PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

MINYA SEND, MINYA SEND

Jamaa mmoja kwa muda mrefu alikuwa anamfukuzia binti mmoja mrembo  na kila mara alikuwa anatolewa nje na yule binti kwa visingizio mbalimbali, hatimae siku moja wakati yumo kwenye taxi mitaa ya Tandale, mesej ikaingia ilikuwa inatoka kwa yule binti mrembo imeandikwa hivi, 'Kwa kweli sasa nimeamini unanipenda kweli, maana ni muda sasa umeonyesha nia ya kuwa nami bila kuchoka. Naomba uje kwangu jioni ya leo, je nikutegemee?'. Jamaa kwa furaha kubwa akajibu, "Ndiyo'.  Kabla hajaminya send kibaka mmoja akaipitia ile simu kama mwewe. Jamaa akabaki kupiga kelele, 'Minya send, minya send"

Comments