KIBIMBIF KIBAMBAF KIDANGANYA WATU

Luninga aka TV aka Kibimbifukibambafu kidanganyawatu ni kitu moja hatari sana. Siku hizi Kibimbifu ndio kimekuwa shule ya kila kitu. Kuvaa, kuongea, kuimba, kucheza, na siku hizi mpaka kulea.
Watu wanatengeneza video za singo zao kwa kukopi na kupest zile walizoona kwenye Kibimbifu, hata muvi zinatengenezwa baada ya wajanja wetu kuangalia muvi kwenye Kibimbifu, kasha kukopi na kupesti za kwao. Ila kali sasa ni wale jamaa zangu wanakopi na kupesti namna ya kulea watoto wao kwa kujifunza kwenye Kibimbifu.
Juzijuzi nilimtembelea rafiki yangu ambaye anajitahidi kuishi kama wale anaowaona kwenye Kibimbifu, sasa yeye ana kavulana kake kako nasari, nako anakalea kama vile vitoto vya kwenye Kibimbifu, na kwa vile kule nasari kamejifunza kutamka Dadi and Mami badala ya baba na mama, jamaa yangu anajiona mjaaaanja,  basi Kabwamdogo hako hakakaripiwi wala kukatazwa chochote, nilipata taarifa kuna siku kalimvua baba yake taulo alipokuwa katoka bafuni tena mbele za watu, jamaa akaishia kusema tu, ‘No Junia no, is bad” Na kucheka cheka huku akisifu, ‘Tatizo la huyu mtoto ni ana akili za kikubwa” Ene wei siku hiyo jamaa akanikaribisha kwake, basi kwa kweli ilikuwa kero, mara Junia kaleta mpira anaupiga mbele yetu anaangusha vitu, anatupiga usoni na mpira anaangaliwa tu, ‘Junia no’, anapanda meza mara kabati, jamaa zangu utadhani wamelogwa, wanakenua tu meno, ‘No Junia no” Mara mbili hivi kakaniparamia na kutaka kunivua miwani yangu, ‘Kwa ustaarabu wa nyumba ile na mie nikatoa ya kinafiki, ‘No Junia no’.  Bahati nzuri mama Junia akaingia jikoni, Baba Juni akaenda chumbani kidogo, sebuleni tukabaki mimi na hiki kidude kisichokuwa na chembe ya adabu. Si kikaanza vimaswali vya maudhi,’Leo umekuja kula kwetu?”  ‘Kwenu mna TV? Babako anakuleteaga chokoleti?” Kikawa mara kivunje kikombe mara glasi, mama yake anapiga kelele toka jikoni, ‘Junia yu a veri bed’. Ila chenyewe kikakosea kikanipanda kichwani na kuanza kunivuta nywele nikaona sasa hii zarau. Basi nilikishika mkono nikakitolea macho na kukifinya vizuri mgogongoni. Kwanza kilitoa macho kama kinataka kufa, kikaniangalia hakiamini akili yake kuwa kimefinywa na binadamu aliye hai, na mie nikakiambia kwa sauti ya chinichini,’We Junya ukinisogelea tena nakukata masikio’  E bwana we kilitimka mle sebuleni mkojo unakitirirka kikaelekea jikoni. Kufika huko nilitegemea kianze kulia kwa nguvu, kikawa kimya. Mama yake anakiuliza ’Junia umefanya nini tena baba?’  kimya “Junia what has happened?” kimya, mama yake akaja huku chenyewe kimejificha nyuma ya gauni la mamake,  ‘Huyu kafanya nini?’ Nikajibu kwa sauti ya mtu asiye na dhambi kabisa, ‘Wala sijui nimeona tu katimka hapa kaja huko’ Baada ya hapo kukawa na displin mle ndani tukala na kuzungumza bila fujo. Baba Junia kila mara akimwangalia mwanae na kumuuliza, ‘Junia a yu sik? Unaumwa?” Junia akinitupia jicho mwenyewe alikuwa ananyamaza anajua kuna kukatwa masikio. Wengine hatuangaliagi Kibimbifu ohooo

1 comment:

Blacktourist said...

Hahahah hii nimeipenda Uncle,
Me nge mtia makwenzi kabisa...

Post Top Ad

Powered by Blogger.