PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

KWA WATENDA DHAMBI TUU


Kuna watu huwa wanajifanya wajanja lakini ujanja wao ndio kifo chao halafu huwa hawajifunzi kila anapojifanya mjanja anakula za uso lakini utakuta hakomi wala habadiliki.  Jamaa yangu fulani baada ya kufa, na kutokana na midhambi yake mingi aliyokuwa akiitenda hapa duniani, akaenda moja kwa moja motoni. Kufika kule shetani akamkaribisha vizuri ila akamwambia kuwa pale kuna vyumba vyenye adhabu tofauti, jamaa yangu akaambiwa azunguke zunguke  aingie kila chumba achague adhabu anayotaka na ndiyo itakuwa adhabu yake  milele.
Jamaa yangu akaona duh kumbe mambo fresh anaweza akapata kaadhabu ambako kidogo kana nafuu, basi  kachungulia chumba cha kwanza kakuta watu wanakula mijeledi kwa kwenda mbele, mijeledi yenyewe imewekwa mizumari halafu imechovya kwenye tindikali, akaona hakufai maana kilio cha jamaa kilikuwa kikubwa. Akachungulia chumba cha pili kakuta watu wako vichwa chini miguu juu, lakini hapo chini ni misumari mitupu, tena misumari yenye moto, wanaumia wanalia na kulaani dhambi walizofanya,  akachungulia chumba kingine kakuta watu huko wako vichwa chini miguu juu na hapo chini moto unawaka vichwa viko kwenye moto, akakimbia haraka . Alipochungulia chumba kilichofuata si akakuta watu wamesimama wanatia stori wengine wanavuta fegi, wengine sigara kubwa, wengine bia mkononi, masupasta wakiume na kike kibao, rafiki zake wanawake kwa wanaume wakitia stori basi raha tu, lakini kulikuwa na harufu mbaya sana kwani walikuwa wamesimama kwenye mfereji wa maji yaliyotoka kwenye vyoo vyote kule motoni. Maji machafu ajabu yamefika kwenye magoti. Ukiondoa maudhi hayo mambo yalikuwa fresh sana.  Jamaa yangu si akaona heri ajiunge adhabu hii maana japo inaudhi  lakini ina starehe. Ile kuingia tu kakutana na jamaa wengi wakamkaribisha kinywaji, kabla hajamaliza hata chupa moja, kengele ikalia na kukatolewa tangazo kwenye spika, “Haya mapumziko kwa sasa yameisha. Mapumziko mengine ni baada ya miaka miaka mia sita, haya wote rudieni hali mliokuwa ya vichwa chini miguu juu………….

Comments