HATUPIMI BANDO

4 February 2014

ENYI BINADAMU ALAMA ZA NYAKATI ZITAWATOKEENI KARIBUNI


ENYI BINADAMU NISIKILIZENI…. Siku hiyo itakapofika.Siku ya kumi na nne ya mwezi ule wa pili wa mwaka, patatokea miujiza mingi…….. Hakika nawambieni ghafla wale wanadamu wenye simu za mkononi watawaambia maneno haya wenzi wao;
Nisamehe  nisamehe kwani sikupatikana  simu yangu ilionyesha Battery Low. Na wengine  watasema, Nisamehe nisamehe sikupiga kwani salio langu lilikwisha, na wengine watalia na kusaga meno wakiwambia wenzi wao, Nisamehe nisamehe kwani bosi wangu alinituma safari ya Mkoa ya ghafla. Kutakuwa na wengine wakisingizia magonjwa na ajali za ajabu na matatizo mengine hata kufiwa. Wengi hawatonekana na wenzi wao siku hiyo. Lakini furahini nawambia kwani alama hizi zitapotea iingiapo siku ya kumi na tano ya mwezi wa pili wa mwaka, Hakika hakika nawambia maneno yangu yatatimia.Ole wao watakaongoja na kukesha na kutegemea kualikwa kwenye karamu zenye vinubi na  na mvinyo, wekeni akiba pembeni ili muweze kujitegemea msije lia na kusaga meno........Joni Mblogaji 14:2

No comments: