PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

MIKUBWA MIZIMA MNAOGOPA BINDUKI YA KUCHEZEA

Majambazi yaliingia katika nyumba moja kuiba. Mwenye nyumba akaamka na kwa ujasiri mkubwa akachukua bunduki ya kuchezea ya mwanae na kuwatisha majambazi wenyewe wakawa wapole, akawaketisha chini, na kuanza kupigia simu polisi. Wakati mzee anaita polisi huku akiwalenga majambazi kwa ile pisto ambayo wao walidhani ni ya kweli, mtoto wa mwenye nyumba akaamka;
DOGO: Baba nataka kwenda chooni
BABA: Nenda tu mi nimewakamata hawa wezi nangojea polisi waje
DOGO: Haoooo mikubwa mizima mnaogopa binduki yangu ya kuchezea......baba mkojo ukamtoka ghafla

Comments