PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

NI KWELI ANA MDOMO KAMA TAIRI YA TREKTA

Mke alikwenda kulalamika kwa mumewe kuwa kuna jamaa mgeni jirani kamtukana kuwa ana mdomo kama tairi la trekta. Mume akapandisha na kuapa kutoa adhabu kali sana atakapokutana na huyo mshenzi. Siku walipokutana mume kanywea maana jamaa alikuwa baunsa wa ukweli;
MUME: Mambo jirani?
JIRANI: Mbona poa sana tu
MUME: Jirani nasikia ulimtukana mke wangu kuwa ana mdomo kama tairi la trekta
JIRANI: Ndio
MUME: Ahahha, tairi la mbele au la nyuma?
JIRANI: La nyuma
MUME
: Ahaa nilidhani ulisema la mbele, inaonekana mimi na wewe tunawaza sawa, ila tu sijamwambia wife, si unajua akina mama wanavyoweza kupanik.

Comments