HATUPIMI BANDO

11 January 2014

WE MKUBALI TU, KIKUBWA UHAI


Jamaa alitoroka jela ambako alikuwa kafungwa miaka 25. Nyumba ya kwanza aliyovunja akamkuta mtu na mkewe wamelala. Akawaamsha kwa vitisho kisha akawafunga kamba kwenye kitanda. Baada ya hapo akainama na kumnong’oneza kitu yule mke, kisha akaelekea bafuni. Wakati yuko huko mume akamwambia mkewe, ‘Sikiliza huyu jamaa ni wazi katoroka jela si unaona nguo zake? Sasa nimemuona anavyokuangalia, ili asituuwe chochote atakachotaka we mkubali tu, mridhishe hata kama kitakuwa kinakuchefua, itakuwa siri yetu kikubwa uhai. Nakuenda sana mke wangu’. Mke akajibu,’ Si umeona kaninong’oneza kitu? Alikuwa ananiambia jela kumemzoesha wanaume, na wewe kakupenda, kaenda bafuni kujitayarisha. Mume wangu ili asituuwe chochote atakachotaka we mkubali tu, mridhishe hata kama kitakuwa kinakuchefua, itakuwa siri yetu kikubwa ni uhai. Na mie nakupenda sana mume wangu”

No comments: