HATUPIMI BANDO

28 February 2014

DREVA WA BLOGU HII AGUNDUA NJIA MPYA YA KUVAA MIKANDA YA USALAMA

DEREVA WA BLOGU HII MZIGO, ameonyesha ubunifu wa hali ya juu, ubunifu huu ambao utagombewa na wazungu wote mara watakapousikia, ni staili mpya ya kufunga mkanda wa usalama. Wazungu walikuwa wanaupitisha kwenye bega, dreva wetu kagundua kuupitisha shingoni, hii ni new invention made in hapahapa. Uongozi wa blog hii unategemea kumzawadia tuzo la mbunifu bora wa mwaka huu.


UTAJUAJE KAMA UNANUKA MDOMO?


Watu wengi huwa hawajui kuwa wana midomo inanuka ile mbaya, aidha kwa kuwa huwa hawapigi mswaki, au walisahau siku hiyo kupiga mswaki au pengine wana jino bovu…tatizo ni kuwa muhusika huwa hasikii hiyo harufu mbaya sasa atajuaje? Blog yako mzigo imekuja na baadhi ya dalili ambazo ukiziona ujue UNANUKA MDOMO ILE MBAYA
1.     Ukiona kila ukianza kubishana na mtu haraka sana anakubali kuwa wewe ndie mshindi wa ubishi huo, ujue UNANUKA MDOMO.
2.     Ukiona unahadithia rafiki zako bonge ya stori, badala ya kukuangalia usoni wanaangalia pembeni, ujue UNANUKA MDOMO
3.     Ukiwa unataka kumla denda mpenzi wako na ghafla anakwambia ‘Acha tu mi sipendi hayo mambo ya kizungu’, ujue UNANUKA MDOMO
4.     Ukitaka kumnong’oneza rafiki yako kitu sikioni, kabla hujamueleza anakwambia, najua unachotaka kunambia ujue UNANUKA MDOMO

MAMA MWANAO KAVUNJA REKODI

Mkuu wa Mkoa: mama mi ni Mkuu wa Mkoa, nimekuja kuongea kuhusu mwanao
Mama: Kuna nini tena baba?
Mkuu wa Mkoa: Si unajua mwanao alienda na wenzie Uingereza?
Mama
: Nilikuwa sijui baba
Mkuu wa mkoa: Basi mwanao ameenda huko na amevunja rekodi ya mbio za mita 100
Mama: Mungu wangu Mungu wangu, huyu mtoto, toka mdogo kazi yake kuvunja vitu, kavunja vyungu vyangu vyote hata kwa majirani nako kavunja sana, Baba naomba serikali  inisaidie kulipa mimi sina uwezo wa kulipa chochote, kama mnavyoona mi mjane

YULE MZEE NDUGU YAKE WA HUYU MZEE WA BLOG HII AKUTWA AKIUZA SURA YU TYUBU CHEKI VIDEO

HAHAHAHAHAHAHAHAHAHAHA yule mzee mwenye kabila moja na huyu mzee mwenye blog hii hatimae akutwa akiuza sura mbele ya kamera. Waandishi wetu mabingwa wa kukopi na kupesti si wameikuta hii video huko yu tyubu wakaikopi na kupest ishu za huyu mzee ambae kumbe ni mkorofi sana kadri ya muvi hii. Aise ngoja nicheke ntarudi baadae, Kama anavyosemaga Prof Jay Pamoko hahahahahahahahahahahaha

BABA MI THAMANI YANGU SHING NGAPI?

DOGO: Baba ingekuwa unanithaminisha na pesa, mimi thamani yangu shilingi ngapi kwako?
BABA: Dah mwanangu wewe sawasawa na mamilioni na mamilioni ya shilingi kwangu
DOGO: Baba niazime alfu kumi tu

JAMANI NAOMBA MSAADA, KUNA TATIZO KUBWA

Jamaa yangu amekwenda hospitali kagundulika ana cerebrocerebelloencephalotrigeminomedulloangiomatosis, ambayo imetokana na kuwa na tatizo la awali la pneumoconiosiliconosarcoidohistoplasmocryptococcitis, hii imepelekea kuwa na tatizo jipya la gastroenteroproctoentamoebovibrioescherichiosis. Halafu hana hata senti tano si atakufa kweli huyu jamani?

CHEZEA WENGINE BWANA


27 February 2014

HAYA TOTO NJULI TULA UPECHI

Bikizee kasikia ‘Izrail mtoa roho’ anasaka vizee zaidi akaona ajifanye mtoto mdogo ili asipatikane. Akaanza kula vyakula vya kitoto na kuongea kitoto. Siku moja wakati anakula Celelac, Izrail akamshukia.
IZRAIL: We unafanya nini?
BIKIZEE: Atula nyamnyam
IZRAIL: Haya tula upechi toto njuli alafu twende kutembea mjini achikia?

KUHUSU WASANII KUSAHAULIKA KWENYE RASIMU YA KATIBA


OYAA MSHKAJI UNATAFUTA NINI KWENYE HII BLOGU MZIGO?


KATIBA IWEKE KIPENGELE CHA KIWANGO CHA KUPIGWA

Anko ushione hivi, kwansha mi shina kosha lolote, jamaa nilikuwa namtania tu, shi ndio akaansha kunishukuma makonde bila shababu sha mshingi. Naomba chama na sheykali shiweke kipengele katika katiba kushuia ukatili huu. Polishi nao eti wananisheka wanashema hawanipi mpshlee, nijitibu mwenyewe shawa kwey hiyo?

MUMEO ANAKUNYWA KONYAGI?

WIKIENDI ndo hiyo wadada wamejazana saluni wanapambwa, ila mmoja katoa kali;
MDADA: Unadhani ulivyonipamba mume wangu ataniona mzuri?
MPAMBAJI: Inategemeana shosti. Mumeo huwa anakunywa konyagi?

KUPATA NA KUKOSA KIPI BORA?

BINTI: mama mtu akipata kitu na mtu akikosa kizuri nini?
MAMA: Vizuri apate kitu
BINTI: Nimepata mimba

WE FALA NINI? ANGEKUWA NA NJAA SI NINGEKUWA MAREHEMU

Sungura na Simba waliingia hotelini. Weita akaja kuwasikiliza,
SUNGURA: Nipe majani kidogo na karoti nyingi pembeni
WEITA: Vipi rafiki yako?
SUNGURA: Huyu hali kitu
WEITA: Vipi hana njaa?
SUNGURA: We fala nini, angekuwa ana njaa mi siningekuwa marehemu tayari

NIFUNGIE WOTE WAWILI TAFADHALI

Mdada alienda super-market kununua kuku, bahati mbaya kwenye friza kulikuwa na kuku mmoja tu, muuzaji akamtoa akamuweka kwenye mzani, akaonekana ana kilo moja na robo. Mdada akamuuliza muuzaji,’Huna mkubwa zaidi?’ Muuzaji akamchukua yule kuku na kujifanya kamrudisha kwenye friji, halafu akamtoa tena kwenye friji na kumrudisha kwenye mzani, safari hii akagandamiza mzani kwa gumba, kuku akaonekana ana kilo mbili. Mdada akasema ‘Duh afadhali huyu mkubwa kidogo, naomba unifungie nawachukua wote wawili’

26 February 2014

HAYA WANAFUNZI SUKARI INAPATIKANA WAPI?

Katika somo la Jiografia mwalimu akauliza; MWALIMU: Katika nchi yetu ya Tanzania, sukari inapatikana wapi Juma? JUMA:Sijui MWALIMU: Lazima unajua, wewe si unatumia sukari kila siku. Haya jibu upesi kabla sijakulamba viboko, sukari inapatikana wapi? JUMA: Dukani kwa Mchaga

ETI WAMEANDIKA NIMEKUFA JANA

ABOUDONA kafungua gazeti kakuta tangazo kuwa amekufa, akampigia simu rafiki yake mpenzi Luwi, ABOUDONA: Aisee umesoma gazeti la leo? Wanasema eti nimekufa jana huko Iringa, aise inasikitisha. LUWI: Ndio nimesoma pole sana bwana, kwa hiyo hii simu unanipigia uko wapi saa hizi? Uliondoka na ile simu yako ya Samsung?

MBONA JIRANI KUNA BINTI BEI ALFU HAMSINI TU!

Juha kataka kuoa kabinti fulani mtaani kwake, ile kujieleza akaambiwa mahari milioni tano. Akaja juu kwa mshangao 'Hee kwa ajili gani hiyo milioni tano? Hapo jirani nimeambiwa kuna binti yuko tayari kuolewa kwa shilingi alfu hamsini, halafu binti mwenyewe ana mimba kabisa tayari acheni utapeli shenzy nyie'

KIUKWELI JOTO BONGO LIMEKITHIRI, KAMA NOMA NA IWE NOMA


25 February 2014

PAMBAF, TOKA VALENTINE NDIO URUDI LEO


NIPE SALAD YA MOTO NA HEINKEN ZILE ZA BLUU

Nimeumbuka, jana katika kutafuta sifa kusudi na mie picha yangu itoke kwenye magazeti ya udaku si nikamtoa out huyu supasta wenu maarufu, nikampeleka kwenye kahoteli ambako chakula chake bei sawa na kamshahara kangu ka wiki. Nikafika pale mi stori nyiiiingi, mdada kaanza mara ananiuliza, 'Sijui ninywe Dompo au St Anna?" Mi nikawa nalamba kaglas kangu ka maji ya bure. Weita alivyokuja na MENU, supasta wenu kaiangalia kama vile anachagua kweli, mwishoe akaiweka chini na kumwambia weita kwa sauti iliyosikika mpaka meza ya tatu, 'Mie nipe tu salad ya moto na Heinken baridi zile za rangi ya bluu'. Nilitaka kujificha uvunguni mwa meza, ikawa haitoshi nikaomba ruksa kwenda msalani kidogo

VICHWA VYA HABARI VYA MAGAZETI YETU...MICHEZOOOOOOOOOOO


KWA HIYO NDIO KUSEMA????????????

DAH KWA HIYO NDIO KUSEMA???????????

BREAKING NEEEEEEEEEEWWWWWWWSSSSSSS SERIKALI YATANGAZA SIKU TATU ZA MAPUMZIKO KWA AJILI YA LILE BUNGE LETU

KATIKA HALI YA KUFURAHISHA SERIKALI YA BONGOLAND IMETANGAZA SIKU TATU ZA MAPUMZIKO KUSHEREHEKEA KUTEULIWA KWA WAJUMBE WA LILE BUNGE LETU LA POSHOPOSHO. KATIKA WARAKA AMBAO BADO HAUJASAMBAZWA AMBAO BLOG HII MAKINI IMEUPATA SEHEMU FULANI NYETI SANA, SERIKALI IMETANGAZA KUWA TAREHE 29/30 NA 31 YA FEBRUARI 2014 ZITAKUWA NI SIKU ZA MAPUMZIKO KWA WANANCHI WAKE

WEWEEEEE MUHINDI MWEUSI AKIIMBA GOROKI DUNIA KWISHNEY..VIDEO


NILIFUMANIWA NDO MANA NAVAA HERENI

RAFIKI: Hee ebwanee vipi tena hata wewe umevaa hereni?
BOUNSA: Yamenikuta makubwa ndugu yangu, wife alisafiri sinikafanya ujinga nikamkaribisha binti mmoja home, mdada alipoondoka kumbe kasahau hereni zake sebuleni kwangu, wife akazikuta kwenye kochi. Aliponiuliza zinafanya nini, nikalazimika kujitetea kuwa nimeamua kutoga masikio, ndo hivo tena, nilikuwa nalinda ndoa, sina ujanja

KUWA MTU MWEUSI NI KAZI NGUMU INAYOHITAJI UBONGO


24 February 2014

WASOMAJI WENYE AKILI WA CHEKANAKITIME TOKA NJE YA TANZANIA KWA WIKI HII, JAMAA WANA AKILI SANA HAWA

Kenya
23349
Indonesia
3671
Vietnam
3370
United States
2821
Bangladesh
1824
United Kingdom
1006
Nigeria
784
Oman
657
Netherlands
576
ASANTE NDUGU WACHEKAJI KWA KUINGIA BLOG HII, NGOJA NIENDE KWA MGANGA ILI MUONGEZEKE....HALAFU HAWA GOOGLE WANGEKUWA WANAONYESHA WADADA NI WANGAPI NI MUHIMU MTU UNAWEZA GHAFLA UKAJIKUTA UMETUA NETHERLANDS KWA MPENZI SEMENI UKAWA UNATAFUTA WENYEJI SI UNAONAEE, AU BANGLADESH, HALAFU HAPA NASHANGAA SANA KUKUTA VIETNAM IKO JUU, SIKUJUA KUNA WASWAHILI HUKO, JAMANI HEBU TUMENI UJUMBE KWENYE INBOX WATU WA INDONESIA, VIETNAM, BANGLADESH, NA NIGERIA KWA TB JOSHUA........................LET LOVE LEAD

NJAA MBAYA CHAI YA RANGI KWA MAPERA


HUYU HAUSGELO SIMTAKI HAJUI KUPIKA WALA KUFAGIA ANAEMTAKA AWEKE COMMENT HAPA TUWASILIANE NIMKABIDHI

KATIKA MAHAUSGELO bom huyu wa kwanza hajui kupika wala kufua, sioni sababu hata moja ya kumlipa hii alfu hamsini kwa mwezi, anaemtaka anambie kwenye comment nimkabidhi maana nilimtoa kijijini kwao alipomaliza la saba nikajua atanisaidia kumbe hakuna kitu. Nirudishiwe nauli tu ya kumtoa kijijini. Asante kwa kunisikiliza

SENGA NA PEMBE NI COMEDIANS WA KWELI ANGALIA VIDEO


KIMBELEMBELE NACHO HASARA JAMANI cheki video
UKINIPIGA UTAONA

Kipofu kampiga mtu mpaka kamuua, akafikishwa mahakamani;
HAKIMU: Kwanini umefanya ukatili namna hii?
KIPOFU: Mheshimiwa marehemu alisema mwenyewe,'We kipofu ukinipiga utaona', kwa vile nilikuwa na hamu kubwa ya kuweza kuona, nikajitahidi kumpiga sana  Ili  niweze kuona, bahati mbaya kafariki na mimi bado sijaona.

HUYO SIO MKE WANGU, UMESHAHARIBU KILA KITU

Jamaa alikuwa kwenye kibajaji mitaa ya Sinza kwa Wajanja, akapita nje ya bar moja yenye guesthouse, si akamuona mkewe akipotelea ndani ya hiyo gest, akapaniki.
 JAMAA: Dreva simama. Unataka laki tatu ya chapchap? DEREVA: Bila shaka mzee JAMAA: nimemuona mke  wangu kavaa ushungi wa njano kaingia kwenye ile gest, picha yake hii, ingia mtoe tena umlete hapa ukiwa unamtandika vibao.......dereva akatoka na baada ya dakika chache akatoka anamburula mwanamke na makonde juu, JAMAA: Mbona umekosea, huyo siyo mke wangu umeshaharibu mambo DREVA: Najua, huyu ni mke wangu, nae nimemkuta huko ndani, sasa ndio naenda kumtoa mkeo

23 February 2014

KARIBUNI WATUMIAJI WA VYOO VYA KISASA


BABA YUKO CHINI YA MAGUNIA

Jamaa alikuwa anapita kijijini akakuta ajali, akakuta Trekta lililokuwa limepakia magunia ya mahindi lilikuwa limepinduka na kuna kijana alikuwa anajaribu kuyasogeza magunia kutoka katikati ya barabara, akiwa amechoka kabisa JAMAA: Pole bwana, si ungepumzika kidogo KIJANA: Hapana baba hawezi kufurahi JAMAA: Huyo baba yako pia ni binadamu, hebu pumzika unywe maji kidogo, nakuona uko hoi KIJANA: Baba hawezi kufurahi JAMAA: Acha hizo, huyo baba yako kwani anadhani we mtumwa? Kokote aliko akijua ulivyofanya kazi atakubali lazima upumzike, kwani yuko wapi saa hizi? KIJANA: Yuko chini ya magunia.

ULIZINGULIWA SIKU YA VALENTINE? USIKONDE MALI MPYA IMEINGIA TUWASILIANE

LIKE UKURASA WETU WA FACEBOOK

HII SIO MELI NI PANTONI , TUKIFIKA KIGAMBONI SHUKA

Jamaa kamkuta mwanamke mmoja pale Ferry analia,  
JAMAA: Nini shida mama angu?
MDADA:Heri nife,maisha yamenishinda
MJAMAA: Huna haja ya kufa, sikiliza mimi ni baharia na meli yetu inaenda Ulaya leo, kama unataka ingia kwenye boksi nikakufiche stoo, meli ikitia nanga Ugiriki, nakutoa ukatafute maisha huko. Bibie akaona heri hilo akaingia kwenye boksi, jamaa akambeba na mdada akajikuta yuko kwenye stoo moja wapo katika meli, jamaa akawa anamletea chakula kila siku na mara nyingine yeye mwenyewe analala huko kwenye hako kastoo,kila mara akimhakikishia mdada kuwa wameshapita visiwa vya Komoro, siku nyingine akimwambia wako India. Zilipita wiki mbili ndipo yule mdada akagundulika na nahodha wa chombo hicho.
NAHODHA:We unafanya nini humu?
MDADA:Chonde naomba msinitupe baharini, nilindeni mkifika Ugiriki mnishushe
NAHODHA: Unajua mbona sikuelewi? Mdada akalazimika kumueleza nahodha ishu nzima. 
NAHODHA:Dah wala usipate taabu sikutupi popote, ila jamaa yako kakudanganya hii si meli ya kwenda Ulaya ni pantoni ya kwenda Kigamboni, tukifika huko shuka

CHEZEA NYUMBA NDOGO WEWE


21 February 2014

MAITI YALALAMIKA KUTEKENYWA

Jamaa walikuwa wanaosha maiti kuitayarisha kwa mazishi, ghafla maiti ikaanza kucheka;
MAITI: Kwi kwi kwi kwi Mnanitekenya mwanzenu jamani ahh...............Mlango ulikuwa mdogo

BIASHARA YANGU YA KUKU


20 February 2014

KATI YA MIMI NA MAMA YAKO UNAMPENDA ZAIDI NANI?

