HATUPIMI BANDO

2 February 2014

TOFAUTI YA WADADA STYLE NA WAKAKA STYLE.

WADADA STYLE
MDADA 1: Hello mpenzi mambo
MDADA 2: Niko poa sweety, dah umenikumbuka mamii
MDADA 1: Yaani nimekumiss, nikaona nikupigie nikwambie leo naja kwako
MDADA 2: Dah nitafurahi mno mpenzi,  shosti navunja safari zangu zote nakusubiri
MDADA 1: Basi baadae sweety tutaonana...........Akikata simu tu  MDADA 2, anamwambia mdogo wake
MDADA 2: Yule Malaya kafosi kuja kunitembelea sijui ana umbeya gani? Au kaishiwa anataka nijee nimnunulie bia za bure, ataula wa chuya halooooo
WAKAKA STYLE
MKAKA 1: We mwendawazimu uko wapi?
MKAKA 2: Hii kali masikini bingwa wa kubip leo umepiga? Mkeo kakuruhusu leo ?
MKAKA 1: Hivi kwanini hujafa watu tule pilau?
MKAKA 2: Kufa sifi na leo nakuja kunywa bia bili yako, haya nikukute wapi?
MKAKA 1: Pale kwenye baa anayonywea baba yako, usipokuja ntashukuru maana hela yangu ina masharti, hakuna kulipia masikini. Alipokata simu tu MKAKA 1 akamwambia mkewe,
MKAKA 1: Yaani huyu jamaa, ni rafiki yangu toka utoto, tukikutana huwa raha sana, ngoja nikamtukane hukohuko bar.

No comments: