PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NILIDHANI UMESEMA WEWE ULIKUWA YAYA

Binti alirudi kijijini baada ya miaka 5.
BABA: We mwanaharamu umeondoka hapa kwa miaka mitano hukutaka hata kutuandikia barua wala kutuma salamu unajua ulimtesa sana mama yako?
BINTI: Baba niliona niwe kimya nilikuwa nafanya kazi ya umalaya
BABA: Ayaaaaaa umetia aibu kubwa familia yangu lohh, ntatembelea wapi mimi? Kijiji chote watanicheka, kanisa litanitenga, loh jamani jamani. Ondoka hapa kijijini haraka sasa hivi
BINTI: Sawa baba, lakini nimemletea mama sanduku la nguo na kanga 20 na pesa, na hii hapa ni hati ya kiwanja nimemnunulia. Na wewe baba nimekununulia hilo Fuso nililokuja nalo na nimekufungulia akaunti benki, ina pesa utaweza kulima vizuri na kujenga nyumba nyingine ya kisasa, mwaka kesho nakuletea trekta.
BABA: Ulisema ulikuwa unafanya kazi gani?
BINTI: Umalaya
BABA: Unajua nilisikia vibaya nilidhani ulisema Uyaya, pole na kazi mwanangu

Comments