BABA: Kati ya mimi na mama yako unampenda nani zaidi?
DOGO: Nawapenda wote
BABA: Mimi ningeenda Dubai halafu mamako akaenda London, we ungeenda wapi?
DOGO: Ningeenda London
BABA: Kwanini?
DOGO: London nakupenda
BABA: Je, mi ningeenda London mama yako Dubai we ungeenda wapi?
DOGO: Ningeenda Dubai
BABA: Hee, unanikwepa unamfwata mama yako
DOGO: Hapana, London si ningekuwa nilishakwenda

MPENZI WA ARSENAL AKUTWA NA SURUALI KWENYE MAGOTI


19 February 2014

FISADI AJIKOJOLEA LAIV

Fisadi kaiba mkwanja akaona itakuwa soo akiuweka benki maana siku hizi mtu hata ukiweka hela zako Uswisi watu wananusa, akanunua sanduku akazisunda zile pesa, akaenda msitu wa Mabwepande akatafuta mti mkubwa akachimba shimo chini yake akafukia mkwanja. Ili awe na kumbukumbu akapiga picha ule mti akaondoka zake kuwahi ndege maana alikuwa kwenye msafara wa bosi mkuu. Akiwa hewani akaanza kuzicheki picha za ule mti aliofukia mkwanja wa wizi, duh kucheki picha vizuri si akamuona mtu yuko juu ya ule mti amtoa bonge ya tabasamu, mkojo ukamtoka palepale kwenye kiti cha ndege bila breki

SIO CASTRATION NILIKUWA NATAKA CIRCUMCISION

Kamjamaa kasmati smati flani, kalienda hospitali kwa aibu aibu kakamuona dokta; KAMJAMAA: Gud moning Dokta, I am serious problem of health DOKTA: Nini tena bwana mdogo? KAMJAMAA: I want castration operation DOKTA: Sikiliza, kwani hujui kiswahili? Hiyo operesheni sifanyi KAMJAMAA: Dokta unajua mambo mengine ni siri so I talk English Please do me castration DOKTA: Sitaki sioni sababu KAMJAMAA: Dokta I pay you 1 milion shilings, mzee nisaidie DOKTA: Dah haya japo kwa kweli sipendi kabisa we bado kijana ntakuwa nakuonea...Jamaa wakati kalala dokta akamfanyia operesheni aliyotaka. Alipoamka dokta akampa maelezo DOKTA: Sasa kama ulivyoagiza nimekufanyia castration  kama ulivyotaka, lakini nikagundua kuwa ulikuwa unatakiwa kuwa cirumcised pia kwa hiyo nimefanya hiyo pia KAMJAMAA: Dokta nilikosea kusema nilikuwa nataka hiyo ya pili tu

MKEO HAJUI KISWAHILI

MLEVI 1:Niambie ukweli , wewe ni kama ndugu yangu, hivi kwani watu mtaa huu wanamfwatafwata sana mke wangu?
MLEVI 2: Unasikia bradha mi ntakwambia ukweli. Mkeo ana matatizo hajui kiswahili sawasawa
MLEVI 1: Toka lini? Mke wangu anajua kiswahili vizuri sana
MLEVI 2: Kwa kweli bradha mke wako anajua maneno mengine ya kiswahili lakini hajui neno hapana

KIUKWELI KABISA HUYU JAMAA TULIMFUKUZA LIPULI


18 February 2014

ULIVYOTUANDIKIA UKASEMA UMEOA DEMU MMAREKANI HALAFU BLEKI, TUKADHANI..............

Aise ndugu yangu nashukuru kwa kunitumia picha ya shem, mara ya kwanza uliponiambia umemuoa Mmarekani tena  bleki, na jinsi ulivyomsifia, kwa kweli mawazo yangu yalikuwa umeopoa kitu cha nguvu kama vile Beyonce au mama Obama, sasa hii picha ya huyu shem imanivunja moyo, japo wahenga walisema kipenda roho kula nyama mbichi, najiuliza si ungekuja home tu kuna watoto wa nguvu sana wamejaa. Ushauri usije ukaja na shem huku, au akija mwambie avae baibui,
Ndimi Nduguyo Joni

UTAKUFA TU, HIYO NDUDE ITAKATIKA YENYEWE

Jamaa katika uhuni wake akakumbana na ugonjwa wa ajabu akavimba sehemu za siri, akaenda kwa daktari ambaye akamuangalia kwa makini; DAKTARI: Umetembelea nchi ya Malawi karibuni? JAMAA: Ndio dokta DAKTARI: Na ukalala na mtu huko? JAMAA: Ndio dokta DAKTARI: Basi umepata ugonjwa unaitwa NYASALIASIS JAMAA: Duh, dokta nisaidie nipone DAKTARI: Ni ngumu kidogo maana wote waliougua ugonjwa huu wanakufa , lakini sijui labda tufanye operesheni. JAMAA: Hakuna njia nyingine dokta, unajua hapo mahala pabaya, sasa kufanya operesheni dah DAKTARI: Jaribu sehemu nyingine lakini kwa kweli mi nadhani operesheni labda ingesaidia. Jamaa akatoka akaenda kwa mganga wa kienyeji JAMAA: Aise nimepimwa nimekutwa na NYASALIASIS, sasa dokta anasema watanifanyia operesheni....Mganga akamwambia avue nguo, nae akamcheki, akaanza kucheka sana JAMAA: Vipi mbona unanicheka? MGANGA: Unajua madaktari wenu bwana hili tatizo dogo wanazunguka eti wanataka kukufanyia operesheni, yanini operesheni? JAMAA: Utaweza kuniponesha? MGANGA: Hapana, ila hakuna haja ya operesheni, mbona hii baada ya wiki itakatika yenyewe.

MI NI KUKU MUDA MREFU SASA

MCHIZI: Unajua mimi ni kuku DOKTA: Okay ni lini ulianza kuwa kuku? MCHIZI: Muda mrefu tu, toka nilipokuwa yai

17 February 2014

MCHUNGAJI KANITEXT LEO HAKUNA IBADA

Jamaa alikuwa njiani anaenda kanisani, si akashtuka kukumbuka kuwa ameacha simu yake nyumbani. Haraka akageuza njia na kurudi  nyumbani, alipofika home presha ikiwa juu, jasho jembajemba likimtiririka, bahati nzuri akakuta mkewe hajaamka. Akaichukua simu yake na kuvunja safari ya kwenda kanisani akaanza kuangalia TV, mkewe alipoamka akamkuta jamaa kajaa tele sebuleni,
MKE: Jamani si nilidhani umeenda kanisani?
JAMAA: Mchungaji kanitext kasema leo hakuna ibada.

VICHWA VYA HABARI......................BAADA YA ARSENAL KUITOA LIVERPOOL............IKAANZA SHEREHE


15 February 2014

WATANZANIA TUCHUKUE FURSA YA KUFURAHIA GIZA

Blog yenu makini imekaa na kutafakari ikaona ni muhimu kuunga mkono juhudi za wasambaza giza, katika mradi wake wa kugawa giza. Tatizo ambalo blog hii imegundua baada ya kufanya utafiti wa kina wa muda mrefu ni kugundua kuwa watu wengi wanashindwa kutumia vizuri fursa nyeti ambazo wasambaza giza wameweza kuwapatia katika wiki za karibuni. Mhariri asiye mkuu wa blog hii ameona ni vyema kuonyesha uzalendo na kutoa msaada wa ufadhili wa tangazo kwa ajili ya taasisi yetu hii nyeti. Hivyo basi tangazo lifuatalo litatolewa bure ili wananchi wajue faida muhimu za giza.

NIPO ICU, ILA NIKITOKA HAPA KITAWAKA

Jana ghafla imeingia mesej kwenye simu yangu, toka kwa mywife wangu inasema,' Sweety mi nimechoka naona tuachane',wakati natafuta mahala pa kuegamie nisianguke kwa presha ikaingia nyingine 'Sorry love hiyo txt siyo yako' Nipo ICU

SIRUDI TENA GWANZHOU

Janfoi chu Li xu huan zhen feu zhech feng Lee.  Ming yao yeng kong hong king? Ming hao shu wein shao shing xhen yui wa.. Na kwa hiyo ndio hivyo tena, tukajikuta tuko kituoni mizigo yote imechukuliwa. Tsan kung fe ming tao li shi shuan Tanzania. Ndo Fulo aktoa msaada wa nauli, Gulo shing wha fung fung li , yaani Gulo ndio hamna kitu kabisa, si akaingia ule mtaa pale pa Wanaijeria akatokomea. Anyway tuko poa  sasa

14 February 2014

KIPIMO CHA UCHIZI

Juzi kwenye hivi vipindi vya TV ambavyo wadada wameshika hatamu kutangaza, na huwa wanawauliza watu mambo mengi tu nilisikia kali. Mdada alikuwa kamkaribisha daktari wa hospitali wa wagonjwa wa akili, ambaye alielezea kuwa mtu anaweza akaonekana mzima kabisa , lakini ukimuuliza maswali fulani rahisi ukaweza kujua kuwa mtu huyo ana matatizo ya akili;
MDADA: Daktari unaweza kutufahamisha ni maswali aina gani?
DAKTARI: Kwa mfano naweza kumuuliza mgonjwa swali la kihistoria kwa mfano nikasema,'Dr Livingstone alifanya safari tatu kwenda Ujiji na ndipo kifo kikamkuta, sasa je ni katika safari ya ngapi alipofariki?'
MDADA: (kwanza alicheka kidogo) Watazamaji hayo ndio aina ya maswali  ya dokta, mimi kwa kweli sikuwa mzuri sana kwa historia wakati niko shule, sina jibu ila nategemea watazamaji kuna wengi mmekwishapata jibu....sasa dokta huwa hamna maswali rahisi yanayohusu jamii tuliyonayo leo? (....nikahamisha chaneli)

PAKA KAFUNGWA DRAFT

Jamaa kaenda kumtembelea rafiki yake akamkuta anacheza draft na paka wake; JAMAA: Duh aise huyu paka wako wa ajabu ana akili sana anacheza draft? MWENYEJI: Hamna kitu hapo, nimeshamfunga mara tatu mfululizo huyu

13 February 2014

KIBIMBIF KIBAMBAF KIDANGANYA WATU

Luninga aka TV aka Kibimbifukibambafu kidanganyawatu ni kitu moja hatari sana. Siku hizi Kibimbifu ndio kimekuwa shule ya kila kitu. Kuvaa, kuongea, kuimba, kucheza, na siku hizi mpaka kulea.
Watu wanatengeneza video za singo zao kwa kukopi na kupest zile walizoona kwenye Kibimbifu, hata muvi zinatengenezwa baada ya wajanja wetu kuangalia muvi kwenye Kibimbifu, kasha kukopi na kupesti za kwao. Ila kali sasa ni wale jamaa zangu wanakopi na kupesti namna ya kulea watoto wao kwa kujifunza kwenye Kibimbifu.
Juzijuzi nilimtembelea rafiki yangu ambaye anajitahidi kuishi kama wale anaowaona kwenye Kibimbifu, sasa yeye ana kavulana kake kako nasari, nako anakalea kama vile vitoto vya kwenye Kibimbifu, na kwa vile kule nasari kamejifunza kutamka Dadi and Mami badala ya baba na mama, jamaa yangu anajiona mjaaaanja,  basi Kabwamdogo hako hakakaripiwi wala kukatazwa chochote, nilipata taarifa kuna siku kalimvua baba yake taulo alipokuwa katoka bafuni tena mbele za watu, jamaa akaishia kusema tu, ‘No Junia no, is bad” Na kucheka cheka huku akisifu, ‘Tatizo la huyu mtoto ni ana akili za kikubwa” Ene wei siku hiyo jamaa akanikaribisha kwake, basi kwa kweli ilikuwa kero, mara Junia kaleta mpira anaupiga mbele yetu anaangusha vitu, anatupiga usoni na mpira anaangaliwa tu, ‘Junia no’, anapanda meza mara kabati, jamaa zangu utadhani wamelogwa, wanakenua tu meno, ‘No Junia no” Mara mbili hivi kakaniparamia na kutaka kunivua miwani yangu, ‘Kwa ustaarabu wa nyumba ile na mie nikatoa ya kinafiki, ‘No Junia no’.  Bahati nzuri mama Junia akaingia jikoni, Baba Juni akaenda chumbani kidogo, sebuleni tukabaki mimi na hiki kidude kisichokuwa na chembe ya adabu. Si kikaanza vimaswali vya maudhi,’Leo umekuja kula kwetu?”  ‘Kwenu mna TV? Babako anakuleteaga chokoleti?” Kikawa mara kivunje kikombe mara glasi, mama yake anapiga kelele toka jikoni, ‘Junia yu a veri bed’. Ila chenyewe kikakosea kikanipanda kichwani na kuanza kunivuta nywele nikaona sasa hii zarau. Basi nilikishika mkono nikakitolea macho na kukifinya vizuri mgogongoni. Kwanza kilitoa macho kama kinataka kufa, kikaniangalia hakiamini akili yake kuwa kimefinywa na binadamu aliye hai, na mie nikakiambia kwa sauti ya chinichini,’We Junya ukinisogelea tena nakukata masikio’  E bwana we kilitimka mle sebuleni mkojo unakitirirka kikaelekea jikoni. Kufika huko nilitegemea kianze kulia kwa nguvu, kikawa kimya. Mama yake anakiuliza ’Junia umefanya nini tena baba?’  kimya “Junia what has happened?” kimya, mama yake akaja huku chenyewe kimejificha nyuma ya gauni la mamake,  ‘Huyu kafanya nini?’ Nikajibu kwa sauti ya mtu asiye na dhambi kabisa, ‘Wala sijui nimeona tu katimka hapa kaja huko’ Baada ya hapo kukawa na displin mle ndani tukala na kuzungumza bila fujo. Baba Junia kila mara akimwangalia mwanae na kumuuliza, ‘Junia a yu sik? Unaumwa?” Junia akinitupia jicho mwenyewe alikuwa ananyamaza anajua kuna kukatwa masikio. Wengine hatuangaliagi Kibimbifu ohooo

HEBU TUCHEKI MAGAZETINI KUNANI?

12 February 2014

UZEE HUO

JAMAA: Dokta sijisikii vizuri yaani nikiwa natembea macho yanaanza kuona vidotidoti
DOKTA: Uzee huo
JAMAA: Pia huwa nikiamka asubuhi mgongo unauma sana
DOKTA: Uzee huo
JAMAA: Kichwa pia huwa kinaniuma sana wakati wa mchana
DOKTA: Uzee huo
JAMAA: We dokta vipi kila ninalokwambia unanambia uzee huo, kama huwezi kunitibu nambie niende kutafuta matibabu kwingine
DOKTA: Unaona unavyowahi kukasirika ni wazi uzee huo

YAANI NI MUUJIZA UMETOKEA

Rafiki yangu mpenzi,
Nakuandikia barua hii lakini roho inanisuta najisikia vibaya sana, lakini tatizo nililonalo ndilo linanilazimisha nifanye hiki kitendo kinachoninyima raha. Kwa uchungu sana naomba unikopeshe shilingi laki tatu. Najua ni usumbufu, yaani hata kununua bahasha ya hii barua ninasita. Yaani ni kama nahisi Mungu aingilie kati usipate barua hii kusudi nisikuudhi. Nategemea jibu jema
C N K


 Dear Friend,
Yaani huu ni muujiza, Mungu kajibu ombi lako, kabla sijamaliza kusoma barua yako upepo mkali umeipuliza na barua ikapotea.
Ndimi Rafiki yako mpenzi. Hivi ulikuwa unataka nini?
King Mfalme

LOH MKE WANGU TUMESHAIBIWA

Wakati kesi inaendelea hakimu akawataka wazee wa baraza watoe ushauri;
HAKIMU; Wazee naomba mnipe ushauri kuhusu huyu mshtakiwa ili nitoe hukumu, lakini ningependa kuwashauri kuwa pamoja na kuwa maelezo aliyoyatoa polisi kuwa hayafanani na aliyoyasema mahakamani hilo lisiwe kikwazo. Kwa mfano wakati naingia hapa nilijikuta ghafla sina saa yangu ya dhahabu, nikawa nina uhakika nimeibiwa, lakini wakati kesi inaendelea nikakumbuka kumbe nimeiacha nyumbani kwenye drawer la kabati la nguo. Haya tuendelee....... Jioni hakimu akarudi nyumbani
MKE WA HAKIMU: Baba imekuwaje tena leo umetuma watu watatu kuja kufuata saa yako?
HAKIMU: Mi sijamtuma mtu yoyote
MKE WA HAKIMU: Haaa kaja mtu wa kwanza kasema umemtuma kuja kuchukua saa yako ya dhahabu tena kaelekeza kabisa kuwa iko ndani ya drawer  la kabati ya la nguo, mi nimempa, ila nikashangaa wakaja wengine wawili nikawambia mwenzao keshakuletea
HAKIMU: Loh mke wangu tumesha ibiwa

PARTY YA KUAGA UBACHELA

WIKI MOJA KABLA YA HARUSIII....
BWANAHARUSI MTARAJIWA : Kesho tuna party ya mabachela wenzangu kuniaga
BI HARUSI MTARAJIWA: Hizo party hakuna kitu zaidi ya pombe kali, na wanawake machangudoa uhuni mtupu unafanyika huko
BWANAHARUSI MTARAJIWA: Sio hivyo mi tutakunywa juis tu na kupata ushauri kwa wenzangu
BIHARUSI MTARAJIWA: Unanidanganya nini? Nimeshashiriki party nyingi za kuaga ubachela
BWANAHARUSI MTARAJIWA: Mungu wangu

11 February 2014

ACHA KELELE SIMU NIMEPIGIWA MIMI

Simu ililia saa nane usiku.....
MUME: Kama simu yangu wambie sipo....mke akapokea simu

MKE: Halooo ndio yupo hapa kalala pembeni yangu
MUME: We vipi mbona huelewi?
MKE: Bwana we acha kelele hiyo simu ilikuwa yangu sio yako

BREAKING NEEEEEEEEEEWSSSSSSSSS...TAMKO LA CHAMATA


Tamko kutoka Chama cha Maboifrend Tanzania (CHAMATA)
 Wapenzi wetu, wake zetu, nyumba ndogo zetu, samsing zetu, dogodogo zetu, kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wetu kama vile;
·      uchaguzi wa Madiwani katika kata 27
·      moto uliotokea mara kadhaa katika masoko ya Mbeya
·      majukumu ya mambo ya shule mwezi January
·      vipigo visivyoisha vya Manchester United
·      ukijumlisha na kipigo kibaya cha Arsenal dhidi ya Liverpool wiki iliyopita
·      kuhamishwa wa viongozi wa polisi karibuni
·      mtafaruku wa Zitto Kabwe na CHADEMA
·      vita vya Sudan Kusini
·      kuongezeka kwa rushwa
·      ujangili wa meno ya tembo
·      kukamatwa kwa shehena kubwa ya madawa ya kulevya
·      uteuzi wa Bunge la Katiba
·      kuongezeka kwa gharama za umeme
·      msongamano wa magari barabarani na mengine mengi sana
Tungependa kutoa taarifa mapema kwamba hatutashiriki wala kuwepo katika sherehe za Valentine mwaka huu.
Nchi yetu inahitaji kufunga na maombi wakati huu, na sisi, kama sehemu ya Taifa letu tumeamua kuwa katika mfungo wa kuombea nchi yetu kuanzia tarehe 12 hadi 16 February mwaka huu. Tunashauri na nyinyi mchukue muda huo mwafaka, kusherehekea Valentine na wazazi wenu kwani nao ni sehemu ya mapenzi ya Valentine.
Tunategemea kukutana nanyi tena tarehe 17 na tunashukuru kwa ushirikiano ambao tuna uhakika mtauonyesha katika kipindi hiki kigumu cha kuliombea taifa letu Tanzania

MWENYEKITI TAIFA
CHAMATA

10 February 2014

VIPI NIWATAARIFU MOCHWARI?

Jamaa alikuwa anafanya kazi mochwari, siku hiyo akaamka na bonge ya homa, akaenda na mkewe hospitali wakati anapimwa damu na nesi, mkewe akaona itakuwa vizuri kutaarifu kazini kwake kuwa anaumwa akamuuliza mumewe; 
MKE: Vipi niwataarifu mochwari? 
 NESI: He mwanamke una roho mbaya wewe, ondoa uchuro mume wako haumwi kiviiile

AFANDE NAOMBA PF 3

JAMAA kaingia kituo cha polisi huku anavuja damu kichwani; POLISI: Nini tena wewe? JAMAA: Naomba PF3 nikapate matibabu POLISI: Umefanya nini? JAMAA: Nimepasuka kichwa POLISI: Umepasukaje kichwa? JAMAA: Nilikuwa nambusu mpenzi wangu POLISI:Toka lini ukibusu mpenzi unapasuka kichwa? JAMAA: Mke wangu alinikuta nambusu

HATA WABONGO TUNAWEZA


DEVI KUONA KIMINI TU........................

Mdada mmoja mrembo sana, mwenye watoto wawili alikuwa kapewa talaka na mumewe akahamia nyumba aliyokuwa kapanga jamaa yangu DEVI. DEVI alipomuona mpangaji mpya roho yote ikamtoka. Akajitahidi kila njia kuonyesha kuwa yupo na ni bachela, mdada akawa anaendelea na shughuli zake bila hata kuonyesha dalili za kumwona DEVI. Jioni moja DEVI akiwa kapumzika akasikia hodi kwenye chumba chake, alipofungua akakutana uso kwa uso na mdada mpangaji, kapendeza sana na akiwa kavaa kimini cha nguvu;
MDADA: Samahani kaka Devi, yaani nimekaa muda mrefu mpweke nimeona leo lazima nitoke nikajirushe kidogo kisha nipate bwana niondoe uchovu. Vipi we uko free?
DEVI: Mimi sana tu niko free sina kitu chochote ninachofanya jioni hii, yaani niko free kabisa si unaona mwenyewe niko free sina ishu kabisaaa
MDADA: Loh nakushukuru sana kaka yangu, basi ngoja nikuletee watoto wangu ushinde nao mpaka ntakaporudi

ANAPIGA KELELE MPAKA NAAMKA

MWANAMIMI:Dokta tatizo langu kubwa sana
DOKTA: Nini tena?
MWANAMIMI: Usiku tukiwa faraga na mume wangu, huwa anapiga sana kelele
DOKTA: Lakini mama hilo ni jambo la kawaida
MWANAMIMI: Hapana ananisumbua, kelele zake huwa kubwa mpaka zinaniamsha usingizini

9 February 2014

NATEGEMEA KUIONA STAILI HII MTAANI KABLA MWEZI HAUJAISHA


KUNA BAR SINZA WANATOA WAPENZI BURE

MWANAKIJIJI 1: Aise nataka kwenda Dar
MWANAKIJIJI 2: Lazima ufike Sinza kuna baa inaitwa SHKAMOO
MWANAKIJIJI 1: Kwanini?
MWANAKIJIJI 2: Hapo ukiingia wanakupa kinywaji bure, halafu unapotoka unapewa mpenzi bure
MWANAKIJIJI 1: Dah huko lazima niende, we uliwahi kufika huko?
MWANAKIJIJI 2: Hapana lakini mke wangu kila akienda Dar lazima afike hapo

WIKI ENDI ILIKUWA TAMU SANA

Ilikuwa Jumamosi asubuhi, kazee kamjini kakaingia na kabinti kazuuri kwenye yard ya magari mapya.
KAZEE: Chagua gari unalotaka mpenzi....kabinti kakazunguka na kwa msaada wa mwenye wa mwenye yard kakapata Verrosa nyeupe nzuri sana.
MDADA: Mi naitaka hii
KAZEE: Hakuna tatizo kabisaaa, mtoto mzuri kama wewe lazima uwe una draiv mwenyewe.  Kakatoa kitabu cha cheki na kuandika cheki palepale na kumpa mwenye yard
MUUZAJI: Sasa mzee kwa kuwa umetoa cheki, gari utakuja chukua Jumatatu tukishahakikisha kuwa una pesa benki. Naomba  namba yako ya simu Mzee
KAZEE: Hilo nilijua. Haya twende zetu sweety Jumatatu tunakuja wote kuchukua gari lako..................Siku ya Jumatatu mwenye yard kampigia simu Mzee.
MUUZAJI: We mzee kavu sana, akaunti yako ilikuwa haina hata senti tano.
KAZEE: Hilo nilijua, lakini wiki endi yangu ilikuwa tamu sana.

KUHUSU ACCOUNT ZA MITANDAO ZINAZODAIWA KUWA NI ZA JOHN KITIME


Kumekuwa na kurasa (accounts) mbalimbali zenye jina la John Kitime, raia mzuri tu wa Tanzania katika mitandao ya kijamii Kama vile Facebook,Twitter,Instagram nk.

Zinazoonyesha kuwa mmiliki wake ni John Kitime.

Ukweli ni kwamba hizo kurasa zote zinamilikiwa na Bw Kitime.

Kwa maana hiyo chochote kinachoandikwa au kuchapishwa kwenye kurasa hizo,kinahusiana nae. 

Hata hivyo Bw Kitime anawashukuru wote wenye kuzipitia account hizo bila ya ruhusa yake, kwani anaamini wamesukumwa na mapenzi yao kwake.

Imetolewa na 
Ofisi ya Kitime
Iringa Mjini.

MKUTANISHE NA NYUMBA NDOGO YAKO

KITIME: Nataka nimfanyie mke wangu bonge ya suprise Valentine ya mwaka huu, sijui nimfanyie nini?
ABOUDONA: Mkutanishe na nyumba ndogo yako

KUONDOA HANGOVER SI MCHEZO, PATA KONGORO LA NGUVU ITASAIDIA


LEO JUMAPILI WATU WAKO KATIKA MAKANISA MBALIMBALI PAMOJA NA HILI


8 February 2014

ONYO MAWICHDOKTA WAMEANZA KUTIBU KIDIJITALI YAMENIKUTA LIVEE

Kwa kweli nilikutana na binti mmoja juzijuzi Njenje, roho ikanitoka. Kila nikitry kumkonyeza wala haniangalii. Nikamtuma weita amuulize anataka drink gani, kagoma kunywa chochote, nikaona problem yake ndogo, mji mzima umejaa matangazo ya waganga wanaoweza kukufanya upendwe. Nikamuendea mganga mmoja aliyedai anaweza kukufanya umpate mpenzi bila jasho, nikampa the whole ishu, witchdoctor akanambia dawa rahisi sana atanipa pete inaitwa Touch and follow. Ila nimtumie airtime ya shilingi alfu thelathini kwenye hendset yake. Haraka sana nikafanya hivyo nikakabidhiwa pete. Masharti rahisi sana kazi yangu ni kutafuta yule demu nihakikishe pete inamgusa tu atanifollow kila mahala. Basi nikamsaka demu nikamkuta Lango la Jiji anasikiliza Taarab, nikamgusa na pete  kisha nikatoka ukumbini kumsubiri, ngojaaa ngoja na wewe, dah hakuna cha kunifwata wala kunifollow. Nikasepa home nimenuna kishenzi.  Kufika home nafungua Whatsapp nicheki washkaji nikakuta demu kanifollow, kucheki Twitter kanifollow, Instagram, Tango, Badoo, Facebook kila mahala kanifollow duh. Kesho yake mapema nikaenda kwa mganga na kumpandishia, nikamuuliza mbona yule binti nimemgusa hakunifuata?. Nae kaja juu, 'We fala nini siku hizi mambo kidijitali. Huoni sikukuomba kuku wala mbuzi nimeomba unilipe airtime, na kwa hiyo huoni binti anakufwata kila mahala kidijitali? Hebu sepa" Nikawa mpole mwenyewe

TUWE SIRIAZ KWENYE PENZI LETU

MDADA: Mpenzi wangu mbona huwa hutabasamu hata kidogo ukiwa na mimi? MKAKA: Jamani si we mwenyewe ulisema unataka tuwe siriaz kwenye mapenzi yetu? Nikaona nikichekacheka utaniacha

MKIPATA DAWA NIPENI NIMPE NA BABA YAKE

MAMA: He mwalimu hujambo?
MWALIMU: Sijambo Mama Devi, tena bahati tumekutana ilikuwa tukutafute tuongee kuhusu Devi
MAMA: Nini tena huyu mtoto?
MWALIMU: Devi ana akili sana, lakini tatizo lake anapenda sana kuchokoza na kucheza na wasichana, hivyo waalimu tumeona tujaribu kutafuta dawa tumkomeshe hiyo tabia
MAMA: Yaani mwalimu mkipata hiyo dawa ntaiomba nimtibu baba yake, naye yuko hivyohivyo

BREAKING NEWSSSSS...BLOG YAPATA MUANDISHI MPYA TOKA TOSAMAGANGA

Yap ndugu zangu nimeamua kwa uamuzi wangu kuacha kazi nyingine nijiunge na blog hii kama mtafuta habari. Nilikuwa nafanya shughuli za kugema ulanzi maeneo ya Msombwe na Lupalama kule Tosamaganga, nimekuja Dar kuweza kufundisha uandishi ni nini. Na nategemea kuteuliwa kuwa mwandishi bora mwaka huu.  I know boss wa hii blog wafanyakazi wengine wanamuita mzigo kwa kuwa halipi mishahara, mi nina taktik ya kudai mshahara so naomba mnipokee.

7 February 2014

HUWEZI KUNIINGIZ MJINI MAL MBILI WE

Mtani kaja Dar akawa anazungukazunguka si ndio akafika chini ya ule mnara wa saa pale Samora. Wakati akizubaa anauangalia mgambo mmoja mjanjamjanja akamwendea;
MGAMBO: We mbona unaangalia sana saa kama unataka kununua?
MTANI: Kwan hii saa wanauza?
MGAMBO: Ndio na mimi ndie muhusika kama unataka sema
MTANI: Wanauz shing ngapi?
MGAMBO:Laki moja tu, Manispaa inataka kununua saa nyingine
MTANI: Hii hap Laki
MGAMBO: Sasa subiri hapo nilete ngazi tuishushe..........Mtani kangoja wee mwishowe akajua  kisha ingizwa mjini. Kesho yake akarudi tena pale pale
MGAMBO: Samahani sana, jana nilienda ofisini wakanambia kumbe wamepandisha bei ni shilingi laki na nusu hivyo ongeza hamsini
MTANI: Hamsini tu hizi hapa
MGAMBO: Haya naenda kuchukua ngazi tuishushe
MTANI: We, we, we, undhani unwez kun'danganya mara mbili. Baki wewe hap mi ndo naend kutafti ngazi leo.

AISEE HUJALOGWA WALA NINI HANA MVUTO HUYU

Jamaa kaenda kwa mzee moja kazini kwake;
JAMAA: Mzee nina tatizo kubwa yaani sina hamu na mke wangu kabisaaa,sijui nimelogwa?
MZEE: Kesho mlete mkeo nimuone................ Jamaa kesho yake akaja na mkewe. Mzee akamuangalia yule mama, kisha akamuita jamaa pembeni.
MZEE: Aise unajua najiuliza yaani ulimuoa vipi huyu? Mbona hana mvuto kabisa? Wewe hujalogwa wala nini

6 February 2014

HAHAHAHA ANATEMBEA NA CONDOM KWENYE POCHI

Walevi watatu wamkutana baa na baada ya vinywaji kadhaa wamekuwa marafiki wazuri wakaanza kuongea kuhusu wake zao;
MLEVI 1: Mi mke wangu hana akili kabisaa, hana TV lakini anatembea na rimoti kwenye pochi yake
MLEVI 2: Afadhali wako, mie wangu hajui kusoma lakini anatembea na novo kwenye pochi
MLEVI 3: Hahahaha hao wenu cha mtoto, wangu hana bwana lakini anatembea na kondom kwenye pochi

HAWATAKI NYAMA YA MBWA MI NIFANYEJE

Mjamaa alikwenda mji mmoja jina kapuni kumtembelea rafiki yake, chakula kikaja, akajikuta kapewa ugali na nyama nyingi na mwenyeji wake pia akapewa ugali na nyama nyingi, watoto na mke wakawa pembeni wanakula ugali na mboga za majani. Jamaa lika mtach lakini akanyamaza akapanga wakimaliza kula amuulize rafiki yake kwa nini anafanya uchoyo huu. Walipomaliza sahani zimekwisha tolewa na baada ya kunywa maji baridiiiiiii;
JAMAA: Aise sijapenda hii tabia, sisi tumekula ugali na nyama kibao mkeo na watoto wamekula mboga za majani bila hata kipande cha nyama
MWENYEJI:Mi sio kosa langu, wao wenyewe hawataki kabisa kula nyama ya mbwa, sasa mi nifanyeje?