HATUPIMI BANDO

27 January 2014

TANGAZO--ANAHITAJIKA MGANGA WA TIMU YETU, inafungwa hovyo hovyo

TANGAZO TANGAZO TANGAZO
Timu yetu ya soka ilikuwa kali kinoma, lakini katika kipindi hiki tumekuwa tunafungwa mfululizo a karibu na kila timu. Kama mashabikiwa damu,tumegundua kuwa timu yetu inalogwa sana ndio maana tunafungwa, kwa hiyo tumeamua kutangaza nafasi ya Mtaalamu Mkazi wa Timu.
Kazi ambazo Mtaalamu atalazimika kufanya ni zifuatazo;
- Kusafisha nyota ya timu ili tuweze kupata magoli
- kusafisha nyota ya kocha wetu mpya, maana kuna kitu katupiwa kinaleta mkosi
- kuhakikisha kila timu ikicheza inashinda
- kuvunja timu pinzani zisambaratike kabisa
Ili kupata mtaalam aliyebobea kutakua na usaili ambao utafanywa mwisho wa mwezi huu mbele ya viongozi wa mashabiki wa timu. Mtaalamu anaeona anaweza kufanya kazi hii atume maombi ili aelekezwe wapi aje kusailiwa.
KLABU YETU HOYEEEEEEEEEEEEEEEEE....

No comments: