PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

BREAKING NYEUSIIIIIIII WAPENZI KUSAJILIWA KABLA YA VALENTINEHabari zilizonifikia kutoka kwa mtu mkubwa ambaye ameomba nihifadhi jina lake (ili isijulikane kuwa yeye ndiye mbeya), ni kuwa uongozi wa mkoa mmoja unaoongoza kwa vituko na ambao uko baharini kabisa na wenye magazeti mengi kuliko mikoa mingine umeamua kupitisha sheria ndogo ya kusajili wapenzi kabla ya Valentine day ili kuepuka ngumi na fujo siku hiyo. Kila mwenye mpenzi atalazimika kwenda kwa ofisa utamaduni na kusajili jina la mpenzi wake . Taratibu zinafanywa ili teknolojia itumike ambapo ukisajili jina la mtu, sms inaingia kwenye simu ya yule uliemsajili ili akubali kuwa anakutambua na hapo usajili unakamilika. Pia kama kisha sajiliwa na mwingine usajili utagoma. Ushauri wangu ni kuwa kwa kuwa tunafahamiana mambo yetu, wahini kwa maafisa utamaduni kabla hamjawahiwa na wengine.
Anko J Kitime

Comments