PAKUA HAPA ANKO KITIME APP

BREAKING NEWSSSSSSSS AUKOSA UWAZIRI ATOSWA NA NYUMBA NDOGO

Katika hali ya kusikitisha bosi wetu wa Blog hii ambaye kwa muda mrefu alikuwa akitamba kwenye mabaa kuwa lazima atateuliwa kuwa Waziri, na hata akaweza kupata nyumba ndogo kwa mtaji huo, amejikuta akitupiwa virago vyake toka kwenye nyumba aliyompangishia nyumba ndogo huyo. Bosi wetu huyo ambaye na blog nayo imemfukuza kazi,kwa kuwa ilionekana angekuwa Waziri blog hii ndio ingekuwa Blog ya Taifa. Blog imejikuta ikipoteza ndoto hiyo siku ambayo Manchester United, timu pendwa ya blog hii ikilambwa 3 -1. Hivyo kisirani cha kukosekana kwa mfanya kazi Waziri na Man U kupakatwa, kimesababisha jamaa afukuzwe kazi na mabosi wenzie tena hadharani.
Asante kwa kupoteza muda kusoma hii ishu

Comments