwake, akahangaika kufungua mlango uliokuwa umefungwa kwa funguo hatimae akauvunja na kuingia chumbani akamkuta mumewe akitetemeka kitandani;
MKE: We vipi?
MUME: Presha imepanda mke wangu, mke akakimbilia sebuleni ili apige simu ambulensi ije wakati anahangaika kutafuta simu yake kwenye mkoba, mwanae akaja akamwabia,'Mama, mama, mama mdogo  yuko uchi kwenye kabati chumbani kwenu', Mke akatupa simu na kurudi chumbani alipofungua mlango wa kabati akamkuta mdogo wake kabatini bile nguo nae anatetemeka ,
MKE: Na wewe vipi unakaa bila nguo unatisha watoto wakati shemeji yako anataka kufa presha. Vaa upesi kaite ambulance pumbavu mkubwa.

HAPA PANAITWA UBUNGOWatani zangu waliokuwa kwenye basi wakiwa wanaingia kwa mara ya kwanza jiji la Dar es Salaam walikuwa wanabishana namna ya kutamka jina la jiji hili, mmoja akasema Darislamu mwingine akisema Daslam. Waliposhuka tu kwenye basi wakamwona jamaa mmoja baada ya salamu wakamwambia 'Bwanawewe si tunu ubishi, hebu sema wewe polipoli hapa panaitwa wapii?' Jamaa akawaambia, 'Hapa panaitwa UUUU BUUUU NGOOO'

JUMA LETE NYUMA

Juma kaenda kuomba kazi ya uboi kwa muhindi, mambo hayakuwa mabaya kwa wiki mbili za kwanza. Siku hiyo ndugu zake bosi wakamtembelea bosi, Juma akaambiwa apange meza ya chakula, akaweka vizuri sahani, visu, vijiko lakini akasahau kuweka  uma. Wageni wote wakawa wamekaa kwenye viti vyao , Juma akiwa nje anapumzika, ghafla akasikia;  
BOSI: Hanee Juma lete nyuma..... Juma hakuamini alichosikia,  
JUMA: Umesemaje Bosi? 
BOSI: Ve apana sikia, lete nyuma vageni nataka...
Bosi hakujua na mpaka leo hajui ni kwanini Juma alimtandika kama vichwa sita vya mfululizo

MAGAZETI YANASEMAJE JAMANI?

 Yanga kumbe nyanya tu dah

 Wapi Man U?

Hahahahaha kwa hiyo sherehe za mechi ya alfu zilikuwa na pilau.....wahariri wa kibongo kiboko

24 March 2014

DADIE LOVE YOU KISS KISS

Dadie yupo Coco Beach na binti mmoja anaependa sana kutokea kwenye magazeti pendwa. DADIE: Mtoto ulisema birthday yako next week? BINTI: Yeah Dadie DADI: Nataka nikununulie kitu unikumbuke daima, unaona lile BMW jekundu pale? BINTI: Wauuuu ukinunulia lile mbona watazima sigara zao, yu are soooo sweet baby, unajua kumhendo msichana, love kiss kiss, DADIE: Subiriiii, unaona lile BMW jekundu, basi nimekununulia rangi ya kucha inamech rangi na lile BMW

HAYA TENA TOKA MAGAZETINI23 March 2014

TOA USHAURI JAMAA AJITETEE VIPI?SAMAHANI BABY NILIDHANI UNA MIMBA

MDADA: Halloo Baby, Mpenzi kuna kitu cha muhimu naomba nikuone tuongee
MKAKA: Nini tena usinambie una mimba
MDADA: Baby kwa vyovyote vile nyumbani watanifukuza wakishasikia  nina mimba yako
MKAKA: Huo upumbavu sitaki kuusikia si nilikuwa ninakupa fedha ukanunue vidonge vya majira?
MDADA: (Huku akilia) Ndio honey lakini imetokea kama ajali, samahani baby
MKAKA: Samahani baby kamwambie baba yako, sitaki kuiona sura yako nyumbani kwangu tena
MDADA: Baby please nielewe
MKAKA: Hata ukiniona barabarani usinisalimie mwendawazimu mkubwa.
MDADA: Lohhhh kumbe ndivyo ulivyo? Nashukuru Mungu sina mimba nilikuwa nakutest tu
MKAKA: Ahhhh si unajua baby panic ya kawaida hiyo, vipi uko wapi saa hizi nikupe mchemsho?
MDADA: Sikutaki wala sitaki mchemsho wako wewe huna ubinadamu
MKAKA: Achana  na hayo, samahani baby
MDADA: Samahani kamwambie mama yako

NG'OMBE , SIAFU NA NGEDERE WALIKUWA WANATAMBIANA.........

Ngombe, Siafu na Ngedere walikuwa wanatambiana, kila mmoja akijisifu kuwa yeye ndie mfanyakazi bora.
Ngombe: Mimi naweza kutoa hadi lita 30 za maziwa kwa siku kutokana na kula majani tu
Siafu: Mi naweza kujenga kichunguu chenye ukubwa mara nyingi kuliko mimi.....Vipi mbona wewe hujielezi uwezo wako? Umeshasoma uwezo wa wenzio haya tunasubiri sifa zako mwaga hapa

22 March 2014

LEO NI VICHWA VYA HABARI VYA MICHEZOOO TU

 Italazimika twende wenye hela zetu, tukanunue mtu

 Hahaha Mshirikina utamjua tu, kwa kuwa yeye anachinja sana kuku kulinda ajira anajua ndo kila mtu dah

 Nyie Wanyalukolo si mumuombe Mhariri wa blog hii mboma mwenzenu? halafu tajiri kinoma

Hahahahahahahaha kwa hiyo aidha ingia na chips kavu au chips Mayai. Chips kuku itakupeleka jela......

21 March 2014

BAADA YA CHANGUDOA KUWA MJAMZITO.....................

Changu kenda klinik maana alikuwa na mimba, akakuta tangazo, KILA MJAMZITO LAZIMA AJE NA BABA WA MTOTO ..
CHANGU: Nesi mi changudoa sina mume
NESI: Hapo itakuwa ngumu hatuwezi kukuhudumia. Yaani unataka kusema huwezi kukumbuka nani haswa ndie aliyekutia mimba?
CHANGU: Hivi nesi we ukila maharage unaweza kulitambua lile harage ambalo limekufanya ujambe?
NESI: Haya dada njoo tukupime

VICHWA VYA HABARI MAGAZETI YA LEO HAHAHAHAHAHAHAHAHA

 Ataungua ohooo
 Hahahahahahahaha walimu hiyo fiksi hahahahahahahaha

 Okay sasa waliiba matofari ya nyumba waliovunja? auuuu

Mabingwa wa mielekamieleka ok nimekusoma mhariri

20 March 2014

HAWA WATAYARISHAJI NI WABABAISHAJI WA HALI YA JUU

Jamaa kanunua tiketi mbili za bahati nasibu, na tiketi moja ikashinda zawadi ya shilingi milioni tano. Akawa anahojiwa na mtangazaji maarufu. MTANGAZAJI: Je unajisikiaje baada ya kushinda milioni 5? JAMAA: Kwa kweli ndugu mtangazaji sina raha kabisa, nimepata hasara ya hii tiketi nyingine ambayo haikushinda kitu, ningejua ningenunua tiketi moja tu. Hawa watayarishaji wa bahati nasibu hii, ni wababaishaji wa hali ya juu

19 March 2014

CHEZEA WAHINDI WA BONGO WEWE--ONA VIDEO YA KUCHKUCH KOTAHE


BLOG YATUMIA FURSA NA KUANZA BIASHARA YA KUUZA BRASHI ZA VIPARANGOTO


Baada ya huyu naninihii huyu kupigwa kipara swafii, ni wazi kutakuwa na wimbi kubwa la TEAM VIPARANGOTO nao kuamua kupigwa vipara, na  kwa kufuata mstakhabari wa kisiku hizi Blog yenu fake imeamua kuchukua fursa na kuagiza toka China kontena sita za brashi za vipangoto, wahi brashi yako sasa bei poa

MHARIRI AOGOPA KUTOA UCHAMBUZI WA HILI


18 March 2014

MUVI KALI INAENDELEA KATIKA ULIMWENGU WA SOKA ...LOST SEASON ONE


JE, ANGEMEZA SHILINGI ALFU KUMI?

Mtoto karudi nyumbani kwao na sura ya unyonge sana;
MAMA: Vipi mbona hivyo kuna nini huko?
MTOTO: Hiyo nyumba ya jirani lazima ni maskini sana
MAMA: Kwa nini?
MTOTO: Mtoto wao kameza shilingi mia nyumba nzima wanalia, je angemeza shilingi elfu kumi?

JE MHARIRI WA GAZETI HILI NAE ALISHUSHIWA KICHAPO? WAPELELEZI WETU WAMO KAZINI

Baada ya uchunguzi wa kina, imeonekana iundwe tume kumcheki kama huyu Katibu aliishia kwa Steve tu, maana na huyu mhariri wa gazeti hili inawezekana nae kichapo kilimuhusu na kusababisha ang'olewe meno kiasi cha kushindwa kutamka neno AMSHUSHIA na kuishia kuweza kusema tu AMSHUHIA maana baada ya hapo ndipo pia mtu huishia kusema MHOHO  badala ya MUHOGO......upelelezi unaendelea

HE KUMBE HATA MAJOGOO WANATAKA NDOA YA JINSIA MOJA DAH

MKULIMA mmoja alikuwa anafuga kuku wa kienyeji. Alikuwa na majike 25 jogoo mmoja. Baada ya kuona jogoo amekuwa mzee akaamua kununua jogoo jipya. Ile jogoo mpya kufika tu kukawa na mazungumzo kati ya majogoo;
JOGOO MZEE: Karibu dogo, karibu sana nadhani tutashirikiana vizuri ili kuhakikisha hawa kuku wanataga mayai
JOGOO DOGO: Wewe umeshazeeka ndio maana nimeletwa mimi damu mpya. Hakuna kushirikiana wala nini umekwisha wewe
JOGOO MZEE: Kama unaona nimekwisha basi tufanye mashindano unipime
JOGOO DOGO: Mashindano gani?
JOGOO MZEE: Tushindane mbio tuzunguke nyumba mara mbili, ukishinda mi najitoa. Ila kwa kuwa mi mzee naomba uniache nianze kama hatua kumi mbele
JOGOO DOGO: Poa sana hiyo haya anza kukimbia... mbio zikaanza, walizunguka nyumba mara moja tu, mkulima akamfwata JOGOO DOGO akamkamata na kumchinja huku akilalamika
MKULIMA: Yaani dunia imeharibika, huyu Jogoo wa sita sasa namnunua badala ya kufukuza majike analeta ubasha hapa. Yaani Museveni yuko sawa kabisa.

17 March 2014

NAKUWEKA KWENYE INSTAGRAM HATA SUPASTAR WOLPER ATAKUONA


HAHAHAHA VICHWA VYA HABARI ZA MAGAETI YETU BONGOLAND

 Dah hapa sitii neno nisije nikajikuta mahakamani bure  na kablogu kangu

 Mzee si alikuwaga na magesti pale Magomeni Makanya toka longi au sio yeye? Lazima kuna kitu anakijua.

 Ndugu mhariri ulikuwa na maana gani bado sijakusoma

DRIDGE---neno jipya maana yake DARAJA kama mnabisha kabishaneni na mhariri wa hili gazeti sio sisi wajameni.

16 March 2014

CHONDECHONDE UKIKAMATWA NA POLISI USITOE MAJIBU HAYA

Tafadhali ukiwa unaendesha gari ukasimamishwa  na polisi tafadhali jizuie usitumie majibu yafuatayo:
-       i. Hebu nishikie konyagi yangu nikutolee leseni
-       ii. Nilitaka na mimi kuwa polisi nikaona huu ufala
-       iii.Unajua mshahara wako unatoka kwangu mimi mlipa kodi?
-      iv. Bosi wako mwenyewe tulisoma nae praimari alikuwa mjingamjinga
-      v.  Umejuaje nimekunywa, au na wewe mdau?
   vi. Jela zimetengenezwa kwa ajili yetu

14 March 2014

HARUSI YA WIKI


WAKATI MTOTO WA KIZUNGU ANALILIA KUWA MWAFRIKA........ VIDEO


VIPI KATI YA HIVI ULIFANYA ULIPOKUWA MDOGO?


-       kuchovya mkate kwenye chai
-       kuweka wali wote kwenye mchuzi
-       kuvunja mfupa ili unyonye
-       kuweka nyama pembeni na kula mwisho baada ya kumaliza chakula
-       Kuonyesha wenzio chupi mpya
-       Kuomba pipi anayokula mwenzio
-       Kulamba sahani mpaka iwe safi
-       Kuvua viatu vipya,  na kutembea navyo mkononi ili watu wavione
-       Kuvaa kaptura mbili ili ukipigwa mboko zisiume
    

MSAADA TUTANI

HII misaada mingine inakuwa kama misaada ya wale jamaa zake Obama

CHEZEA YANGA WEWE???????

WALABU WENYEWE WANAIOGOPA

13 March 2014

BREAKING NEEEEEEEWS WAZIRI WA MAMBO YA NJE AENDA KAZINI NA BAISKELI

Teh teh teh kama ulifikiri Waziri wa Bongo au Afrika ujue hiyo ni ndoto, huyu ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark au kwa Kidenish Udenrigsminister, Bwana Martin Lidegaard ambaye kapata huo wadhifa karibuni kabisa. Lakini si mbaya kubaki na ndoto kuwa one day Waziri wetu mmoja wapo atavunja mwiko na kupanda daladala kwenda kazini, akichelewa ndio atajua apige akili gani daladala na watu wote wawe wanawahi kazini.
Makofi kwa hii blog kwa mara ya kwanza imeongea sens

MHARIRI ACHUNGUZA VINGLEZA VYA MUVI ZA KINAIJERIA


AROO NYIE WASANII WA BONGO MNAPENDA SANA KUBEBA UNGA TURIA TUKUSACHI

Tehe tehe tehe  reo tumerikamata risanii ririkuwa rinatia wasiwasi tukari aresti ili turisachi kama rimebeba maunga, rinaonekana ririkwisha shusha maana turirikuta harina kizibiti

YULE MAMA ANAMNYONYESHA MWANAE

Mlokole mwenye guest alikataa yanki mmoja aliyekuja na mama mtu mzima kupata chumba akisisitiza kuwa guest yake hairuhusu uasherati. Yule mama akaja juu na kumwambia Mlokole kuwa yule kijana ni mwanae, basi wakapewa chumba. Mlokole akamtuma muhudumu mmoja akachungulie kwenye dirisha la wapangaji hao  ili kuona kama kweli ni mtu na mzazi wake. Baada ya muda muhudumu akarudi na jibu,' Mzee kweli wale ni mtu na mtoto wake, nimemuona yule mama anamnyonyesha mwanae'

12 March 2014

NATAKA KUFARIKI NIKIWA NA WEZI KULIA NA KUSHOTO

Msanii mmoja wa Bongo alikuwa kaugua sana hatimae daktari akamwambia kwa kweli una muda mchache sana wa kuishi, ni vema ujitayarishe. Msanii akaomba meneja wake na msambazaji wa kazi zake waitwe pale hospitalini. Walipofika akawaomba meneja akae upande wake wa kulia na msambazaji akae upande wa kushoto. Walipojipanga hivyo ndipo msanii akatoa wosia wake.
MSANII: Kama mmesoma enjili, wakati Yesu alipokuwa  msalabani dakika zake za mwisho, kushoto kwake na kulia kwake kulikuweko na wezi wawili.  Na alifariki wezi hao wakiwa nafasi hizo. Nami nimeona niige mfano huo kwa kufariki nikiwa na wezi kulia na kushoto kwangu, kwaherini. Akakata roho.

BODABODA


VICHWA VYA HABARI VYACHAMBULIWA NA HAUSIGELO WA BOSI WETU

 Blog yenu  tata imetuma jeshi lake ikamhoji Chief Malangalila ni chifu wa wapi na wa nini?Bongo full kuhujumiana, au hata sisi hapa ofisi ya blog tunahujumiwa tusipate matangazo? Ndugu wananchi wote bila kujali wewe ni fisadi au unafisadiwa tutaendelea kukuletea vichekesho humu labda Gugo watuhujumu......Habari hii imeletwa kwenu kwa hisani ya BABANGU MDOGO

11 March 2014

KWA WALE WASIOPENDA U LUPITA NYON'GO

TUMIA FAIR AND LOVELY.........tangazo hili nimeliweka hapa bure

TUANGALIE MAVICHWA YA HABARI MAGAZETI YA LEO

 Blog yenu itamtumia namba ya Mzee wa Upako............
 Ni kweli ukifanya usajili Kiswahili akina Suarez wanakuwa hawajui fomu zimeandikwa nini, aise Simba mna bonge ya akili

 Malaika Suarez, inawezekana mapepo yalikemewa na mtumishi mwenye upako

Sasa ilikuwaje mkashindwa kuwafunga kumi bila?