HATUPIMI BANDO

14 January 2014

USIOMBE KUFUMANIA OHOOO


Usiombe kufumania, narudia tea kwa lugha ya kileo, kufumnia ni soo.
 Nilishawahi kuweko kwenye kijiwe cha washkaji fulani kukawa na mjadala kuhusu kufumania. Swali likawa Je, ukifumania utafanya nini? Majibu yalikuwa mengi, mengine yenye uamuzi mgumu, ‘ohh mi ntaua’. ‘Ohh mi ntapiga mtu  mpaka kieleweke, ‘Ohh mi namuacha mpenzi wangu hapohapo asinijue tena’ , basi majibu yalikuwa mengi, mengine siwezi kuandika humu, kuna madogo wanasoma hii ishu.
Narudia tena usiombe kufumania, kuna jamaa, jina namhifadhi alipashwa habari na watu wenye kufwatafwata mambo ya watu kuwa mkewe ana nyumba ndogo, hahahahaha, kama unadhani wanaume tu wana nyumba ndogo basi ujue hujaufahamu huu mji. Basi jamaa akapewa taarifa kuwa mkewe ana nyumba ndogo, akaamua kwa ushauri usiofaa eti akafumanie. Akaseti mambo yake na siku ya siku akalengeshwa gest ambako kulikuwa kunafanyika usaliti, hakika akawabamba mkewe na nyumba ndogo yake wakiwa katika ulimwengu mwingine kabisa, jamaa akafanya vurugu kubwa sana pale, baadae kwa kelele akaanza kumsaili mkewe.
JAMAA: Mke wangu kweli unanifanyia mimi hivi kweli?
MKE: …macho chini akiwa kimyaaaa…jamaa aliyefumaniwa akatumia wasaa huu kukimbia akiwa na shuka la gesti tupu.
JAMAA: Mke wangu nijibu kwanini umenifanyia usaliti huu? Mapenzi yote niliyokuonyesha, mipango yote tuliyopanga, oohhhhh mamama weee……Jamaa si akaanza kulia mwenyewe……yaani mke wangu unanifanyia hivi mimi, kumbuka tulikotoka, mengi tuliyopitia ….Kimya kikapita mke akakohoa kidogo.
MKE: Mume wangu kwa kweli nakiri nimekudhalilisha sana, sasa kuna kitu naomba niseme
MUME: Yaani unajibu kihuni bila aibu, unajua naweza kukufanya chochote mimi?
MKE: Ndio mume wangu naomba uiruhusu niseme
MUME: Haya sema pumba zako halafu usikie neno langu mimi kama mwanaume.
MKE: Mume wangu mi naona nimekudhalilisha mno hivyo naomba nikitoka hapa hata kwako sirudi, nakubali wewe kuniacha kuanzia leo……Sekunde kama 120 zilipita kwa kimya kikuu, feni tu la gesti lilisikika.
MUME: Sasa mke wangu mbona unaenda mbali, mi sijaongelea hayo ya kuachana
MKE: Hapana hili jambo ni la aibu nimeamua niondoke ubaki na heshima na amani ya akili.
MUME: Ngoja kwanza mi sijafika huko mke wangu, kwanza hili ni kosa la kwanza. Wahenga walisema mwenye makosa husamehewa na mimi nimekusamehe
MKE: Mume wangu mimi ntashindwa kukuangalia machoni nitakuwa sina raha kabisa ukiwepo, aibu imenizidi
MUME: Hapana mke wangu mi nimesha kusamehe, yameisha twende tu nyumbani. Tusahau yaliyopiya tugange yajayo
MKE: Hapana mume wangu, leo mwisho naona aibu
MUME: Usinifanye hivi mke wangu, kosa lenyewe hili ni dogo tu…wakati huo mzee mzima machozi yameshaanza kumlenga
MKE: Mume wangu usijidanganye, hili litatusumbua tukiendelea kuishi pamoja
MUME: Pliz mke wangu yaishe, jifanye mimi sikuja , nisamehe mke wangu kwa kuja huku nisamehe chondechonde…chezea kufumania wewe ILITOKA PIA KATIKA GAZETI LA UWAZI

No comments: