MWANANGU KAOLEWA NA JAMAA MTARATIBU SANAAkina mama wawili waliosoma pamoja walikutana sokoni baada ya salamu;
ISABELA: Jamani Adela vipi mwanao?
ADELA: Kwa kweli mwanangu kaoa mwanamke mchawi, kamloga kamuinamisha mwanangu, we fikiria, mwanamke anaamka saa 5, akiamka hapo ni kuzurula mji mzima kutumia pesa za mwanangu, mwanangu akirudi kachoka jioni, hakuti chakula, badala yake hao wanaenda kula kwenye mahoteli ya gharama, yaani we acha tu. Vipi binti yako?
ISABELA: Mtoto wangu kaolewa na mwanaume mtaratibu sana, na mpole sana, anaamka alfajiri anamtengenezea binti yangu chai anamletea chumbani, anamuachia pesa nyingi za kutumia kwenda kununua anachotaka, kila siku akirudi anampeleka kula kwenye hoteli za gharama maisha yao kwa kweli mazuri sana

No comments:

Post Top Ad

Powered by Blogger.