HATUPIMI BANDO

27 January 2014

ZAMANI BINADAMU WALIKUWA NYANI?

DOGO: Mama hivi binadamu walitokea wapi?
MAMA: Kwanza kulikuweko na Adam na Hawa. Hawa ndio walikuwa wazazi wa kwanza wa binadamu, wakazaa watoto na watoto wao wakazaa ndio mpaka dunia ikajaa. (Dogo akaenda kwa baba yake)
DOGO: Baba hivi binadamu wametokea wapi?
BABA: Hapo zamani binadamu walikuwa nyani, wakabadilika taratibu na kuwa binadamu (Dogo akarudi kwa mama)
DOGO: Mama umenidanganya, baba amesema binadamu walikuwa nyani zamani
MAMA: Sijakudanganya, baba yako alikuwa anakuelezea historia ya ukoo wake

No comments: